Mwenyekiti wa Baraza la michezo nchini Kanali Mstaafu Iddi Kipingu akikabidhi bendera ya Taifa kwa manahodha wa timu za kikapu za Taifa (wanawake na wanaume) tayari kwa safari ya kwenda nchini Rwanda kushiriki mashindano ya kanda ya tano kwa nchi za Afrika mashari na kati mashindano yataanza Februari 7 hadi 12 mwaka huu. Timu hiyo imeondoka kwa basi la jeshi baada ya kukosa wafadhili wa kuwapa tiketi za ndege. Pia hali ya kambi ilikuwa tete kwa kukosekana pesa za kutosha. Gharama ya safari imetajwa kuwa milioni 40. Picha na John Bukuku

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Sasa jamani hii michezo naona imeingiliwa na Siasa "hali ya kambi ilikuwa tete" sasa tunaenda kufanya nini kwenye mshindano?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...