HAbari kutoka mjini Moshi zinasema mamia ya wakazi wa mji huo wamejitokeza kwenye ofisi ya Mbunge wa jimbo hilo, Mh. Philemon Ndesamburo (CHADEMA) kujiorodhesha majina kwa ajili ya safari ya kuelekea kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapile, katika Kijiji cha Samunge, Loliondo anayetoa dawa ya kutibu magonjwa sugu.
Wananchi hao wamejitokeza baada ya mbunge huyo kuamua kutoa usafiri wa bure wa kuwapeleka na kuwarudisha wale wote wenye kusumbuliwa na magonjwa sugu ambayo tiba yake hutolewa na ‘Babu’ baada ya kuona wananchi wengi wanahitaji kwenda ila wanakwamishwa na fedha za nauli ambazo zimefikia kiasi cha shilingi 150,000.
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake jana huku nje kukiwa na misururu mirefu ya wananchi wanaojiorodhesha, Ndesamburo alisema kuwa watawapeleka wananchi hao kwa awamu ambapo kwa kuanzia leo jumla ya watu 73 wataondoka majira ya saa kumi jioni kuelekea Loliondo na wakirudi wataondoka wengine.

So kisa anahela, ila ni kwakua anajali utu na kuthamini mahitaji ya watu wake wasojiweza. Bigg Up ya self men.
ReplyDeleteTunamshukuru Ndesa kwa kujitolea, lakini haoni kuwa antatuharibia soko sisi wasafirishaji, kama anataka sifa akasafirishe wanao kwenda kijijini kwake.
ReplyDeleteMimi naona hizo hela atakazotumia kupeleka watu huko angeweka matangazo na awareness ya kujua jinsi ya kujitunza na kutokupata magonjwa kama HIV< Kisukari , malaria, HB ...Watu wengi bongo hawajui jinsi ya kujiepusha na haya magonjwa.
ReplyDeleteNa kabla hajafanya hivyo angetakiwa kupeleka uchunguzi kuona kuwa hayo matibabu ni ya kweli au ni kupoteza hela tu...