Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu(Katikati), akifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Viwango nchini (TBS) Bw Charles Ikerege(Kushoto). Anaezungumza ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo Prof Apollikaria Pereka aliyekuwa akimkaribisha Mh Nyalandu kutembelea shirika hilo
Naibu Waziri Nyalandu akitembeleamaeneo mbali mbali katika ziara yake ya kutembelea Shirika la Viwango nchini TBS.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu katika Picha ya Pamoja na Viongozi na Maafisa wa Wizara yake na Shirika la Viwango nchini TBS mara baada ya kutimisha ziara ya kulitembelea shirika hilo.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu, amelitaka Shirika la Viwango Nchini TBS kuongeza juhudi katika kusimamia ubora wa bidhaa nchini ili kuwapa watumiaji thamani halisi ya fedha wanazotumia katika kununua bidhaa hizo.

Naibu Waziri Nyalandu ametoa rai hiyo katika ziara yake ya siku moja ya kulitembelea Shirika la Viwango nchini TBS ambalo lipo chini ya Wizara yake.

“TBS mnalinda maisha ya watu, mnalinda mali zao, fanyeni kazi zenu kwa umakini mkubwa, bila woga, serikali haitawaingilia na badala yake, itawasimamia na kuwawezesha ili mtimize vyema majukumu yenu” alisema Naibu Waziri

Akimkaribisha Naibu Waziri, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Bw Charles Ikerege amesema, TBS imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kusimamia ubora wa bidhaa nchini licha ya uwezo mdogo wa kifedha ilionao na kuiomba serikali kuongeza fungu la fedha ili kulipa shirika hilo uwezo zaidi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hii TBS inaitia nchi gharama "SANA".
    TAKATAKA ZINAINGIZWA "LEFT N RIGHT" HALAFU MNASEMA TUNA WAKATA/WANALIPA "KODI".
    "REALY"!!!?? "WANACHOFANYA "NIKUMWAGA TAKATAKA KWENYE NCHI YETU KWA BEI NAFUU/KWAGHARAMA ZETU, HII NI "LONG TERM PLAN" MADHARA YAKE TUNAYAONA NA YATAZIDI MIAKA HAMSINI/KARNE IJAYO.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...