Mzee wa Vunja Mifupa kama Meno iko Samba Mapangala akisalimia mashabiki alipoibuka ghafla katika onesho la kukata na shoka la mahasimu wa jadi katika muziki Msondo Ngoma band na Mlimani Park wana Sikinde usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee hall jijini Dar. Kaiambia Glou ya Jamii kwamba yuko nchini kwa siku kadhaa katika mpango wa kurekodi na baadhi ya wanamuziki wa hapa. Hakufafanua kwa undani akisema atatoa taarifa kamili baadaye. Mashabiki walimshangilia sana alipopanda jukwaani na kuwasalimia
Samba Mapangala akisalimiana na mkongwe Kassim Mapili. Shoto ni MC wa onesho hilo Sakina Lyoka wa Clouds TV
Samba Mapangala akiamkiana na mkongwe na kiongozi wa Msondo Muhidin Maalim Gurumo aliyekuwepo ukumbuni na mkewe. Gurumo ameshauriwa na madaktari kupumzika mara baada ya kutoka hospitali alikolazwa kwa siku kadhaa siku za nyuma. Aliwafurahisha mashabiki wa Baba wa Muziki alipopanda jukwaani na kumtambulisha 'mshambuliaji' mpya waliyemyakua toka Sikinde, Shaaban Dede.
Wanamuziki wa Sikinde wakifurahi na Samba Mapangala
alipokwenda kuwasabahi back stage

Mpiga gita wa Sikinde Mjusi Semboja akiongea na Samba Mapangala
Samba katika picha ya pamoja na Wana Sikinde

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...