Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu, amelitaka Shirika la Viwango Nchini TBS kuongeza juhudi katika kusimamia ubora wa bidhaa nchini ili kuwapa watumiaji thamani halisi ya fedha wanazotumia katika kununua bidhaa hizo.
Naibu Waziri Nyalandu ametoa rai hiyo katika ziara yake ya siku moja ya kulitembelea Shirika la Viwango nchini TBS ambalo lipo chini ya Wizara yake.
“TBS mnalinda maisha ya watu, mnalinda mali zao, fanyeni kazi zenu kwa umakini mkubwa, bila woga, serikali haitawaingilia na badala yake, itawasimamia na kuwawezesha ili mtimize vyema majukumu yenu” alisema Naibu Waziri
Akimkaribisha Naibu Waziri, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Bw Charles Ikerege amesema, TBS imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kusimamia ubora wa bidhaa nchini licha ya uwezo mdogo wa kifedha ilionao na kuiomba serikali kuongeza fungu la fedha ili kulipa shirika hilo uwezo zaidi.
Hii TBS inaitia nchi gharama "SANA".
ReplyDeleteTAKATAKA ZINAINGIZWA "LEFT N RIGHT" HALAFU MNASEMA TUNA WAKATA/WANALIPA "KODI".
"REALY"!!!?? "WANACHOFANYA "NIKUMWAGA TAKATAKA KWENYE NCHI YETU KWA BEI NAFUU/KWAGHARAMA ZETU, HII NI "LONG TERM PLAN" MADHARA YAKE TUNAYAONA NA YATAZIDI MIAKA HAMSINI/KARNE IJAYO.