Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila akitoa maelekezo kwa maelfu ya wageni wake waliofuata dawa nyumbani kwake kijiji cha Samange kata ya Godigodi wilayani Ngorongoro leo. Kuna wasiwasi kwamba maelfu ya wagonjwa na wanaotaka dawa hiyo inayopatikana kwa bei ya shilingi 500 (jero) Sehemu ya mmea unaotumika kuchanganyia na kutoa dawa hiyo
Madawa yakichemshwa...

umati nyumbani kwa babu
Hii ni foleni ya magari leo yenye urefu wa karibu kilomita 10 ikiwa inaelekea Katika kijiji cha Samange katika kata ya Digodigo wilayani Ngorongoro kwa babu anayedaiwa kutibu magonjwa matano sugu yakiwemo Ukimwi,Kisukari ,Kifafa, presha nakuparalazi kwa gharama ya shilingi 500 tu
Foleni ikiendelea...
Hakuna kulala leo
Wananchi wakiwa wamejipanga kwa ajili
ya kunywa dawa nje ya nyumba ya babu


Picha zote na Woinde shizza
wa Globu ya Jamii, Loliondo





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. Ama kweli Watz hakuna msomi wala asiye na elimu sote tuko sawa.

    Bila ya kupata proof yo yote tayari maelfu ya wasomi na masuti yao wanakwenda kupata kikombe cha dawa. Laaa haulaaaaa!

    Mungu atusaidie

    ReplyDelete
  2. Mungu ametusaidia kwa kumleta mtu wa kutibu magonjwa sugu. Ashukuriwe MUNGU

    ReplyDelete
  3. Hiki ni kipimo cha imani ya mtu. Tunaunywa dawa za hospitali kwa sababu wengine walikunywa wakapona lakini dawa hizo zinatengenezwa na binadamu kama huyu mchungaji. Hizi ni alama za nyakati na Mungu anajidhihirisha kwetu kwa namna ya pekee. Enzi za kale, Mungu alitumia manabii kama Nuhu kupeleka ujumbe kwa watu kwamba gharika inakuja waingie ndani ya safina. Kwa vile Nuhu alikuwa mwana jamii kama wao hakuna aliyemuamini. Gharika ikaja watu wabishi wakaangamia. Hivyo badala ya kumpinga huyu mtumishi, tumwachie Mungu afanye kazi yake. Kama wazungu wameshindwa kutibu kisukari na kansa, kwa nini tusimpe huyu babu nafasi? wangapi wannapoteza maisha kila siku kwa wakiwa kwenye majaribio ya dawa za wazungu? nchi za dunia ya tatu sasa hivi ndio sehemu ya majaribio. Madaktari wetu wote wanasafiri nje kuja kuchukua dawa za majaribio bure na kuziuza kwetu. Unabisha? nenda airport uliza madaktari wangapi wanasafiri leo tu utastaajabu. Hitimisho langu ni kwamba Mungu anaweza kufanya uponyaji kupitia ngozi nyeusi sio lazima iwe nyeupe. Fungukeni macho kapateni tiba na mshukuruni yeye aliye juu mbinguni.

    ReplyDelete
  4. WANAO JIFANYA WASOMI WENGI NI WAJINGA KWA SABABU WAMEFUNDISHWA SIJUI WEWE UNAISHI WAPI?? MIMI NA ISHI USA WATU WANAKULA DAWA HAPA HAMBAZO ZIMEZIBITISWA NA SERIKARI ALAFU BAADAE WANASEMA SIO NZURI NA ZINAUA WATU. KWENYE VYAKULA VYA MAREKANI KILA KITU KIMEANDIKWA LAKINI WATU WANANENEPA HOVYO KAMA MAGURUWE YA KUFUGWA INAONEKANA WEWE UNA KASUMBA YA KIKOLONI WACHA WATU WALE DAWA NAJUA BAADAE MZUNGU HATAKU UZIA HIYO DAWA BAADA YA KUWEKA MAHANDISHI NA USOMI WAKO.

    ReplyDelete
  5. anon hapo juu,tambua mkuu kwamba kuna kusoma na kuelimika,na kuna kusoma na usielimike pia,hasa kama bado mtu anakuwa hawezi kufikiri akizingatia ukweli thibitika(fact)from the knowns to the unknowns.
    hii unayo inayoona inajitokeza ni mass psychosis(vurugu la maono la kundi kubwa) ambapo sasa haijalishi huyu ana gari na suti au hana wote wanawahi.
    ninafahamu kwamba dawa nyingi zinatokana na mimea pamoja na wanyama pia hata wakiwemo bacteia na fungus,ila pia ndani ya viti nilivyo taja kuna sumu nadipia,ndiyo maana hadi kupata dawa ni hatua ndefu inayo ambatana na kutenganisha kile kinachohitajika na kisichohitajika, kisha kile kinachohitajika kiwekwe ktk kiwango kinachostahili kutoa matoke chanya ya kitiba.
    zoezi hilo huchukua muda mrefu ikiwa nipamoja na kufanya majaribio kwa viumbe waliokaribiana na binadamu ktk mfumo wao wa utendajikazi wa mwili,na hapo matokeo yasiyotarajiwa(side effects)za dawa husika hutambulika pia.
    sasa kwa upeo wangu nilionao nawashauri wanaokimbilia hiyo dawa washike breki kwanza,maana wanaweza jutia baadaye madhara yanayoweza kujitokeza(mungu pishilia mbali). traditional medicine siyo kuchimba dawa na kutibia kiholela tu,bali kabla ya kutibu inapaswa ujue mechanism ya ugonjwa unaotaka kuutibu ndipo pia ujue dawa unayoitoa inatakiwa ifanye kazi gani ktk kuzuia ule mlolongo husika unaopeleka ugonjwa husika kujitokeza.
    sasa ukiniambia babu anatibu kifafa,kisukari,HIV N.K WAKATI HUYO BABU HAJUI HATA mechanism moja katika hayo magonjwa,itakuwa nikujidanganya mwenyewe nafsi yako.
    kwa kumalizia,nasema DAWA ZINATIBU ZIKITUMIKA SAHIHI na DAWA ZINAUWA na kuleta madhara pia zikitumika bila uangalifu na elimu ya kutosha kuzifanyia kazi.

    ReplyDelete
  6. ehh wacha tuone kama inatibu kweli tutajua maana huo umati si mdogo na wala si lakulitolea maamuzi bado mapema sana saivi ata uyo mtu akizaliwa bas hawi siku hiyo anachukua muda kwanza. ata hao madabii hawajasema siku moja tu wakakubalika walichukua muda na wakaonesha ishara zilizo wazi kabisa then pale ndio watu wakaamini na waliokataa ndo wakapata harika . kwa hiyo huwezi kumfananisha mapema yote hii. kama inatibu kwa tanzania itajulikana. haraka za nini. kila kitu ni proof kuna watu wanasema wanatibu kwa miujiza hapa na mpaka leo watu wamejaa tele mahospitali kwa matatizo hayo hayo kwanini wasiende kumalizia kwenye miujiza tu .
    na kama pana ukweli basi utajulikana sku zone penye ukweli basi uonge hujitenga.

    ReplyDelete
  7. Extraordinary popular delusions and madness of the crowd......

    ReplyDelete
  8. ANAYECHEKA WATU WANAOTAFUTA TIBA NI MCHAWI. ANAYEKEBEHI WATU WANAOJITAHIDI KUBORESHA AFYA ZA WENZAO NI MCHAWI. ANAYEZOMEA MEMA NI MCHAWI. ANAYEVUNJA MOYO WENZAKE WANAOFANYA JUHUDI KUONDOA MATESO NI MCHAWI NA INAWEZEKANA YEYE NDIYO CHANZO CHA MAGONJWA YA HAWA WATU.

    WACHAWI WOTE WASHINDWE!

    ReplyDelete
  9. HAMNA CHA NINI WALA NINI HIZO PANADOL UNAZOPATA ZIMETOKA HUKO HUKO KWENYEE MIMEA NA KUONGEZEWA CHEMICALS ZA AJABU TU KWASABABU YA BIASHARA. MITI SHAMBA NDIYO YENYEWE AS LONGER SIO SUMU MTU HAJAFA BAADA YA MASAA 24 THEN NI ZENYEWE KUTHIBITISHA NINI! HUKU MAREKANI HAWATAKI KUTHIBITISHA DAWA ZA CANCER FOR BUSINESS PURPOSE SASA HIVI TUNAIELEWE VERY WELL CAPITALISM SYSTEM OR SCIENTIFIC SYSTEM AMBAO IMETENGENEZWA NA BINADAMU KAMA MASAPILE, AMBAYO IS ALL ABOUT MONEY FLOWING NOT THE WELL BEING OF LAYMAN AT ALL. NENDENI NDUGU ZANGU MKACHUKUE HIYO DAWA MPONA. HAO WAZUNGU WAMELETA MADAWA HAYO YOTE KWASABABU YA KUJIPATIA HELA WAO WENYEWE. KUNA DAWA NYINGI WATU WEMEGUNDUA LAKINI CAPITALIST PEOPLE WAMEZUIA KWASABAU YA BUSINESS, MIMI NAFANYA KWENYE HOSPITAL KUBWA HUKU MAREKANI NIMEJIFUNZA MENGI NENDENI. HERBAL(MITI SHAMBA) NDIYO YENYEWE SASA KWAKUWA TUMEGUTUKA NIA ZA WAZUNGU KUTUUA TU NA KULA KILA SENTI YETU. NENDENI MUNGU MKUBWA KASIKIA KILIO CHA WENGI WALIOPTEZA MAISHA YO BILA HATIA.

    ReplyDelete
  10. HAHA KUNA DAWA NYINGI ZINATOLEWA NA WAZUNGU WANATANGAZI KILA SIKU KUWA ZINATIBU, NA BAADAE ZINATOREWA KWENYE MASOKO WANASEMA NI HATARI AZITIBU. NACHOTAKA KUSEMA MUACHE HUYO MAZEE HAJARIBU KAMA ZITATIBU SAWA NA KAMA AZITIBU TWENDE MBELE MAISHA NI KUJARIBU. WATU WAZAMANI WALIKUA WANAISHI MDA MLEFU KWA DAWA HIZO HIZO NA AO WASOMI WANAKULA MDAWA YA KIZUNGU WANAISHI MIAKA 55 NA WANAKUFA NA MADAWA HAYO HAYO YALIYO ANDIKWA NYIE NDIO MUNAO WAUA WAZEE WETU MNASEMA NI WACHAWI NA KASUMBA YENU YA KUJIFANYA WASOMI.

    ReplyDelete
  11. huyo anayesema sijui mechanism sijui nini,babu zake wakati wanakula miti shamba wakiumwa enzi hzo kulikuwa na hao wataalamu?na wamasai mpk leo wanakula miti shamba na wanapona?Mungu ana shani yake,huyo aliyewapa akili ya kuwaingiza nyie darasani ndio aliyempa babu bila kuingia darasani..unafikiri hao wazungu hata wakiwa dawa ya ukimwi watakupa kwa jero wakati wanajua kwenye gonjwa la ukimwi kumewapa ajira watu wengi duniani na wanaingiza pesa nyingi kwa dawa za kupunguza makali!?acheni ujinga na ulimbukeni wa kushobokea wazungu

    ReplyDelete
  12. kwa mtu aliyekata tamaa inakuwa vigumu sana kumkalisha chini umpe somo hadi akuelewe. hasa kama haoni njia nyingine mbadala. swala hili kwa sasa itakuwa nivigumu kulizungumzia,hadi hapo muda utakapo pita ndipo kila mmoja atapata majibu sahihi kuhusiana na hili jambo.
    kama nilivyosema awali kwamba dawa hutoka ktk mimea,wanyama na hata wadudu, huenda kweli ndani ya huo mmea kukawa na chemical substances zenye matokeo flani mazuri. lakini kuithibitisha ndani ya huu muda mfupi kuwa nidawa mkombozi hapo panakuwa pagumu kwakuwa hilo halitatokea leo wala kesho,nijambo la muda mrefu sio chini ya miaka kumi hata kama itakuwa kweli ni dawa inayotibu.
    labda iwe ni muujiza ulioletwa na mungu kuwaokoa watu blindly bila kuwa na madhara mengine hapo nitakuwa sina chakuongezea. lakini tofauti na hapo mmmmh sijui nikuelezeni vipi.
    mfano mzuri ni thalidomide, ilikuwa ni dawa iliyowaondolea karaha waja wazito,lakini matokeo ya side effect yake yalipoanza kujitokeza mbona ilikuwa ni huzuni duniani walioanza kuzaliwa watu walemavu.
    kumbukeni,kutokuelewa jambo hakukuepushi na madhara ya jambo hilo. miamea mingi tu hata baadhi ya vyakula pia husababisha matatizo chungu tele kwasababu tu watu wanakuwa hawana habari kuhusu hilo,na wengi kwa muda mrefu wanapoteza maisha kwa magonjwa yanayotokana na utumiaji wa vyakula hivyo bila hata kujua wala kuhusisha magonjwa yao na vyakula hivyo.
    sasa tukisha iita dawa,tutegemee utumiaji wake kuongezeka maradufu,na ikitokea ina madhara basi tutegemee baadaye mlipuko wa madhara yake kama second phase ya matokeo yake.najuwa kwa wenye HIV wengi wanafumba macho tu na kusema to hell let me try it!lkn tukumbuke HIV sio hukumu ya kifo,wenye virus wanahaki ya kulindwa na madhara yoyote yanayoweza kuwapata wasio na virus na walio navyo!.
    kuna mambo mengi sana ambayo jamii zetu zinapaswa kuyafahamu,japo kwa sababu mbalimbali wanakosa kuyafahamu,na hapo ndipo chanzo cha matatizo ktk nchi zisizo endelea kote duniani kilipo.
    "MSHIKE SANA ELIMU WALA USIMUACHE AENDE ZAKE"
    ktk dunia hii huwa hakuna kitu kinachojitokeza from nowhere,siku zote kuna principle of CAUSE-EFFECT relationship. ukifanya jambo flani tegemea matokeo flani,ama mazuri ama mabaya.sasa tujifunze pia kuwa responsible kwa matokeo yanayotokana na maamuzi yetu na kile tunachokitenda.

    ReplyDelete
  13. Mimi ni mtanzania niishiye huku Marekani nimezipokea kwa furaha na faraja taarifa za matibabu ya Babu Jero;kumbukeni kila jambo lina mwanzo na mwisho wake, babu huyu ni mwana harakati katika kutatua matatizo yanayoikabili dunia hii kwa magonjwa sugu, kwa hiyo aendelee kutibu asizuiwe mpaka pale dawa hiyo itakothibisha madhara yake yenyewe au faida zake,pia kwa upande wa wataalaamu wa Muhimbili wanatakiwa wampe tafu babu Jero kiutafiti kuliko kumbeza tu. kila mwanasayansi/ mugunduzi huasiri maisha yake au ya viumbe wengine kabla ya proof, mwisho anayependa kufanya majaribio na Jero hana ubaya mimi namwita ni mzalendo wa kujitolea kwa maisha yake au ya watu wajao.
    Hakuna dawa inayofanikiwa kutibu watu pasifokuwa na majaribio ya hapa na pale kwa Babu Jero wasimuonee wivu kwa umati ule unaokusanyika kwenye clinic yake,Kumbukeni Dawa nyingi za ukimwi zilitangazwa na watu wenye kujiiita Madakta wa Kiasili/miti shamba lakini matokeo yake zilishindwa na watu alizitupilia mbali nakumbuka nilipowa Tanzania 1998/9 ilitokea Dawa inaitwa Monox ilitangazwa sana magazetini na Radioni. Huu kama ni upepo uacheni utapita tu.

    ReplyDelete
  14. Hakuna dawa kipimo kimoja ikatibu maradhi yote.

    Angelikuwa anatibu say Ukimwi tu ningeamini, lakini haijalishi maradhi kila mtu anapewa kikombea kimoja! hapo nakataa

    ReplyDelete
  15. Huu ndio mwisho wa dunia jameni kuueni na akili. Hivi huo umati wote wa watu na magari foleni kilomita kumi na sufuria inayotumika kuchemshia hiyo dawa haiwezi kutosha hata kwa kutibu watu ishirini.

    ReplyDelete
  16. we mtanzania hapo juu unaesema sayansi umeijua wapi sayansi? au unaropoka na kuwa tu brain washed na wazungu na mila zao? nyie ndo mnaoiangamiza tanzania na africa kwa kubeza vya kwenu!uwe na upeo japo kidogo usiropoke tuu kama mwehu! NAMTAKIA BABU AFYA NJEMA NA MUNGU AENDELEE KUMPA NGUVU ATUSAIDIE WATU WAKE.MUNGU AMESIKIA KILIO CHA WATU KWA MAPIGO YA MAGONJWA HAYO!AMINA

    ReplyDelete
  17. Tunaomba ushuhuda wa yeyote aliyepona kwa kunywa dawa ya babu ili kuwatoa hofu na kuwapa imani wale wasioamini

    ReplyDelete
  18. mungu mkubwa jamaa zangu kadha wamepata pata tiba na wanaendelea vizuri taasisi za serikali wasimbanie babu jero

    ReplyDelete
  19. ...Kuna makundi kadhaa nayaona yanabishana na kukatisha watu tamaa hapa!
    1. Kundi la wamiliki wa NGO za Ukimwi, (hawapendi Mchungaji Ambilikile atibu Ukimwi, wao watakufa njaa, hawa hawapendi hata dawa ya kutibu Ukimwi ipatikane)
    2. Wamiliki wa hospitali binafsi (hawapendi watu watibiwe magonjwa sugu ambayo wao huwaingizia kipato kinono, kama vile kisukari)
    3. Watu kutoka serikalini, ambao wameota vitambi kwa pesa za miradi Ukimwi, ambazo haziwafikii walengwa. Hawa nao hizi habari za Mchungaji Ambilikile sio nzuri sana kwao.
    3. Akina Tomaso, wao na imani ni mbalimbali! Hawa nao hawaamini kitu hadi kiwafike wenyewe. Pamoja na kusoma lakini hawajaelimika.

    ReplyDelete
  20. safi sana
    dawa za wazungu zinatuua tu kila uchwao
    miti-shamba ndo asili yetu na tutaitumia tu

    viva babu

    ReplyDelete
  21. mnagombana nini hapa na kuonyeshana ubabe wa nini, atafutwe mtu mwenye cancer, hiv, diebetic, wapewe hiyo dawa wanywe, kisha wafwatiliwe kwa walau 5yrs, ndio kitaeleweka kama inatibu au vipi, mnagombana hakuna hata mwenye proof to eirther side of the story, kabla ya hayo mwacheni mchungaji afanye kazi.

    ReplyDelete
  22. babu hongera kwa kugundua kidawa moto moto, hii ikiwa kweli wabongo tutapata atlist ka one patent life will be good we acha tuu. Msimonee babu wive unajua discoveries most of them in our time zimepatikana na dream… we awasemagi tuu wale wasomi waliota ala alafu wakapata kajibu...

    ReplyDelete
  23. babu adumuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu

    tuimbe tumeponannnnnnnnnnnnnnnnnnna * 2!

    ReplyDelete
  24. kwakweli huyo babu ameletwa na Mungu kwaajili ya kuokoa watu, jamani naomba watu tusimdharau huwezi jua hiyo yote ni maajabu ya Mungu. Wale wote wanaofurika kule c wajinga bali wana shida zao hivyo ni busara sana kuheshimu maamuzi ya mtu na si vinginevyo kwa kuwakejeli. Tumuunge mkono babu na Mungu ampe nguvu azidi kutoa huduma kwa wananchi.

    ReplyDelete
  25. wajinga ndio waliwao, piga fedha babu wakishtuka umeshatengeneza na wewe kau-dowans kako.

    ReplyDelete
  26. imani ni dawa na nikuamni kwa mambo tusiyoyaona wala kuyatarajia
    sas basi tunamshukuru babu kuleta hiyo dawa ila tunaomba kujua historia ya hiyo dawa ameipataje na kwanini hataki dawa itoke nje ya eneo lake?je na kama mgojwa hawezi kuja atafanya nini ili apte dawa

    ReplyDelete
  27. Kula vichwa babu,wanajileta wenyewe hao.

    ReplyDelete
  28. Lazima tukubariane na nguvu za Mungu na tujivunie kuwa mwangaza umeangukia Tanzania, watu wanabisha uwezo wa Mungu Kupitia kwa babu kwa sababu wanafaidika kwa kupitia wagonjwa wa ukimwi kwenye miradi ! sasa waacheni wagonjwa nao wapone Mungu ameshusha neema yake , Tanzania bila ukimwi inawezekana! mambo ya warsha , semina, kongamano wakati watu wanakufa yaishe, Babu endeleaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  29. KUNA TOFAUTI ZA KARAMA ,ROHO MTAKATIFU NDIYE ANAYEMPA KIPAJI CHA UPONYAJI. AMINI. "NENDA USITENDE DHAMBI TENA IMANI YAKO IMEKUPONYA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...