Balozi wetu Marekani Mh. Mwanaidi Sinare Maajar akiwa na kamati ya muda ya jumuiya kuratibu katiba itakayounda jumuiya ya watanzania Washington DC Metro katika mkutano wao mwishoni mwa wiki hapo DC
Mwenyekiti wa kamati ya muda akitoa shukrani kwa wana Metro
Ukumbi ulinoga

Na Sunday Shomari
Pamoja na mambo mengine, Balozi wetu Marekani Mh Mwanaidi Maajar aliwasifu Watanzania wa Washington DC Metro kwa kuunda kamati ya muda itayopelekea kuundwa kwa jumuiya rasmi itayounganisha wadau wote. Pia alitoa nafasi ya watanzania hao kuweza kwenda kumwona ofisini kwake kila Jumanne na kufanikisha uchaguzi wa kamati ya katiba ya jumuiya ya watanzania.

Aidha mh. Balozi aliwataka maafisa wake wa ubalozi kujitambulisha kwa Watanzania wenzao na pia kutoa mawasiliano yao wazi ikiwemo simu na barua pepe na kuweka bayana kuwa milango ya mawasiliano kati ya ubalozi na watanzania iko wazi.

Balozi pia alikuwa wa kwanza kutoa mawasiliano yake wazi mbele ya watanzania wa Washington Dc ikiwemo mpaka nambari yake ya mkononi kitu ambacho hakijawahi kuonekana.

Kwa picha zaidi za Washington DC

BOFYA HAPA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...