Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya (Watatu kushoto) akikata utepe kufungua Tawi jipya la Benki ya CRDB Mwanjelwa Jijini Mbeya. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo Bw.Martin Mmari na Meneja wa tawi hilo Bw. Luila Ephraim. Kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa Benki hiyo Dr. Charles Kimei, Mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Mbeya, Kanali Kayombo na Mama Mwandosya.
Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya akikabidhi baadhi ya vitanda, magodoro na mashuka kwa mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Mbeya, Kanali Kayombo. Vifaa hivyo vilitolewa na Benki ya CRDB kwa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya wakati wa ufunguzi wa tawi la Mwanjelwa. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo Bw.Martin Mmari na katikati ni Mkurugenzi mtendaji wa Benki hiyo Dr. Charles Kimei.
Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya, mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Mbeya Kanali Kayombo, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB Bw.Martin Mmari, Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB Dr. Charles Kimei na Mama Mwandosya wakiwa pamoja na wafanyakazi wa Benki hiyo tawi la Mwanjelwa muda mfupi baada ya ufunguzi wa tawi hilo.
kaka nakuomba nitumie wasaa huu kutoa malalamiko yangu juu ya CRDB bank tawi la Vijana Kkoo, kwanza akabisa imeandikwa kuwa benk inafunguliwa saa 2.30 lkn utanshangaa wakati huo wao ndio wanajiandaa kutoa huduma na sio kama wako tayari kutoa huduma, mfanop leo asubhuhi kulikuwa na foleni kubwa ya ajabu lakini kulikuwa na Telles wa 3 tu na kati yao ni mawili tu ndio walikwa wanahudumia wateja, mmoja alikuwa anahesabu pesa tu kwa takriban saa moja na nusu bila kujali wingi wa watu kazi ambayo angeweza kuifanya hata baada ya kazi, ni kawaida kabisa kwa tawi hili kuwa na watu wengu haswa ukizingatia maeneo haya yamezungukwa na wafanya biashara, lakini jamani huduma inasikitisha sana, foleni ni moja tu lkn inapofika zamu yako unaambiwa dirisha hili sio la kudeposit hivyo either urudi nyuma au usubiri mtu amalize ndio nawe uende kwenye hilo dirisha, imagine zipo telle chambers kama 8 lkn ni 2 tu ndio zinatoa huduma sasa hizi nyingine si bora wangetuuzia hata maja ili ujue kama ukikosa huduma moja basi japo maji yakukate kiu, hakuna hata sehemu ya kukaa hivyo inabidi ubaki kwenye foleni ndefu kwa muda mrefu huku askari wa ultimate akifanya kazi ya kuwasogeza tu kutokana na urefu wa foleni lkn hana uwezo wa kuwaambia wahusika waongeze wafanyakazi. wafanyazi walio customer service ni jeuri utadahani kila mmoja wao ana majority share.ukweli nakuomba utufikishie salam hizi kwa Kimei kwani tawi hili limekuwa na malalamiko sana ni tofauti na unapokwenda Bank hiyo hiyo Mlimani au Azikiwe na holland.
ReplyDelete