Mdudu gani huyu?
Ankal na Wadau wa Globu ya Jamii
Kwa muda mrefu sana niewahi kusikia kuwa kuna mdudu ukimkanyaga unapoteza kumbukumbu kwa muda fulani, mfano kama unatembea kwenye vinjia vya porini unarudi nyumbani basi unaweza kupotea usikumbuke nyumbani kwako ni wapi mpaka watu waje kukutafuta.
Nimejaribu kutafuta jina la mdudu huyu na picha yake sijafanikiwa mpaka sasa. Ila katika kuuliza kwangu watu wengi wamepata kumsikia mdudu huyu lakini hawamfahamu kwa jina wala anafananaje, ila kuna bwana mmoja tu akanambia anamfahamu na jina lake kwa kimasai ni Taire au Taile na anafanana na kinyonga lakini ni mdogo sana wala habadiliki rangi na ana rangi ya udongo ndio maana sio rahisi kumuona kama yuko porini.
Kama kuna mtu yeyote anamfahamu mdudu huyu naomba kujua jina lake la kiswahili au la kisayansi kwa maana nimevutiwa sana na habari zake na ningependa kujua zaidi.Mimi ni mpenzi wa vijidudu vyenye hadithi za ajabu (bugs with wierd stories).
Asanteni
Mdau Dar

Mdau nakushauri uende Loloiondo, Kikombe kimoja tu cha babu, utakumbuka jina na picha ya huyo Mdudu.
ReplyDeleteMimi ninafahamu kwa kimasai anajulikana kwa jina la NAIKANG'A na anafanana na FUKUSI tofauti kati yao ni kuwa yeye ni mkubwa sana ukimlinganisha na fukusi
ReplyDeleteTanga (Muheza) wanamwita SETA. Ni kweli yupo kama kinyonga na hizo ndio sifa zake.
ReplyDeleteEh bwana, umenikumbusha mbali sana. Nilikuwa jeshini Makutupora, lakini nilikuwa nimechaguliwa kucheza gwaride la kumuaga marehemu Mwalimu Nyerere, kwahiyo tukaletwa Ruvu ili tujitayarishe na tushonewe sare zetu ambazo tutazivaa siku hiyo ya gwaride. Nikakutana na wenzangu ambao wote tunatoka Dar, wakaniambia kuwa wao weekend huwa wanatoroka na kuja Dar tukaagana kuwa Jumapili tukutane kituoni ili turudi wote kambini. Tukapanda basi, tukafika Ruvu, sasa hiyo njia ya porini ya kuingilia kambini wenzetu ndiyo wanaijua, sisi hatuijui, huyo mmoja ambaye anajua njia ninafikiri ndiyo alikanyaga huyo mdudu. Tulifika Ruvu saa moja usiku, na ninasikia sio mbali sana kufika kambini kutoka kituoni kwa njia ya porini. Mpaka saa mbili usiku sisi tunazunguka tu. Mwisho tukamwona mama mmoja akatuelekeza njia, lakini bado tulipotea tu. Tukazunguka mpaka tukakutana tena na yule mama, akashangaa kweli na kusema hamjafika tu! Saa hizo ni saa tatu na nusu usiku. Akasema ngojeni niwape kijana wangu awaelekeze, ndiyo yule kijana akatuelekeza, ila karibu tufike tu, tunasikia bigula la kwenda kulala yaanai saa nne kamili usiku. Na hiyo ina maana usionekane unatembeatembea kambini ovyo, lakini tulifika, ila cha moto tulikipata kutembea masaa yote hayo... S.c. Mdau Toronto
ReplyDeleteanaitwa chechere
ReplyDeletekaka kuona! sina uhakika lakini
ReplyDeleteMimi nkumbuka sana hizo hadithi za kuruka mdudu lakini ukweli nadhani hakuna kitu kama. I think those are just legend tails and myths...I could be wrong but I am positive sure there is nothing like that....
ReplyDeleteAnaitwa Masawe kwa kichaga
ReplyDeleteWewe Mdau wa Toronto umenikumbusha mbali sana, mimi nilikuwa JKT Ruvu na pia nilikuwa kwenye gwaride la kumuaga Mwalimu ambapo Kamanda wake alikuwa Brigedia Jenerali Gideon Sayore ( Luteni Jenerali Mstaafu) natamani nikufahamu ili nikaangalie ile picha niliyonayo. JKT tuliambiwa kuwa tulifanya vizuri sana.
ReplyDelete