Serikali kupitia Kaimu Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki, imesema kuwa kila familia inapaswa kuchagua mtu atakayesimamia mirathi ya marehemu ili kupokea kifuta machozi cha shilingi 8.5 milioni kwa kila familia iliyopoteza ndugu kutokana na milipuko ya mabomu iliyotokea katika Kikosi cha 511KJ cha Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam usiku wa Februari 16, 2011 ambapo zaidi ya watu 20 walikufa na wengine zaidi ya 300 kujeruhiwa;
Wakati huo huo, Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kikosi 514 KJ Makambako mkoani Iringa limelipua mabomu yaliyohifadhiwa kikosini hapo katika hatua ya kuyateketeza kutokana na kuisha muda wake.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe bi. Sarah Dumba alisema zoezi la ulipuaji wa silaha hizo lilianza Machi Mosi na linatazamiwa kumalizika Machi 5 mwaka huu.
“Mabomu yanategemea kutoa vishindo vikubwa, hivyo nawatoa wasiwasi wananchi, wasiwe na hofu kwani zoezi hili linafanywa kwa kitaalamu na kwa uangalifu mkubwa,” alisema Dumba.
Kwa mujibu wa Dumba maeneo yatakayoathiriwa na zoezi hilo ni pamoja na vijiji vinavyozunguka kambi hiyo ambavyo ni Katenge, Kilimahewa, Kipagamo na Ikulumambo. Amewaomba wananchi wanaofanya shughuli mbalimbali eneo la kuzunguka kambi hiyo kusitisha shughuli hizo hadi baada ya kukamilika kwa ulipuaji mabomu hayo.

Ni hatua nzuri kwa serikali yetu. inastahili pongezi hasa kwa kulipua mabomu mengine ambayo muda wake ulikwisha
ReplyDeleteKwaiyo mnavyo ona sasa ndo muda mwafaka kufanya ilo zoezi na watu wameshapata mazara na wengine wamekufa. swali ni kwamba mlikua wapi siku zote.
ReplyDeleteNot bad at all...je italipwa familia iliyopanga nyumba au mwenye nyumba?
ReplyDeleteA little too late mpaka watu wafe ndio wanashtuka.
ReplyDelete