Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli, pamoja na Mama Tunu Pinda, kwenye mpaka wa wilaya ya Chato na Muleba alipokuwa ziarani Kagera. Picha na Chris Mfinanga


Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati akikamilisha ziara yake mkoani Kagera, amelazimika kutoa ufafanuzi wa kauli yake, ili kujibu malalamiko ya baadhi ya wananachi na hasa wachambuzi wa masuala ya kisiasa ambao wamekuwa wakimlaumu kwa kumtumia ujumbe hadharani Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli akimtaka kusimamisha zoezi la bomoa-bomoa. Hatua hiyo ilitafsiriwa kuwa Serikali haina kauli moja.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda, amesema Serikali imelazimika kusitisha zoezi la bomoabomoa lililokuwa likiendelea nchini kwa sababu yapo mambo ambayo yanahitaji kuchukuliwa hatua na Serikali.

Alisema yanatakiwa kuwepo maelewano na kutoa elimu zaidi kwa wananchi kwa sababu Serikali ndiyo imewaacha watu wakajenga katika maeneo hayo huku wakijua wazi kabisa kuwa sheria ipo na walitakiwa kuwazuia wasindelee kujenga kwani sheria inayokuja leo ni kwa ajili ya vizazi vijavyo.

“Sheria inayotumika ni ya mwaka 1937, tunapaswa tuwaelimishe wananchi sheria inasema nini. Katika hali hii, tunapaswa tuangalie zoezi zima linavyoendeshwa sababu kuna watu wamejinyima wakajenga makazi yao ya kudumu, kuna watu wamewekeza miradi katika maeneo haya, hakuna aliyewazuia wasijenge japo sheria ilikuwepo...” alifafanua Waziri Mkuu.

Kufuatia malalamiko toka sehemu mbalimbali nchini, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amewaagiza Wakuu wa mkoa yote kupeleka taarifa ya barabara zinazojengwa kwenye maeneo yao ili kubaini ni nyumba ngapi zitakazoathirika na bomobomoa hiyo na athari zake katika maeneo husika.

“Nimemwomba kila mkuu wa mkoa alete orodha ya barabara ngapi zinajengwa sasa, ngapi zinatarajiwa kujengwa, nyumba ngapi zitaathiriwa na operesheni hizo; ngapi zilijengwa kabla ya sheria kupitishwa… nataka tupate taarifa inayoonyesha mchanganuo wa maeneo ya mijini na vijijini,” alisema.

“Lazima tuangalie makazi ya watu yalivyojengwa, tuangalie athari zake zikoje, athari haziwezi kuwa uniform katika maeneo ya mijini na vijijini… tutafute njia mbadala na kujiuliza, je hapa hatuwezi kupindisha barabara ili kuepuka balaa la kuwabomolea watu na serikali kuingia gharama za kulipa fidia.”

Pinda alisema katika maeneo mengi, awali sehemu ya hifadhi ya barabara ilikuwa ni mita 22 na baadaye ikaongezwa hadi mita 30 za eneo la barabara ambapo yapo pia majengo ya taasisi za umma na ya huduma za kijamii kama vile hospitali, benki, misikiti na makanisa ambayo huenda yalijengwa zaidi ya miaka 20 iliyopita baada ya kuomba ardhi na kupewa, na leo kuibuka na kuambia kuwa majengo hayo yako kwenye maeneo ya hifadhi ya barabara na kutakiwa wabomoe ni suala ambalo linahitaji umakini wa hali juu ikiwa ni pamoja na kutoa elimu na mashauriano,

“Hebu fikiria kama eneo la hifadhi ya barabara kuna majengo ya makanisa kama Lutheran, Roman Catholic, msikiti … halafu maaskofu wa makanisa hayo pamoja na sheikh wapangane kuja kwako kulalamikia suala hilo, wakati waliomba ardhi na kupewa na Serikali hiyo hiyo ambayo ina sheria hiyo inayozuia ujenzi katika eneo hilo, unafanyaje? ni taabu tupu ...ahh...ngoma hapo,”alisema Bw. Pinda, “Je tuzibomoe zote hizo kwa sababu sheria inasema hivyo?,” alihoji na kuongeza kuwa, “inabidi tufanye tathmini!”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Ee hii ni busara. I cant imagine nilivyojinyima kujenga nyumba yangu, hakuna aliyeni-stop nikinunua kiwanja na kujenga, leo unakuja kunibomolea. Tunashabikia yanapowatokea wengine, imagine linakutokea wewe (kwa wanaojua uchungu wa kujenga kwa kipato cha mtanzania wa kawaida)

    ReplyDelete
  2. Pinda hana busara. Hakuwa na sababu ya kum-blast waziri wake hadharani. nadhani kuna taratibu maalum ndani ya serikali ya jinsi ya kushughulikia tatizo kama hilo. Je rais angem-blast yeye Pinda hadharani angejisikiaje? Au anataka kumuonyesha nani kuwa hata yeye anaweza wakati mambo yalishamshinda sikunyingi?? ACHA HIZO PINDA!!! heshimu mawaziri wenzako. Huwezi jua kesho rais akawa Magufuli. Mhh!!! sipati picha.

    ReplyDelete
  3. call spade a spade acha sheria ichukue mkondo wake tukianza kuangalia hivyo hatutafika kokote!

    ReplyDelete
  4. Hapa Tanzania barabara ni tatizo kubwa sana. Serikali ilipe tu fidia, barabara zijengwe. Siasa zingine hazina msingi kabisa. Hapa Muhimu ni wale watakao athirika kulipwa fidia halisi na kupewa viwanja bora makazi yawe bora na barabara zitoshe. Kweli ukifikiria mijini kiasi cha muda unaopoteza mtu barabarani (hasa Dar es Salaam) kweli ufanisi wa kazi na muda wa kufanya hizo kazi unakuwa mdogo sana. Watu hawana hata muda wa kukaa na familia muda mwingi unapotea barabarani. Ukifika kazini au nyumbani umeshachoka wala hutaki mtu akusemeshe sasa nchi itajengwa na watu wanaofika kazini wakiwa wamesha choka? Wanafunzi watafaulu vipi kama kila siku anakosa kipindi cha kwanza na hana muda wa kufanya homework kwa kuwa kachelewa kufika nyumbani? Hatufiki popote kwa jinsi hio. Naimani hakuna mwananchi atakae lalamika kama alipewa kiwanja kimakosa na serikali imemfidia na anapata huduma nzuri ya barabara.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...