Na Woinde Shizza wa
Globu ya Jamii, Arusha
Globu ya Jamii, Arusha
Jeshi la polisi mkoani Arusha leo limewapeleka askari wilayani ngorongoro katika kata ya digodigo kijiji cha samange kwa mchungaji anayetoa dawa kwa ajli ya kuimarisha ulinzi.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani hapa Thobias Andengenye alisema kuwa jeshi la polisi limeamua kuongeza askari katika eneo hilo ili kuweza kuimarisha amani na kuweza kusimamia eneo hilo.
Alibainisha nia ya haswa ya kuwapeleka polisi katika eneo hilo ni kusaidia kuangalia jinsi ya kuboresha huduma pamoja na jinsi ya kuharakisha safari watu wawewanaenda haraka na msafara unatembea.
Alisema kuwa mpaka kufikia jana kulikuwa na askari kutoka katika wilaya za karibu ambapo alisema kuwa kuna askari polisi kutoka loliondo na wengine kutoka katika wilaya ya Ngorongoro lakini kutokana na watu kuwa wengi wameamua kuongeza askari wengine kutoka mkoani ili kuweza kuimarisha amani.
"kulikuwa na askari pale lakini kwakuwa watu wameongezeka inabidi askari wetu waondoke Leo ili waweze kwenda kusaidi na kuimarisha ulinzi"alisema Andengenye.
Alibainisha kuwa kutokana na magari kuwa mengi wanawapeleka pia askari wa usalama barabarani ili ili kuweza kusaidia misafara ikaenda haraka sana.
Andengenye alisema kuwa kwa swala la kuzuia serekali hawazuii kwa maana ya kuzuia ila wanahamasisha watu wapunguze kwenda ili waliopo uko wapungue.
Alimalizia kwa kusema watu wanao enao enda wanatakiwa waamini kuwa wanatibika na wajitaidi kuwa wavumilivu wasubiri mpaka wenzao walioenda wapungue ili kuweza kusaidia mathara yasitokee na kusema kuwa wasiofie kwa sababu huduma bado ipo.
Mpaka sasa watu mbalimbali wanazidi kufurika kuelekea katika wilaya hiyo ya ngorongoro kwa mchungaji mstaafu Ambilikile Mwasapile (babu) ambaye ana toa tiba ya magonjwa mengi ambayo ni sungu na ambayo yametafutiwa dawa kwa muda mrefu lakini hayajapata dawa lakini yeye ndiye aliyebarikiwa na mungu na kupata dawa ya magonjwa hayo.
Mwandishi wa habari hizi alizungumza na watu mbalimbali ambao wameshaenda kunywa dawa hiyo na ambao bado hawajaenda kunywa nao walikuwa na mambo mbalimbali ya kusema mmoja wa watu hao alijitambulisha kwa jina la Roda peter ambaye yeye ni mkazi wa kijiji cha Samange naye alisema kuwa yeye anamshukuru mungu sana kwa kumletea mtu ambaye amepata dawa ya kutibu magonjwa haya sugu.
Yeye binafsi alisema kuwa alikuwa ameathiriki na virusi vya ukimwi lakini mara baada ya kunywa dawa hii ya babu alienda kupima mara tatu na akikuta ana virusi kitu ambacho tangu apate hajawai kutegemea kama angekaa apate mtu wa namna hii ambaye atawatibu magonjwa mbalimbali.
"Unajua nilivyokunywa hii dawa nilienda kupima mara ya kwanza baada ya siku saba nikakuta ninao. Nikaenda ya pili nikakuta ninao. Lakini nilivyoenda mara ya tatu uwezi amini nimekuta sina! Acha Mungu aitwe Mungu! Mbali na ilo siku amini nimepima zaidi ya hospitali tatu lakini nimekuta hamna. Acha tu kweli mtu anayemsema huyu babu vibaya alaaniwe kwani mimi kanitibu kabisa nilikuwa nimekata tamaa ya maisha"alisema Roda.
Kwa upande wa mtu mwingine ambaye yeye hajaenda ambaye alijitambulisha kwa jina la Erasto Rafael alisema kuwa yeye alikuwa haamini kama dawa hii ni ya kweli lakini kwa sasa ameanza kuamini kutokana na watu ambao anawajua kwenda na kuwaona wamerudi wakiwa tofauti na wengine wamepona kabisa.
"Mimi nilikuwa siamini uezi amini ninabesti yangu alikuwa analazwa haongee anyi soda yani anafuata masharti ya dawa sukari lakini sasaivi anakunywa mbaya acha tu lazima ata miminiende."alisema rafaeli
Huyu babu kawa wa ukweli sana dunia nzima
ReplyDeleteMimi nitaamini pale shemeji yangu ambae yupo huko tayari anaitwa Emmanuel ambae an ugonjwa wa akili atarudi akiwa amepona au amebadilika kwani ametumia dawa nyingi sana bila mafanikio.
ReplyDeleteMama Avisa wa Usa River
Jambo, samahani kwa kuchangia pasipohusika. Kaka Michuzi, samahani,kwakweli uandishi wa kiswahili unapotoka, hii habari ni nzuri ila kunakuacha au kuweka herufi zisizostahili katika uandishi. kuna tofauti kati ya 'wamekuta ana' na wamekuta hana'.
ReplyDeleteJibu kwa Mama Avisa wa Usa River.
ReplyDeleteMagonjwa anayotibu babu ni 5 na tumetajiwa, hilo la akili halimo. So huyo shemeji yako akirudi hajapona isiwe kisingizio cha kutoamini.
Mimi mpaka sasa siamini, ila majirani zetu 3 wazee wa hapa mtaani kwetu wameenda huko na wanasema wamepona. Ninavyoandika hapa, baba yangu mzazi nae yupo huko Loliondo tangu juzi tunasubiri arudi tukampemi na yeye ana Kisukari na Pressure magonjwa kama ya hao wazee wa mtaani kwetu ambao wamekunywa hiyo dawa na wamepona.
Hivi kwanini wataalamu wa vyuo vikuu huko bongo ama madaktari hapo muhimbili ama kule arusha hawawapeleki wagonjwa kwa mfano wenye saratani ama wenye HIV ili waweze kuhakikisha kama kweli hiyo dawa inafanya kazi tukajua sote....kwasababu ninavyojua mimi bongo watu wanapenda kukuza habari za kusikia na kuzifanya ziwe za kweli..na ni haraka kurukia jambo bila hata kuangalia. eti mtu kapona kisukari sasa anakunywa soda kama kawaida...hii akili kweli kama ni kweli maneno hayo..
ReplyDeleteNaomba kumuuliza huyo anyonymous 04:17:00 PM kuwa kichaa ni yule nduguye aliyeenda kule au ni yeye. Sijaelewa vizuri hapo.
ReplyDeleteLa pili yule mchungaji hatafuti waumini anasaidia wagonjwa wanaoteseka na wamekata tamaa na wanahitaji msaada wa Mungu.
Kuamini au kutokuamini ni masuala binafsi.
waafrika kwa kudangaywa, ehh ndio maanaq wathungu wanatucheka kila kukicha lol
ReplyDeletemimi nitakachokifanya naomba mtu akaichukue hiyo dawa,nitamlipia nauli na nitamshughulikia visa ,aje na hiyo dawa hapa ya kutosha kutibu watu watatu,niwape wagonjwa hao watatu,kisha tutawafanyia vipimo kwa kutumia teknolojia ya mwisho iliyopo hapa duniani ktk kupima HIV kuanzia antibodiea,antigens za sero type za virusi walivyo navyo,kwa kutumia electronic microscoping na marked radio immuno assey,zote zitakapo onyesha hakuna virusi hivyo, tutachukua na sample za cells zake tuangalie receptors za virusi kama ziko free au blocked. baada ya hapo ninaweza kuwa na chakusema. vinginevyo mimi nabakia bado kuwa thomaso.
ReplyDeletekwasababu nina maswali mengi sana juu ya hiyo dawa wanayodai inatibu.na pia uhusiano kati ya majibu yanayopatikana baada ya kupina na aina ya kipimo kinachotumiwa, maana isijekuwa kipimo nicha kuzitafuta antibodies na dawa ukute ina molecular structure inayo bind tkk hizo antibodies na kuzineutralise kisha zinakuwa hazionekani wahusika wanadai wamepona,na kwa imani wanajisikia wazima kisaikolojia kwa kupata majibu -ve.
au ukakuta ina boost immune system inazalisha antibodies zina bind ktk viral antigens,antigens zote zinakuwa neutralised kisha kipimo kinakuwa nichakuitafuta antigen,kikiikosa kinaonekana ni -ve.
hii mimi naomba tuifanye sio kwa lengo baya,bali kwa lengo zuri tu,nakama kweli dawa itaonekana inatibu,nitasimamia hakizote za huyo babu kama mmiliki na mgunduzi wa dawa hiyo hatadhulumiwa, ili mradi tu scientifically mimi nisaidie kuondoa mashaka yaliyopo,na hata akitaka kusaini mikataba kwa masharti yake atakayo yaweka mimi nitasaidia isainiwe bila utapeli.
haya aliyeko huko tz ajitokeze tuifanye kazi hii.
Anon Tue Mar 08, 08:00 pm. si wamesema hiyo dawa lazima akupe babu mwenyewe ndo utapona? sasa wamsafirishe na huyo babu huko USA? we unafikiri watu wamapenda kwenda Loliondo ambako hakuna miundombinu na barabara mbovu? hiyo dawa nimesikia pia haisafiri, sasa sijui huko USA itafikaje?
ReplyDeletehayo mambo unayosema yangekuwa yanawezekana nina uhakika kabisa sasa hivi hayo matibabu yangehamia angalau Arusha mjini kupunguza adha ya mlundikano wa magari huko Loliondo
we any wa march 8 8.00pm umeambia mpaka mgonjwa aende mwenyewe sasa sielewi unaongea utumbo gani wa biashara ya visa wewe kama uamini kaa kimya wanaumwa ndio wanajua mateso wanayoyapata ndio maana wanajaribu kila kitu ni imani yako mdau wa houston
ReplyDeleteMchungaji anahitaji mwanasheria mzuri na asishirikiane na watu wasio na imani kama huyu anonymous wa 08:00:00 ambaye anataka afaidike na pesa kama itaonekana ni dawa ya kweli.
ReplyDeleteSasa iweje kipimo kilichoonyesha ugonjwa mwanzo kitiliwe mashaka kikionyesha ugonjwa hauko tena? Mimi nina jirani yangu amepona ukimwi pamoja na wake zake watatu kwa kunywa dawa hii.
Madaktari wetu hawaaminiwi na wazungu huko walipo wanafanya kazi za u medical assistant lakini wanabeza Mambo makubwa nyumbani.
MICHUZI NIMEFURAI SANA KWA HABARI HII YA HUYO BABU NA KAMA UNAVYO JUA SIJAWAI KUTOA MAONI KWENYE HII BLOG YAKO NA NIMETUMIA JINA LANGU SIJAJIFICHA.NAONA WENGI WANATOA MAONI NA MAJINA YAO YAMEFICHWA NA WANASEMA WANATAKA KUSAIDIA HUYO BABU KU UZA HIYO DAWA KAMA KWELI MNA UO UWEZO TOA JINA LAKO TUKUJUE UNAFANYA NINI NA UPO WAPI? KAMA KWELI MNATAKA KUSAIDIA NENDA TANZANIA KAMCHUKUE HUYO MZEE NA DAWA YAKE MLETE HUKU NI KITU RAISI SANA SIO MNAZALAU WATU WA NYUMBANI KWA SABABU MNAKAA ULAYA WACHA WATU WAJARIBU KUJISAIDIA. WATU WENGI MPO HUKU NJE MNASEMA TU BASI KAMA AMPENDI HUYO BABU MNASEMA MWONGO PELEKENI DAWA NYUMBANI ZA KUWASAIDIA WATU HUKO NYUMBANI.
ReplyDeleteShida ni kuwa Babu mwenyewe hajahitaji kampeni ya huduma yake lakini hapa basi imekuwa kama kichaa kapewa rungu. Kampeni za nini? Unaamini huamini cha nini kutafuta sababu za kuhakikishiwa anaponya ama haponyi? watu wengine bwana. Mleta habari ameileta hapa ili kutujulisha yanayo jiri huko Loliondo kwa huyu mponyaji. Unaamini huamini ni juu yako. Mzee wa watu hajahitaji kukuhakikishia hayo. Sasa kampeni za nini zote? watu bwana mh!
ReplyDeletenimefurah kusikia kwamba, ukipata ukimwi mara ya pili imekula kwako safi sana maana ngono, Watu wangefanya ngono kama breakfast.
ReplyDeleteJamani hehee, me mwenzenu ni mtahalamu wa afya za binadamu, huyo anonyn 8:00pm ameongea point tupu. Kuna uwezekano mkubwa kabisaa kuwa hiyo dawa ina-nutralise Hiv toxins kitu ambacho kinafanya kipimo cha HIV kionyeshe HIV negative, wakati HIV yenyewe ikiwa hapo hapo.Anachosema ni kuwa, kuhakiki hiyo dawa ki-science zaidi kwa vipimo vya kisasa,and confirmatory tests, kama vile ASOT,Elizer vipimo ambavyo vinauwezo wa kupima HIV waliojificha hata kwenye Bone Marrow,na si kwa vipimo vya awali kama vile Capilus Test.Pia ikumbukwe kuwa HIV ni organism ambaye ni most complicated one, with almost six differnt layers, na ndiyo maana dawa nyingi zinazoua HIV zinaua na body cell including Neutrophills.Anoyn 8:00 your totally right..!!!
ReplyDeleteKatika nchi zenye akili, huyu babu angepimwa akili kwanza. Kwa wale tuliokulia darisalama miaka ya 80 na tisini, mnakumbuka hadithi za mzee pangalashaba?
ReplyDeletewatu wengine wanaboa sana humu,sasa kama wewe waweza kumtumia mtu nauli kwanini usiende mwenyewe kuhakikisha na kuongea na hao watu ambao wameshatumia dawa.ama kumchukua mgonjwa wa ukimwi kuhakikisha km ni kweli ana ukimwi we unarukia kumpima tena baada ya kutumia dawa za babu.hiyo km dharau flani.kama waweza amini huwezi kaa kimnyaaa.
ReplyDeleteNimecheka kweli yaani mpaka serikali imesha kubali watu wanaoenda wasiende mara mbili. Ukienda mara moja basi amini kuwa umepona Usirudi rudi...Ahhhh hii inachekesha sana...
ReplyDeleteMimi ni muamini mkubwa sana na Imani yangu ni kubwa lakini kwa hili naomba watu waeeleze kama kweli ni dawa ya huyo mtu na imani kwa nini hiyo dawa isiweze kusafi? kwanini lazima akupe yeye...Na hao waliopona walipimwa kwanza na kuona wana ukimwi halafu wakapona...Bwana unakumbuka wale waliokua wanatembea na magogo Texas na yule mtu wao...Walifika Arkansas wakapona, walivyofika Ohio wakapona tena hao hao kumbe kuna mtu ana kamera...Waliorecord huko TX kulinganisha wakasema jamani walikua TX hawa na wamepona...Leo walikua wagonjwa tena vipi? Toka hapo credibility ya huyo mtu iliisha..Na sijui ameishia wapi....
Halafu huyo pastor mbona jina kama sio la mtu wa huko? alikimbilia nini huko au huko ndio kuna ulaji...Karibu na ule mlima watu wanauita mlima wa Mungu.?
Tuongee ukweli na kuacha kuambiana mtu huyu ana imani huyu hana..Siku hizi kuna technology na tunaweza pima...Pima kabla hujaenda na ukirudi pima...hao wenye kisukari si ajabu waliishia kuwa vegan walivyoenda kuwa huko kwa muda huo kisukari kikatulia rudini mle nyama na carbs kikipanda tena mtarudi tena Loliondo..Twahitaji knowledge ya huu ugonjwa wa kisukari sana..Kama walikua kwenye insulin shots per day haafu hawajaitumia tena toka watoke huko naweza nikafikiria hiyo dawa ina work lakini kama ni kile kisukari cha kule kwetu kila mzee anacho lakini hatumii dawa nitajiuliza tena. je ni displine ya kula chakula bora au? Kama sugar ipo chini sio mbaya kunywa soda once in a while kwa hiyo sioni ajabu huyo anashangaa ndugu yake anakunywa soda sio kapona huko ni kuwa sugar imerudi kwenye normal level..Subiri miezi uje utupe data tena huku...
Katika dunia ya sasa science na technology watu bado wanaamini eti mtu kaonyeshwa na mungu dawa. Mungu anampenda yeye kiasi gani amuonyeshe dawa.Kama unajua cancer au diabetes ni nini itakua niupumbavu kuamini kikombe cha maji kina tibu kwa siku 7. Kwenye Ukimwi atleast naweza kumpa benefit of the doubt....lakini kiaina. Most of the time Cancer na diabetes are geneticaly diseases...ngoja tu...watu watalia huko loliondo. Bongo kwa kukuza mambo...Si tunakumbu ka mambo ya salender brigde na MANYOYA? VIKWAPI? Ni mawazo yangu naweza kuwa wrong.
ReplyDeletewewe kajumulo nazani unaitaji kunywa hiyo dawa pia !!
ReplyDeleteHAHA UKINITUMIA NIJARIBU. LAKINI UJUE NIMEFIKA ULAYA TOKA MIAKA YA 1980 MPAKA LEO SIJAENDA HOSIPITALI HATA SIKU MOJA SINYU POMBE SIVUTI BANGI WARA MADAWA YA KULEVYA NAJILINDA MWENYEWE NA NAJISAMINI NDIO MAANA NAWEZA KUWATHAMINI WENGINE NEMEKULA MITISHAMBA KABRA SIJAJA HUKU KWA WAZUNGU KWA HIYO NATHAMINI MIRA ZETU.HAWA WATU WENYE HIYO SCIENCE NA TECHNOLOGY WANAKUFA KAMA KUNGUNI KILA SIKU NA WANAKULA MADAWA KAMA GARI INAVYO ITAGI PETEROLI IKI ISHA LINAZIMA . MUACHENI BABU WA WATU APATE ULAJI WAKE . MABONA AMUWASEMI AO WATU WA MABASI WANAO LIPISHA PESA NYINGI MNAMSEMA BABU TU.
ReplyDeleteDuh watalaam wetu mlio nje mbona mliotoa maoni hapo juu mnatutisha sasa inatufanya tuogope vipimo vya hapa nyumbani maana mtu anaweza akapimwa akaambiwa hana kumbe vimejificha, Mungu utusaidie na bongo yetu
ReplyDeletehuyu nae eti atatuma nauli na visa unataka kumwambia nani kuwa uko nje ya nchi, kwa nini usije mwenyewe au umejilipua huwezi kutoka? siple njoo chukua mgonjwa mwenye ukimwi aliyekunywa dawa ya babu na uondoke nae ukafanye huo bloody utafiti wako, nyie ndoo waleee halafu unajiiona umeongea ya maana.
ReplyDeleteTatizo tukiambiwa ukweli hatutaki, Duh Bongo tambarareeeeee
ReplyDeleteMjinga ni yule anayepingana na mambo ya imani. Imani haichanganywi wala kupimika kwa science. Wala haiitaji kuwa scientifically proven.
ReplyDeleteMnaojifanya mnajua na wenye akili ndio wagonjwa.Hao wazungu wanaimani na wana miujiza/ushirikina pia. Science ni matunda ya Lucifer kupitia freemasons. Niko USA na nayaona hayo pia.
Itambueni dunia kabla hamjajifanya mnajua kumkosoa babu ama watanzania wanaokwenda huko ikiwa kila mtanzania anaangukia kwenye kuamini ama mungu ama mizimu.
Kaeni kimya
mh. Imani yako tu ndo itakuponya. Ukiwa huna iman hata mafua yatakuua. Mie naona wachangiaji wengi hum hawana imani na kwakuwa hili suala linamhusu Mungu zaidi naona bora kama mtu ukae kimya. Naona mnataka ku-dilute tu dawa ya babu hafu iache kuponya. Achen wenye matatizo wakatibiwe, msimuudhi Mungu.
ReplyDeleteYaani hapa cha msingi kama una imani nenda na kama huna imani usiende and then kaa kimya,waache wenye shida waweze kutafuta ufumbuzi wa maisha yao
ReplyDeletenina shangazwa sana na watu mnaokaa nje ya nchi, ambao mezoea kudhalau mlikotoka na kuona kila tunachofanya ni sababu ya ubongo wetu, wewe kama unalo la kufanya rudi nchini kwako ili uweze kuboresha usisbiri kukosoa tu.
ninachotaka kukuambia imani ni swala binafsi la mtu, hata wazungu sasa wana hirizi wanavaa, je hilo mnalijua?
kama hujui mambo nyamaza kimya, waache wenye imani na wanaohitaji msaada waende kwa sababu sisi kama wanasayansi hatujawasaidia chochoche, kama babu kafanya hivyo, nasisi kama wanasayansi tukae tusugue vichwa, na kama haviwezekani kama ilivyo sasa, TUNYAMAZE KIMYA NA TUACHE WATU WENGINE WANYANYE,
mnakumbuka enzi za Noah? yalikua haya haya sasa ndo watu waamini Biblia na Yesu aliposema yeye ni mwana wa Mungu watu wengi hawakumuamini... ndugu imani yako itakuponya kumbuka hilo
ReplyDeleteNaomba tu mchambue mawazo yenu vizuri hivi mnajua kuwa hiyo dawa anayotumia babu kunywesha watu wenyenji wana tengenezea mishale ya sumu kiasi cha kwamba wanaogopa majani ya mti huo kuwa ni sumu lakini walivyoona watu wanajaa nakunywa nao wakadai wapewe jibu alilowaambia kuwa aliwashawishi wanywe kama tiba wakammdharau sasa wanataka nao wapewe. akawaambia atawaambia siku yao kwa muda huu wamwache ashughulikie wenye maradhi yao wanaotoka mbali hiyo haitoshi pale hurusuwi kutoa hongo kwa kupata nafasi la utakuwa umekunywa maji,usiibe hataki kusikia ugomvi sasa vitu kama hivyo lazima tujue vinatokea mara chache sana cha msingi tuone jinsi gani afanye kazi yake kwa ufanisi pale anapogawa pana jua je mwavuli mkubwa si utafaa akipewa .na hao wanaosema afanya kuvuta watu ajili ya utajiri si kweli hiyo 500/- anatoa 150/- kanisani na 150/- msikitini inayobaki 200/- wafanyakazi wachache wanamsaidia kuchemhsa dawa hapo kweli anafanyia utajiri?nadhani imefika wakati tumsaidie apate urahisi wa kufanya kazi yake.
ReplyDeleteTUNA AMINI KUNA MIUJIZA..watu wote walioenda wakaacha shughuli zao sio wajinga,na tz vile vile kuna wanasayansi..but this is different,hii ni miujiza na sio science.'Yesu alimfufua lazaro aliekufa siku tatu' Je nyie wana sayansi leo mngetuambiaje?We kama huamini acha wanao amini waende. Isitoshe,we sio mgonjwa au labda huna mtu mgonjwa na unaempenda sana na hutaki kumpoteza,ungekua nae ungempeleka kwa babu au ,ila ukiupata ugonjwa utaenda loliondo. Hakuna mtu ana penda kuumwa. Acheni kabisaaaa kukashfu au kuingilia maswala ya imani,ita wacost badae esp now unaweka post za kukatisha watu tamaa badala ya kutoa matumaini. Je in few months ukajigungua una umwa gonjwa moja wapo???????cancer,sukari,pumu,aids au presha??utanga'anga'nia kukaa ulaya usiende kwa babu??be reasonable!
ReplyDeleteWenye Imani tunaami miujuza,na ukifuatilia Yesu alitoa miujiza mingi akiwa na wagonjwa hapo hapo sio wakiwa mbali.Hivyo nenda kwa babu physically.
We sambaza nyuzi kuna miujiza Tz whoever wants to come to Tz atakuja.
Ni mtazamo wangu tu.
kweli sisi watanzania tunataabu sana kuanzia kichwani nahii itatufanya tuwe maskini hadi kufa vizazi hadi vizazi, maana unasema jamboflani bado mtu anashindwa kukuelewa japo umetumia lugha rahisi ya kueleweka.
ReplyDeletemimi nimesema ninacho hitaji ni dawa ije itibu wagonjwa watatu kisha tufanye uchunguzi kuona effect yake,sikwambieni dawa haitibu au inatibu! kama ningekuwa na nafasi si ningekuja mwenyewe? na hao wanaodai haitoki loliondo basi inatia mashaka ya dawa hiyo, vinginevyo tuambiwe hii ni miujiza na sio uvumbuzi wa dawa, maana we believe in miracles too. kina naamani si waliponywa ukoma kwa kujiosha mtoni? kina lazaro si walifufuliwa toka kaburini? sasa ugomvi uko wapi, kama dawa inatibu basi imeletwa iponye watu,kama ni miujiza inatibu basi huyo x-pastor hana cha kufanya zaidi ya kuwa njia ya miujiza inayotendwa kupitia kwake na siyo kavumbua dawa kwa ajili ya kwenda kusaidia wengine duniani,inamaana asipokuwepo yeye na uponyaji umekwisha pia.
tuache majungumajungu na uongeaji bila kufikiri vizuri,sasa wanao kataa basi dawa hiyo isijifunzwe effect yake wanatarajia nini baadae? huu ni mfano mdogo tu wa kuonyesha kwamba bado tuko mbali sana ktk uelewa wa mambo,na kwa mtaji huu umaskini na magonjwa vitaendelea kuindama jamii ya hapo hadi mwisho,wakati wengine wanapo kufa na kwenda kusubiri hukumu wakiwa wameishi ktk hali ya kuridhisha ,hapo watakuwa wanakufa au kuzeeka verey tired with poverty,diseases,hunger etc na si ajabu na mbingu pia wasiione.
ok,ninaweza nikaleta wagonjwa huko,lakini mara nikitaka wapate hiyo dawa sikuhiyohiyo utasikia aaaah yaani wao ni bora kuliko walio wahi? hamtakuwa tayari kuona basi wanaipata mapema na kuondoka ili kurudi huku. acheni mambo ya kuwa mnaongea hovyohovyo tu bila kufikiri,unaweza kuwa kimya na ukaonekana unabusara kama hujui jambo,kuliko kusema ukasema pumba ili mradi unapinga tu.
nchi yetu umaskini umezidi ndo maana hata huduma zingine hazipo zinazopaswa kuwepo,kwa mtaji huu wa kuongea pumba wakati hakuna hata technology moja ya kutokea huko,na hata pesa ya kuinunua pia hakuna, mtaendelea kufa kwa taabu pasipo hata na matumaini ya kupunguza makali kabla ya kifo.
good lucky waongea pumba,stay with your troubles because you were born to suffer and you have neither dreams nor stratergic plans to get out of your ignorance and poverty. waiting for wazungu to think for you and bring misaada .najiskia kukata tamaa sana kuwa na jamii ya namna hii.wenzenu hawako hivyo ndiyo maana wanaendelea kila kukicha toka hatua moja hadi nyingine,maana wanafikiria vizuri.
samahani kwa kutoka nje ya mada, asante sana mleta mada hii,
ReplyDeleteNaomba kabla hujaiweka mada yako Jamvini, ipitie uisome, umekiharibu kabisa Kiswahili, mfano wa maneno machache:ivi,anyi,yani,ata
Pole sana lakini jifunze kuandika vizuri
Hello,
ReplyDeleteNaomba nimuulize huyo anayesema babu anatibu magonjwa ma 5 kwani Mungu anachagua magonjwa ya kuponya?
Na huyo wa USA naona yupo kimaabara zaidi wakati babu yupo kimungu zaidi.
Na huyo anayesema babu apimwe akili akanywe dawa kwanza coz nawasiwasi naye
Mama Samare Usa River
Mimi bado siamini hii kitu,naona usanii tuu...siko huko lakini kama mtu anaweza atafute wagonjwa 100 awaganye 20 kwa makundi matano ya hayo magonjwa yanayotibiwa awapime vizuri then awapeleke kwa babu wanywe dawa then awapime kila baada ya miezi mitatu kwa mwaka mmoja then tujue matokeo..labda nitaamini lakini kwa sasa HELL TO NO!
ReplyDeleteHEY HII NI KWA HUYO ANONYMOUS 09-34:00PM 2011 . WEWE NDIE UELEWI NAMEKWAMBIA NENDA KAMUCHUKUE HUYO BABU TOKA BONGO MULETE MAREKANI MPELEKE HUKO KWA WATU WANAO UMWA AJARIBU KUWATIBU NA WAKATI UO UO ANAWATIBU NENDA MKAPIME HIYO DAWA KAMA DAWA ITAKUA SAWA UTAKUWA TAJIRI SANA KWA SABABU WEWE NDIE UMEMULETA. NATHANI WATU KAMA WEWE INDIO TANZANIA IPO NYUMA KWA SABABU WATU MLIO NJE MNAWAZALAU WATU WA NYUMBANI MUNAJIFANYA WAZUNGU NA KUWADANGANYA WATU KWAMBA MNAKUNYWA KUKU KWA MRIJA. KUMBE BADO MA BUBUMBU.
ReplyDeletehaya magonjwa siyo kitu kizuri.kama kuna watu walikuwa positive wameenda kwa babu wakapewa dawa wakakutwa negative na wanafurahia hiyo safi sana.waacheni watu wafurahie msilete vikwazo tena.kwanini watanzania tunapenda kupiga domo sana????hatutakiani mema kabisa.wewe siyo mgonjwa tulia.wale wenye magonjwa waache waende wafurahie uzima nao.haijalishi kama dawa haisafirishwi au lazima upewe na babu tu na siyo mtu mwingine.what matters is kuna watu walikuwa wagonjwa na wamekula dawa wamepona.safi.waacheni wengine wenye magonjwa waende nao wakapate dawa wapone sote tuishi kwa furaha.Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
ReplyDeleteNuhu alipokuwa anawaambia wanadamu waache dhambi walimdharau wakaangamia kwa gharika,akapona yeye na familia yake. Sodoma na Gomora vivyo hivyo. YESU alipohubiri na kuponya walisema huyu si yule mtoto wa seremala? Hawakumwamini. Sishangai hii ya 'Babu' wa Loliondo wapo watakaoamini na wapo ambao hawataamini. Ila cha msingi hapa sio dawa ni ya aina gani nani anatibu ila ni IMANI yako tu. Kwa wale wanaotumia biblia wanajua waebrania 11:1 inaeleza bayana imani ni nini. Cha msingi hapa sio kukosoa na kuongea hovyo. Kama huamini kaa pembeni halikuhusu wapishe wanaoamini wapite. Wapo watu wameteseka na magonjwa muda mrefu na wanatamani kupona, kama wewe unajiona mzima mshukuru MUNGU.
ReplyDeleteTutumie hekima ktk kuchangia hii mada jamani.
kwakweli huyo jamaa anaejiona mmarekani kanibore sana na lugha zake chafu. Oh sijui nikija na wagonjwa wakitaka kutibiwa kabla ya wengine sijui itakuwaje blah blah blah. Shut up!! We beba mabox huko na usijifanye oh watanzania wamezaliwa kwenye poverty, wewe je? Ndugu zako? Come on?? Kama una kitu hata usingefatilia haya waonyesha hata shughuli ya kufanya huna. Eti no strategies no plans eti no technology. We ya kuwaosha hao wazee huko mbona hujaileta huku wazee watu nao wakazeeka vema. Huna unachojua na kukaa kwako huko ni u-coward wako tu. Pumba waongea wewe usimhusishe kila mtu. Tunapoongelea suala la babu tuko kiimani zaidi. Uwe unasoma akili za watu unaposoma comments na kutoa comments sio unatapika tapika na kutukana nyumbani kwenu.kuwa na adabu.
ReplyDeleteWewe ushangai?Bill gates anatumia bilions of dollars akijaribu kugundua dawa ya aids alafu wabongo mnapewa kwa mia5 mnaona feki.Ni bora ukanywe isifanye kazi kuliko usinywe ukasikia waliokunywa wamepona.Jambo la imani halithibitishwi kisayansi. Iam in Brandenburg,de... Love kiswahili.
ReplyDelete