Kamanda Ras Makunja na FFU
Ughaibuni wana Ngoma Afrika b
and

Jinamizi la mziki limeigeuzia kibao bendi maarufu ya mziki wa dansi barani ulaya, Ngoma Africa band aka FFUkwa kutaka kuwatosa pabaya -- nchini Egypt!
Bendi ya Ngoma Africa aka FFU imelazimika kuvunja safari ya Egypt,ambako
Kikosi kazi hiko kilitakiwa kushiriki katika maoyesho ya "World Music Festival 2011" yaliyokuwa kuanzia tarehe 6 hadi 12 Mai 2011,mjini Port Alexandria
Kutokana na sababu za kiusalama kikosi kazi Ngoma Africa band kimeshauriwakuachana kabisa na safari ya Misri,kwa kupitia wakili wa bendi hiyo kamanda wa FFU Ras Makunja amelazimika kuvunja mkataba na watayarishaji wa onyesho hilo.

Ngoma Africa band yenye tabia ya kuwatia kiwewe na kuwadatisha wasahabiki kwa mziki wao..wamejikuta wanaelekezwa pabaya na dira na mzuka wa bongo dansi wanaelekezwa kwenda kutumbuiza mahala ambapo amani hakuna!
Mashirika ya bima za maisha nchini ujerumani imetoa onyo kwa bendi hiyo
hiwapo itajifanya kichwa ngumu na kwenda nchini Misri..basi chochote
kikitokea wasitegee kulipwa au huduma.

Pamoja na kuwa bendi hiyo ina uzoefu kwa kupiga tour mara nyingine katika
nchi ambazo zilizowahi kuwa na mapigano...lakini hili tour la Egypt ni utata
mtupu! Ambao unaonyesha wazi kuwa "Virungu vya FFU havitambi mbele
ya majamvia na mijeledi ya wamanga"

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kamanda ras makunja kulikoni tena?sasa tutakufukuza kazi,
    ffu ndio mnaotegemewa kila penye fujo lazima patulizwe na virungu sasa
    soo hili vipi? kamanda naona hili zito,vingivyo pale kwenu kariakoo
    tutafunga tulubai

    ReplyDelete
  2. Kamanda wa ffu,tunakupa siku saba ujielezee kwa nini?umechomoa
    kwenda kutuliza ghasia?wakati umekula kiapo cha utii kuwa kila
    penye ghasia lazima virungu vitembezwe.

    ReplyDelete
  3. te te te kamanda si mngekwenda tu,vyeo mngepandashiwa,mshiko mkubwa,
    kamanda mimi nawamshauri nendeni tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...