akikabidhi misaada hiyo kwa niaba ya uongozi na wafanyakazi wa mamlaka ya viwanja vya ndege,meneja mariasili watu alisema " tumeguswa sana na maafa hayo yaliyowatokea wananchi wa gongo la mboto ukizingatia ni majirani zetu, kama taasisi tunawajibu wa kuwasaidia kwa hali na mali waaathirika wa mlipuko huo wa mabomu".
kutokana na kuwa jirani na eneo la mlipuko mamlaka ya viwanja vya ndege iliathirika kwa kiasi flani na mlipuko huo ikiwemo ku cancel safari za ndege kwa muda ili kuhakikisha usalama wa kiwanja.
kaimu Mkuu wa mkoa akipokea misaada hiyo, aliushukuru uongozi huo kwa misaada na kuweza kuwakumbuka hata kinamama maana wao ni katika kundi lililoathirika zaidi na mlipuko huo kutokana na kuunguliwa na kila kitu zikiwemo nguo.
Wahanga?! teh teh teh, Michuzi si ulikuwepo kwenye semina iliyoendeshwa na Dk. Harrison Mwakyembe?! Kazi kweli kweli!
ReplyDeletewahanga wanapaje misaada kama walijilipua?? huwezi toa msaada kwa mtu ambaye hayupo. Hawa ni WAATHIRIKA wa mabomu ya Gongo la Mboto.
ReplyDelete