Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini unawatangazia Watanzania waishio katika Jimbo la Gauteng kuwa kutakuwa na mkutano utakaofanyika tarehe 2 Mei, 2011 katika ukumbi wa Manicipali ( Municipal) iliyoko Kempton Park, Makutano ya Barabara za Pretoria na S.R Swart Johannesburg, Afrika ya Kusini kuanzia saa nane mchana(1400hrs) hadi saa 12 za jioni (1800hrs). Dondoo za mkutano zitakuwa kama zifuatavyo:

Kuzungumzia hali ya maendeleo ya Jumuiya ya Watanzania katika Jimbo la Gauteng
Kutakuwa na uchaguzi wa nafasi mbali mbali za uongozi
Kuandaa mikakati ya namna ya kusaidiana ndani ya chama hicho

Katika mkutano huo Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini Mheshimiwa Radhia Mtengeti Msuya atakuwa mgeni rasmi. Aidha, Jumuiya ya Watanzania Gauteng inawajulisha kuwa kwa wale ambao hawajalipa michango ya uwanachama yaani Ada R300 kwa mwaka na kiingilio cha uwanachama R200 wanatakiwa kulipa kupitia accounti ya Jumuiya Ned Bank 1916139183/Branchi ni Kilarney code numba 19160535. Lakini pia siku hiyo tutapokea michango hiyo pale pale wale ambao watakuja na michango hiyo.

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na wafuatao:

J.R Fhika jfhika@hotmail.com Simu +27762949049 begin_of_the_skype_highlighting +27762949049 end_of_the_skype_highlighting begin_of_the_skype_highlighting +27762949049 end_of_the_skype_highlighting
D.K Robert Ngude Robert.ngude@gauteng.gov.za +27823566963 begin_of_the_skype_highlighting +27823566963 end_of_the_skype_highlighting begin_of_the_skype_highlighting +27823566963 end_of_the_skype_highlighting
Mrs Josephine Mshilla jmshilla@hotmail.com +27721999833 begin_of_the_skype_highlighting +27721999833 end_of_the_skype_highlighting begin_of_the_skype_highlighting +27721999833 end_of_the_skype_highlighting
Lumbi & Ethel Simu ya mezani ya Ubalozini 012 342 4371/2

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Jumla R 500.Halafu ikitokea misiba tuchangishane wenyewe kwa wenyewe pesa za mifukono mwetu hata ukiwa mwanachama hiyo JUMUIYA inachangia R 100 tu tena hapo ndiyo wamejitahidi.Mimi mwanachama mbona alipokufa dada yangu gharama za usafirishaji tumemaliza wenyewe na hiyo JUMUIYA ya uzushi haikusaidia chochote yaani hata MBUNI.Maana ya JUMUIYA ni nini???Wizi mtupu.
    Kingine tumechoka mambo ya kubadilisha viongozi kila wakati na katika huo MKUTANO uchwara siji NG'OO.

    ReplyDelete
  2. Hongereni sana! Nawatakieni mkutano mwema. Napata faraja kuona chama kinaendelea kuwa imara.
    Faustine Ndugulile

    ReplyDelete
  3. Naomba uliza je kuna jumuiya ya watanzania western cape? na mawasiliano je?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...