Na. Aron Msigwa - MAELEZO,Songea.
Serikali imepiga marufuku shughuli zote za ukataji wa miti sanjari na utoaji wa vibali vya ukataji miti ndani ya hifadhi ya msitu Matogoro ulio katika manispaa ya Songea kufuatia ukataji holela wa miti na uharibifu mkubwa wa mazingira unaotishia kutoweka kwa chanzo cha mto Ruvuma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais mwenye dhamana ya kusimamia uhifadhi wa mazingira nchini Dkt.Terezya Huvisa Luoga ametoa agizo hilo mara baada ya kutembelea hifadhi hiyo na kushuhudia vitendo vya ukataji holela wa miti usiozingatia athari za mazingira na taratibu za uhifadhi endelevu unaohatarisha maisha ya wakazi wa manispaa ya Songea.
Amesema kuwa hivi sasa dunia inakabiriwa na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi na kuongezeka kwa hewa ya ukaa angani na joto inayosababishwa na uharibifu wa mazingira kwa kiasi kikubwa na kubainisha kuwa hali hiyo ya uharibifu wa mazingira ndani ya msitu matogoro haiwezi kuvumiliwa.
"Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zimesaini mikataba ya uhifadhi wa mazingira na imekuwa ikishiriki kwa kiwango kikubwa katika programu nyingi za kitaifa na kimataifa za uhifadhi wa mazingira, hivyo hali inayotokea sasa ndani ya msitu huu ni hatari na mimi kama waziri mwenye dhamana ya mazingira siwezi kukubaliana na hali hii" amesisitiza.
Amebainisha kuwa hakuna nchi yoyote duniani inayoweza kuvumilia uharibifu huo wa mazingira kwa kisingizio cha uvunaji wa misitu huku akiwatupia lawama maofisa misitu wa manispaa ya Songea na viongozi wa msitu huo kwa kutokuwa makini katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kisingizio cha ukusanyaji wa mapato.
"Jamani ifikie wakati muwe na uchungu na rasilimali za taifa letu na kuwa wakweli kuzieleza wizara husika maendeleo na hali halisi ya msitu huu ili uvunaji uwe endelevu sambamba na upandaji wa miti na sio hali hii iliyopo ambayo inasikitisha"
Hata hivyo akiwa bado ndani ya hifadhi hiyo Dkt. Terezya alikutana na kundi la wafanyakazi waliokuwa wakiendelea na shughuli za kukata mbao za mfanyabiashara mmoja (jina halikuweza kupatikana)ambaye walidai alikuwa na kibali kutoka mamlaka husika na kumfanya aruhusiwe uongozi wa msitu huo kuvuna ambapo wafanyakazi hao walipoulizwa walibainisha wazi kuwa wao hukata miti zaidi ya 152 kwa siku.
Kufuatia hali hiyo ameuagiza uongozi wa hifadhi kuhakikisha kuwa unavifuatilia kwa makini vibali vyote vya uvunaji vilivyotolewa mwaka huu na kuvizuia ili kupisha shughuli za upandaji wa miti katika maeneo yote ambayo ardhi iko tupu na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa kurudisha miti iliyokuwepo.
Awali akitoa taarifa kwa waziri kuhusu uvunaji ndani msitu huo kaimu meneja wa msitu huo Bw. Hamis Ally amesema kuwa juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanyika katika kuhifadhi na kusafisha msitu huo kwa lengo la kuandaa maeneo yaliyovunwa kwa ajili ya kupanda miti mipya huku akibainisha kuwa kila mwaka vibali hutolewa kwa uvunaji wa hekari 40.
Hata hivyo maelezo yake yalipingwa vikali na na waziri pamoja na viongozi wengine waliokuwa kwenye ziara hiyo akiwemo Meya wa manispaa ya Songea Bw. Ally Manya na diwani wa kata ya Matogoro ambayo msitu unapopatikana kwa madai ya kutokutolewa kwa takwimu sahihi za uvunaji na hatua za makusudi zilizochukuliwa kabla ya uvunaji ili kuunusuru msitu huo ikiwemo uoteshaji wa vitalu vipya vya miti itakayopandwa katika eneo hilo.
Kwa upande wake Meya wa manispaa ya Songea Bw.Ally Manya alikiri na kubainisha kuwa sheria za uhifadhi wa mazingira zipo wazi chini ya manispaa na tayari ameshaagiza maeneo yote yaliyokuwa chini ya mamlaka nyingine yarudishwe chini ya manispaa huku akiahidi kufuatilia kwa karibu uendelezaji wa msitu huo ambao kwa kiasi kikubwa umeharibiwa vibaya na ukataji holela wa miti.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...