
Habari za kazi na mihangaiko ya hapa na pale. Tafadhali niwekee tangazo hili tena. Leo siku ya Jumamosi ya Tarehe 19 March tutakuwa na kisomo cha kumuombea Mama yetu marehemu Asha Nasibu Shefa kitakachofanyika huko Stockholm, Sweden.
Watoto wa Marehemu Viwe na Fatuma watakuwa wamesharudi kutoka nyumbani Tanzania.
Kisomo kitaanza saa tisa mchana huko Vista skolan (Hageby Allè 25 Huddinge). Ukitokea Huddinge Station unachukuwa Buss NO 714 mot Vistaberg shuka Vista Skolan.
Kwa wanaoendesha kutokea Huddingevägen ingia Glömstavägen 259 halafu ingia kulia kwenye round about Hageby Allè simama Vista skolan.
Tafadhali Mfike kwa wakati na wote mnakaribishwa.
Kwa maelezo zaidi (0704671940)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...