Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Anne Makinda akitoa mada kuhusu Ushirikishwaji wa Jinsia katika Vyama vya Siasa katika Mkutano wa kuhamasisha ushirikishwaji wa wanawake katika vyombo wa kutoa maamuzi unaoendelea mjini Gbarnga, Liberia
Spika Makinda akitambulishwa kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Liberia, Mhe. James Fromoyan (kulia)na hatimaye kufanya mazungumzo ya pamoja
Spika wa Bunge la Tanzania Mh. Anne Makinda (wa pili kutoka kulia) akiwasili katika ukumbi wa Mkutano wa kuhamasisha ushirikishwaji wa wanawake katika vyombo wa kutoa maamuzi unaoendelea mjini Gbarnga, Liberia kwa mwaliko wa Taasisi ya Kimataifa inayosaidia uimarishaji wa Demokrasia na Chaguzi huru(International Institute for Democracy and Electoral Assistance-IDEA). Kulia kwake ni mwenyeji wake na ni Mwenyekiti wa Taifa wa Wabunge Wanawake nchini Liberia Seneta Carice A. Jah akimtambulisha Spika kwa viongozi wa wa chama cha wanawake wabunge wa Liberi
Spika Makinda akiwa kwenye picha ya pamoja na wanawake wa Liberia.

Picha na Prosper Minja-Bunge

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongereni akina mama asilimia kubwa hapo kwenye picha mumevaa vizuri sana - very African.

    Yaani mumependeza ile mbaya na vitenge vyenu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...