Hayati Hamidu Bisanga

Ni siku, mwezi,mwaka na sasa miaka miwili tangu ututoke ghafla kwa ajili ya gari iliyotokea tarehe 29/03/2009 pale Kijitonyama, Dar es salaam. Tuliumia sana. Tunakukumbuka sana baba yetu mpendwa HAMIDU AHMED BISANGA.

Ni vigumu kusahau ila sisi tulikupenda,ila mungu amekupenda zaidi.
Unakumbukwa sana na mkeo,watoto,wajukuu,ndugu, na marafiki zako wote pamoja na wafanyakazi wa NDC na Daily News.

TUNAKUPENDA DAIMA BABA YETU

INNALILAH WAINNA LILAH RAJUIN.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Mungu akulaze mahali pema peponi Mr Bisanga....Sisi wana Brake Pointi Kijitonyama, tutakukumbuka daima.

    Rodrick Mwambene

    ReplyDelete
  2. Hakika hutosahaulika milele kutokana na ukarimu wako na roho yako ya pekee ambayo Mungu alikujaalia. Vizuri kweli havidumu.
    Inna Lilaah wa inna illaah rajiun.

    ReplyDelete
  3. M/Mungu akulaze mahali pema peponi...Ameen.

    Saleh Senga.

    ReplyDelete
  4. Tunamuomba Mwenyezi Mungu akulaze mahali pema peponi, rafiki yetu, ndugu yetu mpendwa Bisanga "Hambis" kama tulivyopenda kukuita. Nilisikitishwa sana sana, niliposikia umetutoka ghafla. Bado ninayo machungu moyoni na hayataisha, hasa nikikumbuka upendo, ukarimu mawazo, na ushauri wako ulionipatia wakati wote. Ingawa haupo nasi kimwili lakini kiroho upo pamoja nasi. Tutakukumbuka daima. Upumzike kwa amani my very dear friend Hamidu Bisanga. Amen. S.K.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...