Mkuu wa Masoko wa Benki ya Stanbic Tanzania, Abdallah Singano (kushoto) akikabidhi msaada wa mafuta ya kupikia, vyakula, nguo na misaada mingine ya kibinadamu kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Leonidas Gama kwa ajili ya waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam jana.Wa pili kulia ni Meya wa Ilala, Jerry Slaa na ofisa wa benki hiyo, Kay Mbwambo.
Mkuu wa Masoko wa Benki ya Stanbic Tanzania, Abdallah Singano (kushoto) akikabidhi msaada wa mfuko wa unga wa sembe kwa Meya wa Ilala, Jerry Slaa pamoja na mafuta ya kupikia,vyakula, nguo na misaada mingine ya kibinadamu kwa ajili ya waathirika wa mabomu ya
Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Leonidas Gama,kushoto ni maofisa wa Stanbic, Eva Kombe na Kay Mbwambo kulia.
Mkuu wa Masoko wa Benki ya Stanbic Tanzania, Abdallah Singano (kulia) akizungumza na mmoja wa watoto ambao wazazi wake waliathirika na mabomu ya Gongo la Mboto walipowatembelea na kuwafariji waathirika hao na pia kuwapa misaada mbalimbali ya chakula na mahitaji mengine katika eneo hilo, Dar es Salaam jana.
Mkuu wa Masoko wa Benki ya Stanbic Tanzania, Abdallah Singano (kulia) akiwaongoza baadhi ya wafanyakazi wa benkim hiyo walipokwenda kuwafariji wahanga wa mabomu ya Gongo la Mboto na kuona uharibifu wa makazi ukiosababishwa na mabomnu hayo ambako pia walikabidhi misaada mbalimbali ya chakula na vitu vingine.
Baadha ya wafanyakazi wa benki ya Stanbic Tanzania walipowatembelea na kuwafariji waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto na pia kuwapa misaada mbalimbali ya chakula na mahitaji mengine.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Guys you are toooo slow to react, yaani leo hii ndio mnapeleka chakula?? Kwa mawazo yenu hicho chakula atapelekewa nani na kila mtu karudi kwenye makazi yake? Cha maana kufanya ilikuwa kuwasaidia waathirika kurudi hali yao ya kawaida kimaisha sio kuwapa msosi.

    ReplyDelete
  2. wahanga?! teh teh teh

    ReplyDelete
  3. PIA KULIKUWA NA HAJA YA KUPELEKA WATAALAM WA KUCHORA MICHORO MIPYA NA MJI HUO WA GONGO LA MBOTO KUJENGWA KISASA ILI KUTENGENEZA PIA NJIA ZA KUPITA WAKATI WA DHARURA NA KUWA NA STREET NZURI SASA UNAWEZA KUSHANGAA WAKARUDISHIA UCHAFU ULE ULE JAMANI WABONGO SIJUI AKILI ZETU ZITAFUNGUKA LINI, HAO STANBIC NI UBISHOOO TU JAMANI UMEWAJAA KWELI LEO UNAPELEKA CHAKULA BADALA MISAADA YA MIUNDO MBINU AU NDIO PROMOOO YENYEWE MANAKE NAONA CHATA HAPO KAKA MICHUZI HAPO UMEMTANGAZA MTU KUFA KUFAANA LAKINI NDIO USEMI WA KIBONGO
    MJAU JERRY
    HOLAND

    ReplyDelete
  4. Kutoa msaada mbele ya kamera, sioni kama ina tija. Wastaarabu wanaenda aninonimazi!!

    ReplyDelete
  5. The Good Dr. Mwakyembe amewanyoosha...mlikuwa mnaandika WAHANGA WA GONGO LA MBOTO. Dr. amewanyoosha juzi sasa sawasawa mnaandika WAATHIRIKA wa mabomu!! Long live Dr.!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...