ANKAL,

TAFADHALI NISAIDIE KUPOSTI;

WADAU NAOMBA MSAADA WA KITAALAM, NAHITAJI KUNUNUA GARI HONDA CR-V AU SUZUKI (HELLY HANSEN/GOLDWIN)

  • VIPI KUHUSU UPATIKANAJI WA SPEA NA BEI NI REASONABLE?
  • JE MATUMIZI YA MAFUTA YAKOJE (WASTANI WA 1LT/KM)?
  • UMADHUBUTI NA UIMARA WA INJINI
  • MUSHAURI MWINGINE WA KITAALAM

ASANTE.

MDAU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. KUNA RAFIKI YANGU ANA HONDA CR-V ILA TATIZO LAKE AKIENDA NAYO KILIMANJARO AKIFIKA CHALINZE INACHEMSHA INABIDI AIPOZE KWANZA ILA KWA MATUMIZ MENGINE HAKUNA TATIZO

    ReplyDelete
  2. Mkuu hiyo Honda CRV usiguse, ni gari bomu kweli kweli. Kwa matumizi yetu hiyo si gari imara, ni nyanya na spare zake bei ipo juu na upatikanaje wake pia ni wa shida. Mara nyingi naona wenye magari hayo wakilazimika kuagiza spare Nairobi. Hiyo Suzuki Escudo (wewe umeiita Helly Hansen) ndiyo gari ya kununua. Ni 4WD ya mlala hoi. Gari imara ambayo kila fundi magari hapa TZ ameizoea na spare zake zinapatikana kila kona ya nchi hii kwa bei nafuu. Engine zake ni 2000 CC hivyo matumizi yake ya mafuta pia ni mazuri. Ila tatizo kuu ni wizi wa "Power Windows". Hivyo inabidi uwe makini ni wapi unapaki gari lako.

    ReplyDelete
  3. Mimi nina Honda CR-V. Spare zake hazina taabu kupatikana bei yake huwa sio ya juu sana ila ni gari ambayo ukibadili spare itakuchukua muda sana kuharibika. Ni gari ngumu sana. Utumiaji wake wa mafuta kwa kweli inategemea na matumizi yako ya gari, mfano sehemu unayoishi kama ni mbali adha ya foleni inaweza kukufanya ukaichukia gari kwa kuona inakunywa sana ile huwa ni CC 2000. Kwa kawaida nikiweka mafuta full tank huwa natumia kwa wiki 2 na nusu. H/Hansen tatizo lake huwa liko kwenye AC haina nguvu sana ila matumizi yake ya mafuta ni poa sana huwa ni CC 1900. Tusubiri maoni mengine kutoka kwa wataalamu zaidi.

    Hilda

    ReplyDelete
  4. Mzee,
    Gari hapo ni Suzuki Escudo Nomade/Helly Hansen/Godwin. Hizi gari ni roho ya paka na bei yake tokea zianze kuingia zimeendelea kupanda wakati bei ya Honda CR-V imeshuka sana. Kuna sababu nyingine za msingi zifuatazo kwanini Honda huwezi linganisha na Suzuki Escudo. Mosi, Honda engine yake ni kubwa 2000cc, wakati Suzuki escudo zipo za 1600cc, bei ya gharama za mafuta na kubadili oil (service) kidogo ni nafuu kwa Suzuki. Pili, spea za Honda ni gharama kiasi ukilinganisha na Suzuki. Tatu, mafundi wa Bongo bado hawajazipatia sana kuengeneza Honda tofauti Suzuki. Nne, Suzuki kwenye barabara mbovu inapeta vizuri sana tena 80km/hrs wala husikii mashimo, wakati Honda itatafanya hivyo wakati huo huo uwe mwepesi wa service ya mara kwa mara. Tano, mafuta lita 20 unasafiri kms 100 kwenda na kurudi pasipo na matatitzo. Sababu zipo nyingi sana. Kwa ufupi tuwasiliane kwa e-mail na kutembelea link ya web:
    info@johnsoncardealers.com
    http://johnsoncardealers.com

    ReplyDelete
  5. Mimi ninayo Honda CRV na sina matatizo nayo. Nimeendesha zaidi ya 1000km non stop na sikuona matatizo nayo. Kuhusu Spare zinapatikana kwa mafundi maalum na ukisha miliki hiyo utawajua tu.
    Ni gari spacious si compact kama Escudo. Ukimiliki Honda unafaidi maana lina nafasi ya kutosha.. suspension zake poa na kwa kweli ni raha.

    ReplyDelete
  6. Suzuku Vitara ndio gari, cc ni 159..ambayo ni 1600,ni moja ya 4wd chache ambayo inatumia mafuta kidogo, nafikiri raking the 2nd from Toyota Cami na Terios(1300cc) nimeshaiendesha na ninaifahamu, off road nzuri sana na iko stronger than Honda, Honda nyanya! wala usijaribu,

    vitara easy ku mantain, ila honda ni more confortable than vitara, so depends unataka uimara au comfort zaidi,ila tatizo la vitara ni wizi wa spare, na wezi wanaingia ndani ya vitara kama kwao vile muda wowote, ila unaweza kudhibiti na kimsingi wizi wa spare za vitara umepungua kidogo ukilinganisha ni ilipokua gari common miaka kama mitano iliyopita,

    nafikiri kutokana na watu wengi kununua magari mengine latest kama GX100,110,CRV, Cami, terios nk nk, na soko la vifaa vya vitara limeshuka kidogo, but vitara is still the best!but get it in 5doors, 3 doors haiko stable sana hasa ukiwa off road,

    alll the best

    ReplyDelete
  7. Mathew
    Hi all
    That is Fantastic ila kwa Gari zisizo na Uchakavu haoa Tunaongelea suzuki ya kuanzia mwaka 2002 (suzuki mayai) na Honda CRV ya kwanzia 2002 Second generation zote ni cc 2000 leteni Tofauti za kinifu na siyo Ushabiki kwa spare nakubali za Honda zipo juu kidogo hilo halina mjadala kwa safety CRV inazidi honda maana hata mimi naweza fungua escudo kwa waya kwenye mlango kama umefunga sasa leteni hoja bora maana hapa tunahitaji kipi zaidi ili watanzania wenzenu wapate ushauri bora

    ReplyDelete
  8. suzuki zipo kuanzia cc 1600, 2000,2500 kuna straight engine na v6 engine.
    tatizo la haya magari kama suzuki, toyota ni wizi wa kama sio gari lote basi wewe kila siku utakua unanunua vitu kama power window yani ukikaa sehemu unakua huna amani. mi ndo maana napenda magari kama honda au VW asiku danganye mtu spare zote zipo mjini sema tatizo spare za honda ni ghali kwa sababu sio fake. kwa suzuki na toyota spare fake ndo zimejaa mjini na ukipata hizo wanazosema ni genuine huwa ni semi genuine.
    Mdau Bongo forever

    ReplyDelete
  9. MwnaharakatiMarch 05, 2011

    Mdau i aint speaking for long. Gari hapo ni suzuki Hally Hansen. Mengine of your choice achana nayo. Honda zote ni ugonjwa wa moyo na utaja juta and then worst thing ukinunua huwezi kuiuza. Kinyume na hivyo go for any toyota car, spare zipo dunia nzima and reasonably cheap.

    ReplyDelete
  10. Napata tabu na jinsi Watanzania tunavyofikiri,nadhani hali ya nchi yetu kiuchumi,kijamii na kiutamaduni imeanzia kichwani!!!.mtu mzima anafikiri kuwa ubora wa Toyota unaletwa na upatikanaji wa urahisi wa vipuri!?,hivyo Honda si bora kwa sababu spea zake ni ngumu kupata!!!.nadhani bado hatujajua nini maana ya ubora.Toyota inatumika dunia nzima kwa sababu ni gari imara na siyo eti kwa sababu vipuri bandia vimejaa kibao,vivyo hivyo kwa Honda,Ulaya, Asia na Marekani wanaitumia Honda si kwa sababu spea zake zinatolewa bure isipokuwa ni kwa sababu ni gari ya kuaminika na ya uhakika.kama Tanzania hakuna vipuri vya Honda hilo si tatizo la Honda bali ni hitaji la soko.Mdau leta gari yoyote Tanzania ufurahie maisha,sasa hivi vipuri vipo tele kanzia halisi,bandi mpaka vya mitumba

    ReplyDelete
  11. Ukimiliki honda crv sio rahisi kupenda escudo wala Rav 4

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...