Jumuiya ya Watanzania wanaoishi katika Jimbo la Gauteng, Johannesburg, Afrika ya Kusini (TALGA), inatoa salamu za pole na rambi rambi kwa Watanzania wote walioathirika na hata kupoteza maisha kutokana na mlipuko wa mabomu katika Kitongoji cha Gongo la Mboto, jijini Dar es Salaam. Hakika ni vigumu kuelezea janga hilo zito na hasara iliyowakuta waathirika hao pamoja na Taifa kwa ujumla. Jumuiya iko nanyi katika wakati huu mgumu na iko tayari kusaidia kwa hali na mali.
Dr. Robert Ngude
Mwenyekiti wa muda.
Nataka kuwapongeza TALGA kwa kutoa salamu za pole na rambirambi kwa wakazi wa Gongo la Mboto. Ni faraja kubwa sana kukumbukwa na ndugu na jamaa mlio mbali nasi.
ReplyDeleteNaiombea TALGA maisha marefu na mafanikio mema.
Mdau
Faustine