For once, I am not hesitating to jump and airing my opinions on this issue that seems to take fore news spots in Tanzania presently. What Mr.Mashaka’s elaborates in a detailed about Babu’s miraculous concoction drink is absolutely true, and here under I am explaining my personal opinions about Babu’s bizarre so called treatments on chronicle diseases.
I can say that, one thing that cause mass of people to take a trip to Loliondo for medical treatment is cultural effect; under the cultural phenomenal, you might get to a point and understand why people are flocking to Babu. To be more precisely, I can attribute the belief part of culture as a core reason that makes majority of individuals to travel to Loliondo. Culturally, Tanzanians are affected at large in their daily endeavors on natural beliefs in witchcrafts and its applications in their daily activities, for example, an ordinary Tanzanian will credits witchcraft on a very ordinary thing like tripping when he/she walks on the street.
Based on the mentality of an ordinary Tanzanian with the elaborations that Mashaka and also Mjengwa aired on their writings about philosophical works, you might come into agreement with my thought that majority of Tanzanians who are currently traveling to Loliondo are influenced most with their beliefs that miraculous concoction created by Babu Ambi will cure their diseases.
Moreover, I am very much dismayed with the fact that, there are those who travel to Babu for a reason more that their belief rather than a far reaching goal for the expense of those who are really sick and desperate for the cure of their illnesses. On this, I am very much talking about those who use the wave of Babu’s emergence as the political stage for their future goals. As I read and see on various news Medias, without a doubt, I believe there are those who went to Babu and are in the efforts of going there just to show up in order to be seen with majority Tanzanians that they are affected like any other and believe for the cure.
I will classify those whom are well educated, wealthy and in some public political or governmental posts are the one I am talking about here. According to my views, there are some individuals are politicizing Babu’s bizarre for their far reaching goals in future to the extent that they are ignoring their official responsibilities of leading and directing ordinary Tanzanians. For instance, at one time, the Health minister correctly came forward and gave out directions for Babu to stop his practices, for it should be reviewed for its effects in human life, a short while, another minister in the government came out and correct the first official directives and insisted that the government did not want to stop Babu’s practices; and in addition, the government will help Babu’ in the delivery of his unapproved medication to human beings.
With this instance, I will directly accuse the later official that not only is misleading Tanzanians but also is in no doubt using the situation as a political aspect for his endeavors. To be more precisely, I read on the other day that the same official (Mr. Lukuvi) traveled to Loliondo for a cup of concoction. There are many Lukuvi’s that are among those travel to Babu not to get the cup for the cure rather for their other political goals.
To say the least, among thousands of Tanzanians who are traveling to Loliondo, there are those who are sick and desperate but also there are those whom are supposed to give out directions and leadership on this bizarre rather they are going there to score cheap political credits.
Mwilima
NYC.
Kwa taarifa rasmi ya serikali kuhusu kikombe cha babu Loliondo
Hello Mwilima,
ReplyDeleteThank you for the candid response. Even though we differ slightly (me and Mujengwa) we do however, agree that there is a problem in our country that needs immediate attention. The situation in Loliondo is going to explode. The government must do something right away to avert the human catastrophe.
We need more informed, and deep thinking individuals like Mujenga, whom i found to be very much informed to tackle this rapidly emerging problem. Lets not sit on our ideas, we must stand up against the society vices
Regards,
John Mashaka
Yaani ukitaka umaarufu kwa siku moja andika article ambayo inampinga John Mashaka, na hapa kwamba utakuwa maarufu instantly. Angalieni USblogers amekuwa maarufu bila kufahamika, ni jini wa Oxford university lakini maarufu kweli
ReplyDeleteHello Mashaka, Schoolmate (Tambaza) Mjengwa na wengineo;
ReplyDeleteMy opinion is that, the whole issue of Loliondo-Babu has more to do with people being desperate and have no where to go and the little willingness to reason; worse enough is the political leadership which is supposed to direct people towards the right track instead of supporting issues which can not be proved scientifically and even themselves getting involved directly.
Look, If a Minister in President's office supports a move and participates himself directly what do you expect from my grand mom from Nyololo (mafinga), first she is not well educated and the Minister is well educated and spents significant time with Mr President to run state affaier!, whatever political leaders in big offices preach is the correct tune to join for my grand mom and normal villagers in TZ. Hence we are killing our people by supporting the Loliondo thing.... The roots used are known to contain poisonous chemicals, I believe once somebody takes kikombe cha babu.. probably within short period of time while these chemicals are in ones body they may react with the reagents used for various disease tests leading to wrong results.
I think the minister for Health was not supposed to keep quiet unless if the case was discussed and agreed in the TZ Cabinet under its chairman and agreed to let things go natural and stopped any move planned by the Minister to stop the activities... otherwise I do not think Lukuvi has direct powers to stop Minister for Health to execute his duties within his scope of work.... Mungu Ibariki Tanzania na Watu wake, na Uwape Mwanga wa Kuona yaliyo maovu... Benny
JOHN MASHAKA IS WRONG. AENDE TANZANIA KAMA WATU WENGINE WENJE KUTAKA KUFANYA MABADILIKO YA NCHI ZAO. SIO KUANDIKA TU HAPA WAKATI HATA VITENDO HANA.
ReplyDeleteTanzanian 'miracle' pastor Mwasapile calls for a break
ReplyDeleteA Tanzanian pastor has asked people to stop going to his remote home for a "miracle cure" after thousands flocked there, causing chaos in the surrounding area.
Rev Ambilikile "Babu" Mwasapile, 76, says he does not want any new arrivals until after Friday 1 April, to let the crowds die down.
Local media report that about 52 people have died while waiting to see him.
A BBC reporter says the queues to see him stretch for 26km (16 miles).
Belief in magic and the powers of traditional healers are widespread in Tanzania.
Some witchdoctors say that the body parts of people with albinism are effective when making magic charms, leading to the killing of dozens of albinos in recent years.
In 2009, the government outlawed all witchdoctors and traditional healers.
But on Monday, Prime Minister Mizengo Pinda said he would not take any action to stop Mr Mwasapile's activities.
'Safe to drink'
Mr Mwasapile's concoction is made from herbs and water, which he sells for 500 Tanzanian shillings (five cents; 3p).
When she visited Mr Mwasapile's home near the northern Loliondo town recently, the BBC's Caroline Karobia found 6,000 people waiting to see the retired Evangelical Lutheran Church of Tanzania (ELCT) pastor.
They are waiting for days by the roadside and outside his home in Samunge village without shelter, clean water or toilets.
As word has spread in the past month of the pastor's supposed ability to cure any ailments, some people have even been taken out of hospital by their relatives who believe they are more likely to be cured by Mr Mwasapile.
Some of these have died before seeing him, while others are reported to have died after taking his concoction.
Health Minister Haji Hussein Mponda told the BBC that tests had shown that the mixture was safe for human consumption.
He said tests were now being conducted to see if it has any medicinal properties.
Extra police have been deployed to the area to control the huge crowds, some of whom have travelled from neighbouring countries such as Kenya and even further afield.
Mr Mwasapile asked for the break following a meeting with local officials.
http://www.bbc.co.uk/news/world-africa-12878811
TAARIFA YA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII KUPITIA TAASISI ZAKE ZA UTAFITI KUHUSU DAWA YA MCHUNGAJI MSTAAFU AMBILIKILE MASAPILA WA SAMUNGE- LOLIONDO, AMBAZO NI: MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA (TFDA), TAASISI YA UTAFITI WA DAWA ASILI YA CHUO KIKUU CHA AFYA YA SAYANSI SHIRIKISHI MUHIMBILI, (MUHAS) MKEMI MKUU WA SERIKALI (CGC), TAASISI YA TAIFA YA UTAFITI WA MAGONJWA YA BINADAMU (NIMR)
ReplyDeleteTaarifa ziliifikia serikali kuwa, Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila, anatibu magonjwa sugu kwa kutumia dawa aliyooteshwa na Mwenyezi Mungu. Inasemekana kuwa, mchungaji alianza tiba hii tangu mwezi Agosti 2010, lakini watu wengi walianza kumiminika kwenda huko Samunge, kuanzia mwishoni mwa mwezi wa pili, mwaka huu wa 2011.
Kufuatia taarifa hii, serikali iliielekeza Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuwa, ufanyike haraka uchunguzi kuhusu dawa hii na itoe ushauri Serikalini ipasavyo. Baada ya kupokea maagizo hayo, wizara iliteua wataalamu kutoka taasisi zake tukiwemo sisi, TFDA, NIMR, Muhimbili kwa maana ya MUHAS, Mkemia Mkuu na tulijumuisha wataalamu wa hapa wizarani, ili kuifanya kazi hiyo muhimu, akiwemo Msajili wa Tiba Asili na Mbadala.
Hapo Machi 7 mwaka huu, sisi TFDA na wenzetu wanasayansi tulifanya safari kwenda Samunge kuonana na kufanya mazungumzo na Mchungaji mstaafu AmbilikileMasapila. Sisi TFDA na wataalam wenzangu wote, tunamshukuru sana mchungaji mstaafu, kwa ushirikiano na msaada mkubwa aliotupa sisi watafiti wote. kwa kuwa, tulifanya mazungumzo kwa masaa kadhaa kuhusu dawa hiyo jinsi alivyoanza, pia, alituonyesha mti unaotumika na alitupa sehemu mbali mbali za mti huo, kwa uchunguzi zaidi. Kadhalika, alituonyesha jinsi anavyotayarisha dawa hiyo na kutupatia sampuli yake iliyokwishategenezwa, tayari kwa matumizi. Sisi TFDA na wataalamu wenzetu tuliondoka nayo, kwa ajili ya uchunguzi zaidi, kwenye maabara zetu.
Baada ya kurejea kituoni Dar es Salaam, kazi ya utafiti wa dawa hiyo ilianza:
Jambo la kwanza kama watafiti, ilikuwa ni kuangalia na kuhakikisha usalama wa dawa ya Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila kwa watu. Uchunguzi uliofanyika, umetoa matokeo ambayo tumeridhika kuwa, dawa kwa kipimo anachotumia Mchungaji mstaafu AmbilikileMasapila, haina madhara yoyote yanayotambulika kwa sasa, kwa matumizi ya binaadamu.
Kazi inayofuata kwetu sisi watafiti baada ya matokeo haya, ni kuchunguza na kubaini, kama kweli dawa hii inatibu magonjwa hayo matano (5), kama anavyoeielezea yeye Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila. Uchunguzi huu utakapo kamilika, matokeo yake yatatolewa mara moja kwa wananchi wote!.
Hata hivyo, ninaomba kuwatahadharisha kuwa, hatua hii ya uchunguzi, si ya muda mfupi. Kwa mujibu wa kanuni na taratibu za kisayansi duniani, tafiti za namna hii zina mchakato unaohitaji muda wa kutosha kukamilisha hatua zake mbali mbali, na pia, kufikia viwango na vigezo vinavyokubalika Kitaifa na Kimataifa. Tunafanya hivyo kwa kuzingatia kuwa, dawa hii ni kwa ajili ya matumizi ya binadamu, na inafuatiliwa na wananchi wetu na mataifa mbalimbali.
Sambamba na utafiti katika hatua hii, pia tunafanya uchambuzi wa kisayansi, katika maabara zetu, kwa sampuli tuliyoichukua kwa Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila, kwa kuangalia mambo mengine mawili muhimu kama ifuatavyo:
Read more: BongoCelebrity
nimeshapata siri na mimi pia. nitakuwa naanzisha mada, kumpinga au kumsapoti john mashaka ili niuze sura bongo, tehhhhheteeee
ReplyDeletehii blogu inatoa stress kweli
Michuzi makala kama hizi ni nzuri, lakini ni vizuri zingekuwa zinaandikwa kwa kiswahili kwa faida ya wengi.
ReplyDeleteJohn, as a medic working in Arusha, what really worries me is that many people who had gone to Loliondo (especially those suffering from diabetes and hypertension "BP") and decided to stop taking their medication have experienced serious complications (at least one of which was renal failure) and I know of at least three fatalities over the last two weeks. The problem is that there is a local (TZ) media blackout whereby TZ media have refused to publish or air any views expressed by many doctors in Arusha and Kilimanjaro regions warning people who have gone to Loliondo not to stop taking their prescribed medications. Whereas the negative impact of Loliondo's cure on diabetic and hypertensive patients are already being felt, my fear is that in the next three to six months the same negative impact on HIV+ patients is going to be felt with devasting consequences. It is time for the Government to send fact-finding missions to hospitals (including reputable religious-supported ones) in the northern regions to speak to doctors who are dealing with patients who have had life threatening conditions - and some even died - AFTER returning from Loliondo.
ReplyDeleteMashaka umesema kweli kabisa...its a time bomb! soon will explode !!! YAngu macho na masikio! kuna kitu kimejificha hapa na tutakijua siku chache zijazo! kweli serikali ya Tanzania! yenye wasomi kabisa wanaweza kudangaya umma wa waTanzania kuwa imefanya utafiti wa siku mbili na kugundua kuwa dawa haina madhara! tumeona sumu zinazoua taratibu, jamani TAnzania kweli tupo gizani! Mungu tubariki
ReplyDeleteMikoa ya kusini watu wanalalamika kupinga hatua ya serikali kumsimamisha 'babu dogo' asiendelee kutoa tiba yake. Huko Rombo, licha ya babu wa Rombo kukatazwa na serikali asiendelee na tiba yake, bado watu wengi wanakwenda kwa siri kumuona kwa siri. Jamani tutafika?
ReplyDeleteNi kweli maana kiingereza kilichotumika ni kigumu haswa ! ili uweze kuelewa uwe na Mr Dic pembeni kurefer ....teh teh teh MIMI MAIUNAAAA...
ReplyDeleteKipi cha kushangaza? Tuko katika nchi ambamo maalbino wanauliwa, watoto wanatolewa kafara, vikongwe wanauliwa, watu wanachunwa ngozi, etc etc etc... Imani ya watu ya Mungu ni ndogo mno kiasi cha kwamba watu wengi wanahitaji "miujiza" ili kuthibitisha imani zao dhaifu kabisa. Miujiza ya Mungu iko kila siku, lakini miujiza hiyo si ile ya watu kunywa dawa na wakifa na madaktari wakisema watu wanakufa madaktari hao hao wanatukanwa.
ReplyDeleteIf you don’t believe in Babus Miraculous cure, just keep quit. Msiwachanganye watu kwani ukweli ni kwamba watu wanapona. What the government should do is to improve the services offered by Babu. Siku mtakapopata shida hata njie Mnaotuona Watanzania hatunazo kwa sababu ya kunywa dawa ya Babu, na nyie mtaitafuta lakini mtakuwa mmechelewa. Chezeeni vitu vingine, sio imani za watu.
ReplyDeleteJohn, mashaka, makala yako ya kumpinga mchangiaji ni nzuri na nimawazo yako. cha msingi endapo unataka kuitendea haki nchi yako rydi nyumbani tanzania kama akina shayo, ukapambane na hali halisi ili uweze kuleta mabadiliko. kuandika tuu mkiwa huko nje haisaidi, we need you back home.
ReplyDeleteWaheshimiwa Mashaka wa marekani na Mwilima wa marekani kule New york. Mwilima nimesoma maoni yako juu ya matibabu ya Babu kule Loliondo. Maoni yako yanaambatana na kumuunga mkono Mashaka. Kwa maelazo yenu inaonekana kuwa nyinyi mnatoka kwenye koo zenye kheri, hivyo munaouwezo wa kwenda kwenye hospitali kubwa kubwa hapa TZ na kupata matibabu. Au pia inaonesha kuwa munaouwezo wa kwenda nje (ng'ambo) kwa matibabu. Nadhani hii haina mjadala maana mumeshatuonyesha kuwa munaishi Marekani. Je, wazazi wenu, na ndugu zenu wote ktk ukoo wanatibiwa Hospitali kubwa na pia munawalusha ulaya?
ReplyDeleteMwilima umetaja kuwa mila ndiyo shinikizo kubwa linalofanya watu waende Loliondo. Ninataka kukujulisha kuwa dunia nzima kila jamii ina mila zake na katika taaluma ya tiba huwezi kutenganisha mila na maradhi, kwa maana vyote vinakwenda pamoja. Unapojifunza maradhi ya sehemu fulani unajifunza na mila (culture) inasemaje kuhusu maradhi hayo au watu wanaamini nini. Hata huko muliko watu wana mila, na ndiyo maana wewe ukalitumia hilo neno (Culture) kwa lugha yao. Pia wana miiko, maadili mbali na hata imani zisizo za kidini nk. Kwa hiyo basi kuwabeza watu wanaokwenda Loliondo kwenye matibabu sio sura ya kiubibadamu wala maadili mema.
Umetaja mambo ya uchawi (witchcraft) nadhani unachanganya matibabu ya Loliondo na mambo ya ushilikina- Albino. Hata hivyo huko muliko pia kuna wachawi na wachirikina wakubwa. Hao ngozi nyeupe munaowaona kama miungu ni wachawi wakubwa, wanapiga ramli, wana hirizi wanatoa kafara sawa kama wewe Mashaka na Mwilima. Huko Loliondo sijasikia ramli, kafara, majini,au masharti yanayoendana na uchawi. Amkeni na jipendeni.
Bwana Mwilima wa New York, kuna ubaya gani kiongozi wa juu serikarini kama Ndugu Lukuvi akienda kupata matibabu Loliondo? Ninaomba ujuwe kuwa binadamu wengi unaowaona wanoyomatatizo mbalimbali ya kiafya, ila kwa mapenzi ya nchi yao inabidi wafanye kazi na mara nyingine hata wayapuuzie maradhi ambayo wamekuwa wakijitahidi kuyatibu kwa maisha yoa yote bila mafanikio. Kwa taarifa zaidi ni kuwa Waganga na wakunga dhidi ya kutibu wana kazi ya kuwafundisha wagonjwa jinsi ya kuishi na magonjwa yasiyotibika. Kwa wastani maradhi ni sili ya mtu. Hasa huko mliko. Kheri hata hapa nyumbani TZ watu wanaelezana maradhi yao, kwa kuwa tunaamini kuwa "ono arabhesabhesa obhorwere ekerero keramubhora" yaani Mficha maradhi kilio kitamfichua. Kwa hiyo basi panapokuwa na tetesi kuwa kuna tiba ya maradhi sugu watu huenda kujaribu. Umudhanieye leo kuwa ni mzima wa afya basi sio. Tuko pamoja? Binafsi kiongozi wa serikari anapoungana na wananchi wa kawaida kwenye matibabu hiyo inaonyesha kiongozi huyo alivyopondeka. Bwana Mwilima kama Ndugu Lukuvi angekuja huko uliko NYC, basi si ajabu wazo lako ingekuwa Ooh! ametumia pesa ya umma. Hivyo ndivyo unavyosomeka kwenye maoni yako. Binadamu lipi jema! Tupendane!
Kwa taarifa ya hivi karibuni toka kwenye jounal ya wafamasia wa huko mliko inasema dawa zote za magharibi zinafanya kazi asilimia sitini tu (60% )Asilimia iliyobaki 40% ni makapi. Kwa nini unahoji Loliondo.
Inaonekana Mwilima na Mashaka hamjauguwa
bado, au hamjaona watu waliokwenda kwa waganga na waganguzi wasipate tiba? Ninaomba Mwenyezu Mungu awape afya njema. Or wait, you will get yours!
Je, nyinyi ndiyo viongozi wa kesho? mutalipeleka wapi taifa letu!
Mbagala mwisho.
Hata wewe Mwilima umetoa maoni yako mazuri. Lakini mimi nawaomba kama mnataka kuwaelimisha watanzania andikeni articles zenu kwa kiswahili. Ndio lugha inayosomwa na wengi na tunajivunia kuwa nayo. Hofu yangu kwa mada zenu (akiwemo mashaka, mwilima na waliochangia hapa), mbali na kutumia lugha isiyojulikana na wengi, mnaandika tu kulaumu, kukosoa, kulalamika lakini sioni anayetoa ushauri wa kutatua matatizo mnayoyataja. Matatizo yataendelea kama hamtayatolea ufumbuzi.
ReplyDeleteSijaona point zaidi ya viingerza tu ambavyo vimepitwa na wakati. Kama mliandika ili tujue mnafahamu kizungu basi tumeshajua lakini mjue english kwa watz sio deal.
ReplyDeleteSwali: wengi wenu mna dini hasa ukristo au uislamu, hivi ni lini mtaamini kazi za mungu hapa duniani?
Jambo lingine, kama mnampinga babu kwa vigezo vya watu kufa, hata muhi2, Agakhani, St.Thomas, KCMC n.k. watu hufa na kuna dawa zilizofanyiwa utafiti.
Kuhusu wanaosema huo mti una sumu kama wakenya walivyosema, hata dawa za hospitali zina sumu ndio maana unaambiwa usinywe nyingi. hata panadol ni sumu. Kunywa chloroquin nyingi uone kama hujafa.
Cha msingi ni kuboresha usafi wa hiyo dawa, mazingira inapotolewa na kuhakikisha uharibifu wa mazingira loliondo unaimarishwa.
Babu uko juuuuuuuuu. Udumu.
Pia wakumbuke kuwa hata hizo dawa za hospitali zilizofanyiwa utafiti zilitokana na mitishamba. Sasa kwa nini ukatae mtishamba wa babu? Huo ni wivu.
ReplyDeleteVilevile dawa ya babu ni chanzo cha uchumi, inaweza kuboreshwa na kutumiwa kama chanzo cha utalii. Msiojua uchumi "karaga baho".
Ndio maana hao jirani zetu wanafiki waliojaa wivu wanapiga kelele ili babu afungwe ili tanzania isipate fedha.
Mnaowaunga mkono kama Mashaka, Mwilima na Mjengwa hamna la maana ni kujipendekeza tu kwa wazungu ndio maana hamuandiki makala zenu kwa kiswahili. Mimi naomba serikali inipe kazi ya kuifanyia promotion Semunge ili iwe "tourism niche market" tuanze kupata fedha za kigeni.
Leo nimesikia kuna dada wa TABORA nae anatoa kikombe, shame on Tanzania....
ReplyDeleteNami niko USA, nawashangaa mashaka na Mwilima kwa kujikanyagakanyaga humu blogini kuponda dawa ya babu, kuponda viongozi wanaokwenda kupata kikombe na kuponda watanzania wanaokwenda kupata kikombe cha Babu.Karibu wote wamegusia sana suala la elimu wakisema hao watu (educated) nao wanaenda huko? Hapo sijawaelewa kuwa elimu wanayoizungumzia ni ipi hasa na tafiti gani hasa?Kwa sababu elimu ni elimu tu haihusiani na ugonjwa sugu unaoweza kumsumbua mtu kwa miaka mingi.Na elimu inaitwa elimu pale inapotatua tatizo la mtu alilonalo katika mazingira anayokabiliana nayo.
ReplyDeleteKama Mashaka na Mwilima wana elimu kwa sababu wanaishi Marekani, labda wawadanganye wale wasiyoishi hapa marekani,lakini kwa mimi niishiye hapa hawawezi kunidanganya maana naelewa yaliyo nyuma yao na yaliyo mbele yao.Ninachoweza kusema ni kuwa "Asiyejua kufa, angalie kaburi".Kuishi Marekani hakujawabadilisha chochote na wala hamtabadilika kuwa eti sasa ni wamarekani!!Hata hapa Marekani ziwe shule, vyuo, mahospitali au huduma yoyote inatofauti na ndiyo maana kumekuwepo na wapi bora zaidi, au wapi panatolewa huduma nzuri zaidi, au nani daktari bingwa zaidi.Kwa hiyo, kama huduma ya Babu haiwaingii kichwani pumzikeni hapo mlipo waachie wale wenye elimu mnayoiona duni kwani inawafaa wao na inawalipa wao ndiyo maana wana uchaguzi wao ambao una busara kwa kutatualia matatizo yao.
Haiwezi kuingia kilini na sitakubali kuwa eti wewe Mashaka na Mwilima ndo mna elimu yenye tija, kuliko watu wote waliokwenda kwa Babu kupata kikombe.Kama mna elimu yenye tija basi nendeni Tanzania mkaisaidie nchi ile isiendelee kulemewa wakati mpo wenye viwango vya juu lakini mmebaki kuishi kwenye mafleti ya New York huku mkijitutumua kwenye mablogs kutupa makombola kwa wenye matatizo.
Sidhani kama hata Mungu mnauelewa naye na sidhani kama ninyi mna elimu yoyote ihusuyo jamii.Nawatakieni kila la heri.
Mdau Nguswiga Fijo
USA
Mdau Fijo wa USA, Tue,March 29, 09:00pm 2010 UMELONGA!!
ReplyDeleteNdaga.
Mbagala mwisho.