Heka heka langoni mwa Timu ya Netiboli Polisi Pwani waliopambana na wenzao wa Polisi Arusha, hata hivyo Polisi Pwani walishinda mabao 21-13.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Adolfina Chialo, akitoa hotuba ya kufunga mashindano ya ligi daraja la pili ngazi ya taifa netiboli kutafuta timu za kupanda daraja la kwanza msimu huu.
Timu ya mpira wa Netiboli ya Hamambe ya Mbeya wakishangilkia ushindi wa kuoanda ligi daraja la kwanza msimu wa mwaka huu .
Bechi la wachezaji wa timu ya Netiboli ya Tigo wakati wa mchezo wao na Ruangwa na kufungwa bao 37-26.
Picha ya pamoja kati ya timu ya Netiboli Polisi Arusha ( machungwa) na Polisi Pwani ( msimbazi) wakiwa na viongozi na waamuzi wao siku ya Feb 24, 2011.

Na John Nditi, Morogoro

TIMU tano kati ya nane za Mpira wa Netiboli zilizokuwa zikishiriki kinyang’anyiro cha ligi daraja la Pili ngazi ya Taifa hatua ya nane bora , kwenye uwanja wa Jamhuri wa mjini hapa, zimefuzu kupanda ligi daraja la kwanza msimu wa mwaka huu.

Zilizofanikiwa kupanda msimu wa mwaka huu ni timu ya Hamambe ya kutoka Jiji la Mbeya, Polisi Arusha, Polisi Pwani, Ruvu JKT na Alliance One ya Mkoani Morogoro.

Akitangaza matokeo ya kupanda wa timu hizo mbele ya mgeni rasmi, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Adolfina Chialo, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Mpira wa Netiboli Tanzania ( CHANETA), Shiza Mwakatundu, alisema ligi hiyo imeendeshwa kwa ugumu kutokana na ukosefu wa fedha na kuzifanya timu zilizishiriki kuwa 11 badala ya 18.

Mahindano hayo yalianza kutimua vumbi kwenye uwanja wa Jamhuri kuanzia Februari 16 na kushirikisha timu hiyo 11 , ambapo yalifikia tamati juzi ( Feb 24) .

Kwa mujibu wa Mjumbe huyo wa Kamati ya Utendaji ya Chaneta, pamoja na kuzitaja timu hizo tano kuweza kupanda daraja la kwanza msimu wa mwaka huu, pia alizitaja timu zinazoendelea kubaki ligi daraja la pili ngazi ya taifa ni Ruangwa ya Lindi na Tigo ya Jijiji Dar es Salaam.

Timu nyingine ni pamoja na Tandahimba kutoka Mtwara, Tupendane ya Lindi , Mzinga kutoka Mkoa wa Morogoro na Black Sisters ya Mkoa wa Pwani.

Hata hivyo alisema, ligi daraja la kwanza inatarajia kuanza mwenzi Agosti mwaka huu Mkoani Arusha na kuzitaka timu zilizipanda na zilizokuwepo kwenye ligi hiyo kudhibitisha ushiriki wao hadi ifikapo Juni 30, mwaka huu.

“ nazipongeza timu zilizofunzu kupanda ligi daraja la kwanza na zote zilizoshiriki ligi daraja la pili ngazi ya taifa mwaka huu , licha ya timu nyingi kukabiliwa na matatizo mengi yakiwemo ya ukosefu wa fedha “ alisema Mwakatundu.

Naye Mgeni rasmi Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Chialo, akifunga mashindano ya ligi hiyo, amewaomba wadau wa michezo kujitokeza kufadhili mchezo wa netiboli sawa na mchezo wa mpira wa miguu ili kuuendeleza mchezo huo.

Hata hivyo aliwataka wachezaji na viongozi wa timu zinazoshiriki michezo nchini, kuondokana na dhana iliyokua ikitumiwa zamani ya timu kwenda kulala makaburini ili ipate ushindi kuwa fikra hizo zimepitwa na wakati.

“ sasa hivi ushindi wa timu yoyote ni mazoezi ya timu na si vinginevyo …lazima mfanye mazoezi kwa bidii ndipo ushindi unatokea …lakini pia ninazipongeza timu zote zilizoshiriki waliodhinda waongeze bidii wasirudi tena nyuma na walioshindwa jipangeni upya ili mpate mafanikio mwaka ujao” alisema Chialo.

Katika michezo wa kufunda dimba ya mashindano ya ligi hiyo, timu ya Polisi Pwani iliweza kuwafunga ndugu zao wa Polisi Arusha mabao 21-13 hadi kipindi cha mapunziko , Polisi Pwani walikuwa mbele mabao 8-7.

Hata hivyo michezo mingine mitatu ya ya kuhitimisha ligi hiyo iliyofanyika asubuhi ya siku hiyo, timu ya Ruvu JKT ilishinda mabao 16- 13, Hamambe ya Mbeya iliifuga timu ya Tandahimba ya Mtwara mabao 41-17 na Ruangwa kuibuka na ushindi wa mabao 37-26.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...