Meli ya kivita ya Uingereza ikishambulia Libya kwa makombora asubuhi hii

Habari za kimataifa zinasema Uingereza, Marekani na Ufaransa mapema afajiri ya leo zimeishambulia Libya kwa makombora katika awamu yao ya kwanza ya pamoja kutaka kumng’oa kiongozi wa nchi hiyo, Kanali Muammar Gaddafi.

Hatua hii imechukuliwa masaa machache baada ya mataifa hayo makubwa kukutana kumjadili Kanali Gaddafi ambaye amegoma kuacha kushambulia waasi wa nchi yake, huku akiapa kupigana hadi mtu wa mwisho.

Maafisa wa Pentagon wamethibitisha mashambulizi hayo na kusema Marekani na Uingereza wamerusha makombora zaidi ya 110, wakati ndege za kivita za Ufaransa zikishambulia majeshi ya Gaddafi yaliyokuwa yanapambana na waasi wanaoshikilia mji wa Benghazi.

Kanali Gaddafi amesema hana mchecheto na atajibu mashambulizi, akiongezea kwamba atafungulia maghala ya silaha kwa watu wake ili kuihami Libya, wakati makombora ya Marekani na Uingereza yakishambulia makambi ya jeshi katika mji mkuu wa Tripoli na Misrata.

Ndege ya kivita ya Ufaransa ndio iliyofyatua risasi ya kwanza dhidi ya Libya mnamo saa 10.45 alfajiri, na kuharibu magari kadhaa ya kijeshi ya Libya.

Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. David Cameron amethinitisha asubuhi hii kwamba ndege za kivita za nchi yake ziko kwenye mapambano nchini Libya.

Rais waq Marekani Bw. Barack Obama akiongea akiwa ziarani Brazil, amesema nchbi yake inachukua hatua kiasi sana za kivita ikiwa ni sehemu ya muungano wa mataifa hayo katika kumng’oa Kanali Gaddafi.

“Hatuwezi kukaa kando wakati kuna mwendawazimu anayewaambia wananchi wake kwamba hakutakuwa na huruma”, alisema Bw. Obama, na kusisitiza Marekani majeshi ya ardhini ya Marekani hayatoshiriki kwenye mpambano huo.

Baada ya mashambulizi ya alfajiri hii, Kanali Gaddafi ametoa hotuba fupi kuwataka wananchi wake wajibu mashambulizi, na kusema vyombo vya kiraia vya angani na majini katka bahari ya Sham vyote viko katika hatari kubwa..

“Maghala ya silaha yamefunguliwa na wananchi wanapewa kila aina ya silaha kulinda uhuru, umoja na heshima ya Libya”, ametahadharisha Kanali Gaddafi.

Baadaye, televisheni ya taifa ya Libya imetangaza kuwa watu 48 wameuwawa na wengine 150 wamejeruhiwa katika shambulio hilo. Bado hakujawa na uthibitisho toka kwa chanzo huru cha habari hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Uonezi na ugandamizaji wa nchi za Ulimwengu wa tatu!! Hawa jamaa wanatumia nguvu zao vibaya. Waarabu na Waislam kwa ujumla amkeni!

    ReplyDelete
  2. Nchi kama Uingereza imeanguka sana kiuchumi, wanafanya Cut kila sekta ya serikali to save money, the only option s to wedge war on rich oil country kama LIBYA, they will be able to secure new oil agreements' with REBEL @ Cheap price, this is oil war, na waarabu ni wanafiki they are not united, Mzungu is a greed creture, atawaonyesha sasa,. watch out.

    ReplyDelete
  3. sioni ni suala la udini hapa eti waislam amkeni.mtu mwenyewe anauwa hao waislam wenzake kama ktu cha kawaida sa waamke ili waendelee kunjinjwa au?its time to go.aende zake huyo nchi siyo kitu binafsi cha mtu au familia.

    ReplyDelete
  4. waingereza na wamarekani wanaendeleza mipango yao michafu wao ndo walowapiga jeki akina osama na watalebani sasa wanawaunga mkono waislamu wa siasa kali ambao wanataka sheria law na sheria law inagandamiza wasio waislamu . it will cost them kwani waislamu wengi watakimbilia ulaya kwa gia ya mapigano na kuwa serikali za kiislam zinaonea watawakaribisha watalebani kwao wawabomu vizuri.

    ReplyDelete
  5. wa libya watakoma! wao wanadhani eti mzungu ataingia libya kusaidia? never... mzungu atakachofanya ni kwenda kujuwa wapi adhibiti ili achukue utajiri wote wa libya na si vinginevyo. wazungu ni watu wa maslahi sana. si bure na wao ndiyo wamewachonganisha. tukiangalia kwa makini huu uamuzi wa haraka haraka waliouchukuwa wa kwenda kupiga Gadaffi ni kwa sababu Libya ni nchi tajiri sana. je wanaweza kuchukuwa huo uamuzi kwa kwenda kutatua shida kama za tanzania? never... why? watawin nini Tanzania? hakuna. waje waitoe na CCM iliyotawala tangu miaka hiyoooooooo na kamwe haitokubali kutoka. mdau juu kwa juu

    ReplyDelete
  6. UKOLONI BABU MPYA
    Nakubali raia walikuwa na malalamiko,
    Nakubali viongozi walikuwa viziwi
    Kuna methali ya jirani aliyemshambulia babamtu kwa kuwa alimuonea sana mkewe,lakini jirani huyo alikuwa na mawazo mengine kabisa, na sio kuondosha ugomvi baina ya mtu na mkewe
    It will take a couple of generations before we wake up
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  7. ni jambo la kusikitisha sana mbona ivory coast,congo au nchi kibao za kibantu hamna chochote kilicho fanyika faster faster kama huko libya ni kwa sababu sisi ni watu weusi na mtu mweusi kwa mzungu hana samani kabisa yaani hilo lazima tulitie kichwani.wazungu wanatutenganisha na kutugombanisha kwa manufaa yao,wameanguka kiuchumi sana sasa hawana njia nyingine zaidi yakupigana vita na kuiba rasili mali za wenzao. kwa nini sisi wa waafrica tusiwi kitu kimoja?
    na hao wunzungu ndo wako behind ya conflits chafu chafu bara la africa alafu wanasema human rigths.sasa naona ukoloni karibuni unarudi africa na sio muda mrefu labda baada ya miaka mitano hivi watakuwa na full utawala africa.sasa ndugu zangu waafrica kweli tukubali hawa wazungu waje kututawala tena? matukio ya utawala sisi wote tunayajuwa so time is up! mdau toka bujumbura

    ReplyDelete
  8. HAPA NDIO MUJIULIZE MBONA ZIMBABWE HAWAENDI SABABU ZIMBABWE HAKUNA KITU KUMEBAKI MAHINDI TU AMBAYO USA WANAYO...

    GADDAFI NDIO KIONGOZI PEKEE ANAENDA NCHI ZA NJE ANAVAA NGUO YENYE NEMBO YA AFRICA ANASAIDIA AFRICA BILA KUTAKA KITU APEWE..

    KAMA UKATILI HAPO HATA NCHI ZA NJE ZIMETUMIA MAGUVU WAMEPANDISHIWA MAFUTA WANAHENYA...

    HAPA NDIO TANZANIA TUJIULIZE TUNAFANYA NINI KWENYE JUMUIYA YA MADOLA WAKATI HAKUNA FAIDA YOYOTE TUNAYOPATA JUMUIYA YA MADOLA?

    MAANA YA JUMUIYA YA MADOLA NI KWAMBA BADO TUPO KWENYE UTAWALA WA BRITISH NDOMANA SHERIA ZA TANZANIA NI ZA KI BRITISH.

    AFRICA UNION INAFANYA NINI HAITETEI UTETEZI WA KUINGILIWA AFRICA NAMNA HIYO? KZ.

    ReplyDelete
  9. Kuna faida nyingi za jumuiya ya madola kama
    - scholarship
    - safari za kuhudhuria mikutano
    - na mengineyo

    ReplyDelete
  10. Libya ilikuwa nchi iliyoendelea kuliko nchi nyingi.Gadafi ni mtu mzuri tu.
    Viongozi wa Afrika wanatakiwa kumsaidia.Kitendo cha kupiga mabomu makubwa kwenye Ardhi ya Africa ni marufuku inabidi walipe nchi nyngi zitakazoathirika na uchafuzi wa mazingira wanaofanya WAHUNI WAKUBWA .
    AFRICA FOR AFRICANS.... is not about Gaddafi is about AFRICAN future.African leaders Awake....

    ReplyDelete
  11. TUACHE KULETA FIKRA ZA KIDINI HAPA,HIZI DINI NDIZO ZINAZOTUPUMBAZA NA KUJIKUTA KATIKA UJINGA NA UMASIKINI USIOKWISHA,TENA UKIANGALIA KWA UNDANI UNAKUTA DINI ZOTE HIZI SIYO UTAMADUNI WETU WAAFRIKA,ZIZLIENEZWA ENZI HIZO BABU ZETU WALIKUWA WAJINGA,INABIDI TUAMKE TUONE NAMNA YA KUJITOA KWENYE TATIZO SUGU LA UMASIKINI ULIOKITHIRI KATKA NCHI ZETU ZA KIAFRIKA.MAMBO YA LIBYA MIMI NAUNGA MKONO UN,KWA KUVAMIA MAANA YOTE HAYA GADAFFI AMEYATAKA MWENYEWE,TABIA HII YA VIONGOZI WETU AU VYAMA VYA SIASA KUKAA MUDA MREFU MADARAKANI,VIONGOZI KUJILIMBIKIZIA MALI NA KUFANYA NCHI KAMA MALI YA FAMILIA,KUCHAKACHUA KURA NK.HAYO YOTE HATUYAONI TUNAKIMBILIA KUTAJA DINI HUU NI UPUUZI KABISA,HATA NCHI YETU TANZANIA INATAKIWA IWE NA MABADILIKO MAKUBWA ILI KUPAMBANA NA UCHAKACHUAJI WA KURA,SIASA ZA UBABAISHAJI,VIONGOZI KUJILIMBIKIZIA MALI,RUSHWA,UMEME WA MGAO NK.KWA JUMLA NI UFISADI MTUPU.KTK MATATIZO KAMA HAYA MSITAJE KABISA UPUUZI HUU WA DINI,MENTALITY NDIYO INATUPOTEZEA KABISA MALENGO YA KUDAI HAKI ZETU.GADAFFI AENDE KABISA TENA ITABIDI IWE KAMA DIKTETA SADAM HUSSEIN NA WATOTO WAKE.HILI NI FUNDISHO KWA MADIKTETA WOTE WA AFRIKA.

    ReplyDelete
  12. sababu ilikuwa inatafutwa sasa imeshapatikana. Tuangalie uonevu unao tokea Bahrain na Libya wapi kuna mauaji ya waiziwai??? Kuna kipengele gani kina ruhusu kuingiza majeshi ndani ya nchi ya mwenzake bila ya kupitishwa na umoja wa mataifa??? Uonevu wa dhahiri unaotokea na wananchi wa kawaida ndio tunaumia. Sijakia ufaransa wala mwingereza kukemeea mauaji ya Bahrain wanafiki wakubwa. Sishangai uchumi upo unstable kwa majangili kama hao. Na kama wakiendeelea hivi watu wote duniani tunapata portion yetu kwa kila kitu kuvurigika. Hili sio jambo la mlibya au Mmisiri au Mbaharain, ni janga la watu wote.

    ReplyDelete
  13. Mdau unazungumzia Bahrain,mimi nimewahi kuishi huko kwa miaka kadhaa,kuna matatizo makubwa hasa ya ubaguzi wa matabaka,kwa wasio wahi kuishi huko hawawezi kulielewa hili.wanaoandamana na kupinga uonevu huu wana haki ya kufanya hivyo.Na wakati huu ni wakati wa mapinduzi na watu kujikomboa kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia,miaka hii hakuna namna ya ku control media na kuwa fanyia brain washing wananchi kuna internet nk.watu wanapata habari zote za dunia,kwa hiyo hakuna mtu anadanganywa siku hizi kwa propaganda za srikli zetu dhalimu.WEnye kuandamana kudai haki Bahrain wana sababu za kufanya hivyo na tusiwaone kuwa ni wajinga,huu ni mwisho wa udikteta,na mambo ya ufalme yanaelekea kuisha karne hizi.

    ReplyDelete
  14. Mmeomba msaada mkapewa, Sasa mnalalamika. Marekani iwaache waarabu wachinjane kama somalia. Wanauana wenyewe kwa wenyewe. Kila mtu ajifunze kufurahia madikteta wake.

    ReplyDelete
  15. Nyie watu wenzangu(waafrica)tunapenda kulalamikia hukuhuku kwa michuzi, kunaishia hukuhuku, kwa nini basi tusiweke haya katika vitendo? Umoja wa nchi za Africa ndio ilikuwa wawe kipao mbele dhidi ya mgogoro wa Libya! matokeo yake wamekaa kimya! kama hawajui kinachotokea! sasa ndo walikuwa wanasubiri wazungu waje kuwatatulia tatizo!!?? ndio hao sasa.. I think we are still sleeping!! sisi na viongozi wetu pia.... ASHAME..

    ReplyDelete
  16. SAWA MIMI HAYO YOOOTE NAKUBALILIANA NA NYINYI ALIIENDAMANA KUMPINGA GADAFI SIWALIBYA????? NA GADAFI KWANINI ANATAWALA MIAKA YOOOOTE ZAIDI YA 40 ANGEKUBALI DEMOKRASI YOTE YASINGETOKEA GADAFI ANAWAKE WANGAPI???? NANYINYI BONGO UMASKINI MNAUTAKA MZUNGU ALIKUJA TZ KUTUFUNDISHA UOONGO???? UTAPELI KILA MAHALI, MANESI HAWAKUTIBU MPAKA UWAPE PESA MSIWAONEE WAZUNGU UMASKINI TUNAUTAKA WENYEWE MIE MWAFRIKA NAPATA HAKI SASAWA NA MZUNGU ACHENI PROPAGANDA ZISIZO NA MSINGI KAYATAKA GADAFI MWACHENI AIPATE JOTO YA JIWE

    ReplyDelete
  17. Mdau hapo juu unasema dikteta hemu angalia madikteta duniani ni africa tu au huyo sadam jee ktk nchi za magharibi wao sio madikteta, ile mahakama kuu ya ICC imewekwa pale kwa ajili tu ya waafrica ndio mtu mwengine. Halafu huko iraq umekuona kulivochafuka hakufai kabisa bora ule utawala wa sadam kuliko sasa, wao hawajui tena hayo lengo lao ni mafuta na yameyapata na libya maisha itakuja kuwa kama vile iraq kama huamini utakuja kuona.
    Africa union wamejitahi kuitetea libya lakini wapi hawasikilizi coz hawaonekani kama wana uwezo wowote ule.

    ReplyDelete
  18. Tuache ushabiki wa kidini hapa. Huyu Gaddafi anauwa watu wake kama mbuzi mlitaka nchi tajiri wakae kimya. Issue ya Rwanda mpaka leo inawasumbua sasa mlitaka Gaddafi aendelee kuchinja watu wake halafu kesho mje mseme mbona Marekani hawakusema kitu sasa wanafanya kinachotakiwa oh wana lao jambo tuangalie ukweli wa issue yenyewe sio kushabikia bila kufahamu ukweli uliopo

    ReplyDelete
  19. Nyie mnaomtetea gadafi mmerukwa na akili, kwani hiyo nchi aliumbiwa yeye na ukoo wake? miaka 42 bado umo tuu kwani yeye tu ndiye mwenye uwezo wa kuongoza hiyo nchi? huo ni uselfish, mwache atwangwe hadi afilie mbali, na tayari mwanawe mmoja keshauwawa khamis al gadafi , bado lile moja seif bedui kama babake watakufa wote pambafff..... uroho wa madaraka ndiyo unafanya hao wazungu watuone tulivyofekihapo ndiyo wanapopatia mwanya mie nasapoti kichapo!

    ReplyDelete
  20. SIYO JAMBO LA BUSARA KUWAPIGA WATU NDANI YA NCHI YAO TAKA HUSITAKE INSHU NI UTAJIRI WA LIBYA, WAMAREKANI NI WATU WA AJABU SANA SIJUWI KWA NINI WAAFRIKA HATUSHTUKI MPAKA JAMBO LITOKEE...!!!!
    KIKUBWA NI KIONGOZI KUBADIRIKA AMA WATU KUPATA MAITAJI YAO YA MSINGI? LEO TANZANIA KILA NDANI YA MIAKA MITANO TUNAUCHAGUZI, JE TANGU TUANZE KUWA HURU NI CHAMA GANI KINAONGOZA? KUNA TOFAUTI YOYOTE NA GADAFI?
    MAISHA YETU SISI WENYE UCHAGUZI KILA BAADA YA MIAKA 5 NA WALE WA LIBYA NI SAWA?
    KOYISON
    TUAFENI UNAFIKI WAZUNGU SIYO WATU WAZURI KABISA ASA PALE WANAPOTAKA MAISRAI YAO.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...