Waziri wa Uchukuzi Mh. Omary Nundu (kaunda suti kijivu) akitembelea bandari ya Bukoba iliyoko katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera leo. Wengine mwenye miwani ni mstahiki meya wa manispaa ya Bukoba Mh. Anatory Amani na aliyevaa suti ya mikono mifupi ni mkuu wa wilaya ya Bukoba pia kaimu mkuu wa mkoa wa Kagera Mh. Samwel Kamote. Picha na Audax Mutiganzi,Bukoba

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Huyu mpiga picha anahitaji shule ya nguvu ya namna ya kufyatua taswira nzuri na zinazoonekana kwa uwazi zaidi. Pia anahitaji kamera inayoendana na kazi yake badala ya hiyo ya matumizi ya nyumbani
    Hii taswira mbali na kutaja majina ya waliomo bado haipendezi/haionekani vizuri kwa wasomaji.
    Mtindo huu wa taswira ni wa mwaka 47.
    Naishia hapa kwani naogopa kuchafua hali ya hewa.
    NB:
    Ankal, please usiibanie kwani nimejitahidi sana kujiheshimu mbali na kwamba nina hasira za picha mbovu.

    Abiola Jr. - Mikanjuni, Tanga

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...