Na Woinde Shizza,wa Globu ya Jamii - Arusha

Wananchi ambao wanaenda kupata dawa kwa mchungaji Ambilikile Mwasapili wa kanisa la kiinjili na la Kilutheri Tanzania ambaye amerudishwa kazini mara baada ya kugundua dawa inayosemekana inatibu ya magonjwa sugu wametakiwa kufikisha taarifa zozote mbaya watazofanyiwa na madereva kwenye vyombo vya dola.

Hayo yamesemwa na kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha, Bw. Akili Mpwapwa wakati akiongea na waandaishi wa habari ofisini kwake.

Alisema kuwa wameamua kusema hivyo kutokana na malalamiko ambayo yamekuwa yakitokea ikiwa ni pamoja na madereva wa magari yanayowapeleka watu loliondo kwa babu kuwaacha abiria wao.

"tumeamua kufikia hatua hiyo kutokana na wananchi wengi kuachwa na magari ambayo yanawapeleka na kibaya zaidi hawa madereva unakutwa wameshalipwa nauli ya kwenda na kurudi"alisema Mpwapwa.

Alisema kuwa kwa kila abiria wanatakiwa ashike gari namba za gari ambalo ameenda nalo ili iwapo tatizo lolote litatokea basi iwe rahisi kulipata gari hilo.

Alibainisha kuwa kwa kila abiria ambaye atakuwa anaenda loliondo kupata dawa anatakiwa adai tiketi yake mapema ili iwapo tatizo litatokea awe na tiketi yake ya gari ambalo amelipanda.

Aidha alisea kuwa mpaka sasa kuna baadhi ya madereva wameshafikishwa mahakamani kwa makosa mbalimbali ambayo wamewafanyia abiria waliokuwa wakienda Loliondo kupata kikombe kwa Babu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. nchi inahamia kwa mganga

    ReplyDelete
  2. foleni ya msongamano wa magari na watu inaonekana anaeenda kwa miguu atafika haraka kuliko anaesubir trafik imove

    ReplyDelete
  3. Huyo Polisi kashakunywa na ndiyo sababu nawajibika, wewe angalia viongozi owte waliokwenda kwa baba wanawajibika kwa sasa. Karibu bunge zimalitakwenda kwa baabu utaoba watu wanawajibika sasa.

    ReplyDelete
  4. we unaesema mganga inaelekea ushazoe kwenda kwa waganga,na utabaki hivyohivyo wenzako ndo twanywa dawa kwa raha zetuuuu!ushasikia babu anataka jogoo fala weee embu tupisha kaa na imani yako ya kichawi mwisho wa siku plate namba utaisoma!!!!

    ReplyDelete
  5. Mkoloni mmoja alisema "You can take the african from the bush but you cannot take the bush from the African". Huu ni mfano halisi.

    ReplyDelete
  6. uganga wa kienyeji ndio, kwani hiyo sibitali?

    ReplyDelete
  7. Jamani hii inaonyesha wazi jinsi nchi yetu bado tuko nyuma sana, na hii ni aibu kubwa hata kujionyesha mapicha haya. Huyu Mchungaji kama mkweli au si mkweli ataleta madhara kwa jamiii. Serekali amka, Viongozi woote amkeni. Babu apelekwe mahala rahisi kufika mfano arusha mjini au mji wowote atakao, na awe na kituo/Vituo maalum na watu sasa waende kwa mpangilio, ikibidi ianzishe taratibu ya kumwona kwa ahadi.. Hili ni wazo maana kwa kweli mwisho wa hii hali tutakuja juuuuta, tutapoteza ndugu, jamaa, marafiki na imani zetu zitazidi kuwa duniii, hata Mwenyezi Mungu tena hatopenda!
    By Mamkubwa -2011

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...