Kocha Sam Timbe kutoka Uganda akitangazwa kwa waandishi wa habari jijini Dar. Kulia ni msemaji wa Yanga Louis Sendeu. Klabu ya hiyo ya mtaa wa Twiga na Jangwani imemtangaza kocha Sam Timbe kuchukua mikoba ya kocha toka Serbia Papic ambaye ameingia mitini. Hata hivyo Timbe bado hajasaini mkataba na ameahidi kufanya hivyo Jumatatu. Kocha huyo amesema ameangalia mechi mbili za Yanga dhidi ya Dedebit na Mtibwa na amegundua kuwa wachezaji wa Yanga ni wavivu hawajitumi kutafuta mipira ,ataanza na kurekebishaudhaifu huo.Tangu kuondoka kwa Papic klabu ya Yanga ilikuwa chini ya kocha Fred Felix Minziro ambaye hajabahatika kushinda katika mechi mbili alizosimamia. Picha na Jane John
Home
Unlabelled
sam timbe atambulishwa kuwa kocha mpya wa yanga
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...