Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa Luoga(kulia) akihoji jambo kuhusiana na uharibifu wa hifadhi ya msitu Matogoro - Songea unaosababishwa na ukataji holela wa miti na kuwa tishio la kukauka kwa chanzo kikuu cha mto Ruvuma ndani ya hifadhi hiyo na kuamua kupiga marufuku ukataji wa miti. Kutoka kushoto ni mkurugenzi wa manispaa ya Songea Bw. Nachoa Zacharia,Diwani wa kata ya Matogoro Bw.Charles Muhagama,Meya wa Manispaa ya Songea Bw. Ally Manya (wa tatu kutoka kushoto),Meneja msaidizi wa msitu wa Matogoro Bw. Hamis Ally na Afisa Misitu wa Manispaa ya Songea Bw. Robert Mgowole.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa Luoga akizungumza na baadhi ya wafanyakazi (vibarua) waliokutwa wakiendelea na zoezi la ukataji wa miti ndani ya eneo la hifadhi ya msitu Matogoro na kumweleza waziri kuwa kwa siku hukata wastani wa miti 152 na kuendelea.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa Luoga akikagua eneo la hifadhi ya msitu Matogoro lililoathiriwa na ukataji holela wa miti akiwa ameambatana na viongozi wa Manispaa ya Songea na kutoa agizo la kusitishwa kwa shughuli zote za ukataji wa miti ndani ya hifadhi hiyo.
Juu na chini ni eneo la hifadhi ya msitu Matogoro, Songea likiwa limeachwa wazi bila kupandwa miti kutokana na ukataji holela usiozingatia kanuni za uhifadhi wa mazingira hali inayotishia kutoweka kwa chanzo cha mto Ruvuma.Picha na Aron Msigwa - MAELEZO. |



Viongozi wetu bwana utafikiri wanaishi sayari nyingine, matamko yao kama vile wanaota! Maofisa wao ndio wanaongoza katika uharibifu wa hiyo misitu kwa kutoa vibali bila kuzingatia taratibu pia kutotoa njia ya mbadala za kuyakabili matatizo haya.
ReplyDeleteMimi nauliza Dr Kilahama aliposema hakuna tatizo katika msitu wa matogoro alikua ana maana gani. JK angalia hawa ndio wanaoua chama chako na kusababisha wananchi waione serikali yote ni ya wachakachuaji. Inauma sana, lakini poa ndio bongo.
ReplyDelete