CCM Manchester inapenda kutoa shukrani zao za dhati kwa wanachama wote na wanajumuiya wa Manchester na vitongoji vyake pamoja na uongozi wa CCM UK, Jumuiya ya Watanzania UK, Wananchama wote wa CCM miji mbalimbali, Watanzania wote UK bila kusahau jumuiya ya Wasomali Manchester kwa kushiriki kwa hali na mali kuweza fanikisha mazishi ya kada wetu wa CCM, kaka yetu, ndugu yetu Modibo Keita alietangulia mbele ya haki.
Tunawashukuru sana kwa kujitokeza kwenu na kuweza kufanikisha swala zima la mazishi ya ndugu yetu huyo.
Mungu amlaze mahali pema peponi ndugu yetu Modibo Keita.
Amin.
Uongozi CCM Manchester
Tunawashukuru sana kwa kujitokeza kwenu na kuweza kufanikisha swala zima la mazishi ya ndugu yetu huyo.
Mungu amlaze mahali pema peponi ndugu yetu Modibo Keita.
Amin.
Uongozi CCM Manchester
Ingependeza kama ungeshukuru wale wote waliofanikisha mazishi ya ndugu Keita, sisi wengine hatuna itikadi za KiCCM ila tulikuwepo
ReplyDeleteMdau Manchester
Umoja na Upendo ulio onyeshwa Manchester wakati wa mazishi ya aliyekua mpiganaji wa maendeleo ya jumuiya yetu kama Watanzania, ni wa kupongezwa na kuigwa.
ReplyDeleteWazee,vijana,watoto waume kwa wake toka Manchester na mikoa mbalimbali ya UK hamkusita kuacha kazi na majukumu yenu ili kushiriki kumpa heshima na hifadhi ya mwisho ndugu yetu Keita Denis:HONGERA SANA.
MUNGU AWABARIKI.
MAINA ANG'IELA OWINO
UK