Uncle habari za leo.
Mimi ni mdau niliyeko Mkoani Shinyanga. Nimeona picha na msongamano wa magari kule kwa Babu kwa ajili ya kunywa dawa. Umati ni mkubwa na kwa taarifa hali ya chakula ni ghali.
Mimi naomba mawasiliano ya Babu niweze fanya “APPOINTMENT’ kwani nina mdogo wangu ana HIV na naamini hata yeye anaamini kwa Babu atapona. Naomba sana msaada huo kutoka kwa wadau wenye kujua japo namba yake, maana sitapata pesa ya kwenda kusubiri siku nyingi huko kwa Babu.
Mdau Shinyanga
Kwa mujibu wa watu walioenda huko ni kwamba, babu hana hata muda wa kupokea asante au discussion, ukifika pale ni kwenda kunywa dawa tu. Gharama hazikwepeki na kama upo Shinyanga njia rahisi ni kwenda hadi Mugumu, Serengeti kupitia Bunda. Unachotakiwa ni kupanda gari gari mpaka Bunda alafu unapanda gari nyingine kutoka pale Bunda mpaka Mugumu-Serengeti kwa nauli ya shilingi 5000 kwa kila mtu na ukifika Mugumu utapata usafiri nafuu wa gharama ya shilingi 30,000 kwenda na kurudi Mugumu kisha utaendelea na safari yako ya kurudi. Huo ni usafiri ambao unaanza kuanzia kesho wengine gharama zao ni kubwa sana.
ReplyDeleteni vyema kwa maombi yako lakini kwa bahati mbaya au nzuri babu hatoi dozi kwa apointment yani huduma yake ni lazima ufike pale na ukiweza usubirie foleni mpaka zamu yako ifike
ReplyDeletebabu kaoteshwa kutoa huduma hiyo kwa bei ya shilingi mia 500 yani jero
sasa ili kukamilisha huduma hiyo ni lazima uchangie michango mbali mbali ikiwemo ya kuwaungisha wenye kuuza vyakula na wenye usafiri.
pole sana kwa huyo mdogo wako ambae ameathirika na ugonjwa mbaya wa ukosefu wa kinga mwilini
nina imani kuwa kwa uwezo wa mungu atapona kupitia miujiza yake ya kumtumilia babu.
mdau wa mahakama kuu ya dunia ambae nategemea kumuomba ankal niwe mkwe wake kwa maana aniwekee bint yake
Mdau toka Shinyanga, pole. Huko kwa Babu hakuna mawasiliano ya aina yoyote ile, hakuna mtandao wowote hapa nchini unaopatikana pale. Kaza buti ujitahidi umpeleke huyo mdogo wako mwenyewe.
ReplyDeleteKWA MGANGA WA KIENYEJI HAKUNA APPOINTMENT, WAHI UKAPANGE FOLENI, UKISHANGAA SHANGAA UTAKUTA MTI UMEISHA AU KACHANGANYA MAJI MENGI DAWA HAIFANYI KAZI TENA. SHAURI YAKO HA HA HAA HAAAA...mpe mdogo wako dawa za kueleweka akichanganya na maisha salama na chakula bora ana chance ya ku-survive kama mtu asiye na HIV.
ReplyDeleteWewe unayejiita mdau kutoka Shinyanga. Kwa uzoefu wa kusoma na kuandika maoni magazetini, najua watu wengi hawasemi ukweli kwamba ni wao wenyewe ndio wanaoumwa ukimwi. Lakini kwa kukufahamisha ni kwamba kama wewe unaumwa, hakuna atakayekuwakilisha kwa Babu katika jambo lolote. Ni lazima uwepo kwa Babu wewe mwenyewe na kuimwaga siri yako kwake. Hata hivyo, wadau wenzetu wamekupa njia ya kufika kwa Babu, ingia mzigoni kuichangamkia safari yako ya kwenda kwa Babu, na ninakutakia mafanikio mema.
ReplyDeleteIt's Great To Be Black=Blackmannen
Anza kumpa mlonge kwanza, ulizia unauzwa huu paketi shs 1000 au 500 utasaidia sana kupandisha kinga za ndugu yako kabla hajaenda huko kwa babu.
ReplyDeleteKwa wanaobisha kuhusu huu wonder tree just google moringa olifera, basi utaona kazi yake, nimeweka hivyo ili msifikiri na mimi nimeota la hasha!