Mbunge wa jimbo la Ludewa Mhe.Deo Filikunjombe (kushoto) akikabidhi kombe la mashindano ya mbunge kwa vijana ,wanaopokea ni diwani wa kata ya Lupanga Atilio Kinyaga na diwani wa viti maalum kata hiyo Consolatha Mgogo ,mbunge huyo amekabidhi vifaa hivyo vya michezo leo kama sehemu ya ahadi aliyoahidi wakati wa kampeni katika kuboresha michezo pia ameahidi kutoa zawadi ya ng'ombe mnyama kila kata kwa kata zote 25 wa jimbo hilo mbali ya kombe hilo la dhahabu pia watapata ng'ombe

Diwani wa viti maalum kata ya Lupanga ,kushoto Mhe.Mgogo akikabidhi mpira kwa timu ya wanawake uliotolewa na mbunge wa jimbo hilo Deo Filikunjombe kwa ajili ya kuendeleza michezo baada ya kazi pia kupunguza kasi ya maambukizi ya VVU

Mbunge Filikunjombe akikabidhi mpira. Picha zote na Francis Godwin

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mlamwikhe Yunyi!March 05, 2011

    Niliwahi kuishi katika hii wilaya. Ndugu zangu mnaotoka ktk hii wilaya mfanye jitihada ya makusudi kuikomboa kiuchumi. Kwakuwa iko pembezoni mwa Tanzania imekuwa na mazingira magumu na labda iko nyuma kwa maendeleo pia.

    I have a great love kwa hii wilaya japo sitoki huko. Wazawa please ongezeni jitihada za makusudi kuisaidia hii wilaya. Ni wilaya yenye wasomi na matajiri wakubwa walio nje ya wilaya na nje ya nchi. Wekeni juhudi ya makusudi kuiinua hii wilaya.

    Asante kwa kuweka hii post na endeleeni kutuletea habari zaidi za Ludewa

    ReplyDelete
  2. Kweli wilaya hii ni nzuri kasoro yake haina maendeleo, ina raslimani nyingi na muhimu (makaa ya mawe) kwa nchi ya Tanzania.

    Kwa kweli inasikitisha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...