Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Leonidas Gama (kushoto),
akipokea msosi kutoka kwa Doto akiwa Grace Nicolaus
Grace Nicolaus kutoka Uk akitoa tarifa kwa waandishi
wahabari mpango mzima wa Timu Saidia Gongo la Mboto UK
Picha ya pamoja baada ya makabidhiano

Timu ya Saidia Gongo la Mboto UK Ikiwakilishwa na DOTO NYADUNDO toka UK ilipeleka msaada wa chakula mapema Jumanne hii ikiwa ni sehemu ya pili ya ahadi zao tatu walizotoa kwa ajili ya kuwasaidia wahangwa wa Gongo La Mboto walishirikiana na bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta Sugu Kisima cha Burudani’ walikabidhi msaada wa chakula jumla ya kilo 400 kwa mkuu wa wilaya ya Dar es Salaam Mhe Leonidas Gama. Vilevile Mkurugenzi wa Twanga pepeta iron Lady Asha Baraka alikabidhi michango yao.
Timu ya SAIDIA GONGO LA MBOTO UK imetoa misaada katika makundi matatu:

1. Pesa taslim sh milllion moja na nusu
2. Chakula ambacho kimeshakabidhiwa
3. Nguo, viatu, vitabu na vifaa mbalimbali ambavyo vimepakiwa kwenye kontena tayari kwa safari ya kuja Tanzania

Aidha mkuu wa wilaya ya Dar es Salaam Mhe Leonidas Gama amewashukuru na kuwapongeza watanzania wachache walioko UK waliojitolea kutoa michango mbalimbali kwa ajili ya kusaidia wahangwa wa Gongo la mboto. Shughuli hiyo ya uandaaji na ukusanyaji wa michango hiyo kutoka Uingereza iliandaliwa na Shilla Frisch, Jestina George kutoka MISSJESTINAGEORGE.BLOGSPOT.COM, Frank Eyembe na Baraka Baraka wa URBAN PULSE CREATIVE na Bernard Chisumo kutoka Locus Impex Shipping Co.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Go, go, go, go mwana wa Nyadundo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...