Tumia utaalamu na uwezo wako wa uelevu wa hali halisi ya Majita, kuihudumia Majita, kwa maslahi ya Majita!

Nani? Wewe unayetoka Majita, Musoma, popote pale ulipo – hasa uliyestaafu.

Sababu? Kuiendeleza sehemu ya Majita ukijitolea katika kubuni, kupanga, kutekeleza, kupanua na kutathimini mradi-kusudiwa wa maendeleo–ambatana (ambao utakuwa ni ‘not-for-profit' NGO): Majita Integrated Rural Development Initiative.

Ujuzi? Dini, Kilimo, Komputa, Madini, Maji, Mazingira, Menejimenti, Miundombinu, Mistu, Nishati, Sheria, Takwimu, Ualimu, Uandishi/Utangazaji, Uchukuzi/Usafirishaji, Udaktari/Afya, Ufugaji, Ufundi/Ujenzi, Uhasibu, Ukarani, Upishi, Utalii, Utamaduni, Uvuvi . . . . na kadhalika.

Lini? Mara moja . . . . Sasa hivi . . . . Leo!

Wapi? Ki-jadi, walipanga, walibuni, walitekeleza, walipanua na walitathimini

mikakati kama hii, wakikutana uso kwa uso wakikaa chini ya mti (orality culture). Wakati wa mashini (industrial culture), wanagawana umbali wa kusafiri na kukutana katikati ya nchi (Canberra, Lilongwe, Rawalpindi, Brasilia, Dodoma). Leo hii tulio na bahati ya mtandao (digital culture), tumewezeshwa kufanikiwa kukutana ‘instantaneously’, kana kwamba tumo katika ‘global village’.

E-Mail - (wasiliana moja kwa moja)? romuinja@yahoo.com (au) MUJUNGU@unhcr.org

Omurimu ogukomera gutakorelwe!

Bhamugaire, najayo!

‘If it is to be, it is up to me.’

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. wajita fanyeni kweli,Mh Mkono amewasahau nyie

    ReplyDelete
  2. mbona haieleweki!?

    ReplyDelete
  3. wewe unayesema haieleweki una maana gani? watu wengine bwana bangi kweli!
    hii kitu ni nzuri kwa kweli maana mkoa wa Mara watu wamejisahau sana... ni wakati wa kukumbuka makwao sio wajita tu na makabila mengine!!

    ReplyDelete
  4. Wazo la kuendeleza Majita kama lilivyowasilishwa hapa ni zuri. Ila kwa upande wangu kwa kweli naona kama habari haijaeleweka vizuri yaani kwa asilimia mia moja japo kuna mchangiaji mmoja hapo juu aliposema habari haieleweki kuna mchangiaji mwingine alimponda na kumwita mvuta bangi.

    Pia binafsi kama wazo ni kuendeleza majita preference isiwe kwa watu waliostaafu tu. Nadhani kwa kufanya hivyo Initiative itapoteza input ya kutosha kutoka kwa vijana. Zaidi ya yote Initiative ikiwa na watu mchanganyiko (wazee na vijana) itatoa nafasi kwa makundi yote mawili kujifunza vitu kutoka upande mwingine. Kukiwa na reciprocity ya aina hiyo itasaidia sana katika kufikia hayo malengo ya kuendeleza Majita. Mfano kuna wazee waliostaafu lakini wengi wao hawana uelewa mzuri katika masuala ya kompyuta lakini vijana wengi wana uelewa mkubwa katika eneo hilo.
    Ahsante sana wasu kwa wazo hili zuri nitawasiliana na wewe ili kufahamu zaidi kuhusu Initiative hii.

    mdau
    Baba La & Vee

    ReplyDelete
  5. wewe mtu wa tatu umeongea la maana fanyeni hima muondoke Dar rudini makwenu huko musomaaaaaa

    ReplyDelete
  6. majita,machinga,pemba,tabora,singida,iringa.....kukiendelezwa hakutakuwa na ulazima wa kila mtu kukimbilia dsm. tena watu wa dsm nao wataweza kwenda hayo maeneo mengine kutafuta rizki. bravo wana Majita kwa ujumbe huu!!!

    ReplyDelete
  7. safi sana potizz.tuko pamoja angalau hawatausema tena kwa fujo

    ReplyDelete
  8. Kaama kuna yeyote ambaye hajaelewa ujumbe wa tangazo hili, anaombwa sana kuwasiliana kwa kupitia hizo e-mail zilizowekwa.

    Hizi e-mail addresses si feki; mimi nimewasiliana nao na wamenielekeza vizuri.

    Hili ni tangazo tu; halina details za kila kitu wanachojaribu kukifanya.

    Haya kazi kwenu, wa Majita!

    ReplyDelete
  9. Mdau Baba La & Vee,

    Umeandika, inter alia, "Pia binafsi kama wazo ni kuendeleza majita preference isiwe kwa watu waliostaafu tu. Nadhani kwa kufanya hivyo Initiative itapoteza input ya kutosha kutoka kwa vijana."

    Asante sana kwa mchango wako!

    Katika maelezo yenye details, sio kwamba vijana wamesahauliwa katika initiative hii. Kila mwenye kuipenda Majita anakaribishwa kuchangia: mtoto, kijana au mzee kutoka Majita, Tanzania na nje.

    Mkazo wa waliostaafu ulizingatiwa kwa makusudi maalum.

    Mosi, baadhi ya waliostaafu hubakia kunywa pombe baani, kucheza darts na snooker (pool) - au yote matatu - na kusahau kuwa wana hazina kubwa ya kuchangia maendeleo ya sehemu walikotoka.

    Pili, ndio kusema kuwa wastaafu wengine wana muda mwingi kushinda vijana ambao wengine wako shuleni au wanachapakazi za ajira.

    Tatu, kuna haja ya kuwapata watu (a core team)ambao watajitolea kutayarisha mipango ya mkakati wa Majita Integrated Rural Development.

    Nne, kufikiria kuwa wastaafu wengine hawajui ya komputa, nk, ukweli ni kwamba kila atakayependa kujiunga atashirikishwa tu mara uzinduzi wa NGO hiyo ukikamilika.

    Kwa sasa sisi tuliopendekeza wazo la kuisaidia Majita tumetengana ki-mabara. Lakini internet imetusaidia sana kuweza kukutan na kukubaliana ki-msingi kuisaidia Majita.

    Currently, tunajaribu kupata database ya watu wa kujitolea na ujuzi wao katika kutayarisha Majita Integrated Rural Development.

    Wasiliana na hizo e-mails addresses zilizowekwa. Utapata maelezo zaidi.

    Asanteni,

    Mdau Aliyeleta Tangazo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...