Dkt. Hadji Mponda akiongea na wanafunzi wa chuo cha uuguzi na ukunga cha Mkomaindo,wanafunzi hao walisema kero yao kubwa inayowakabiri chuoni hapo ni ukosefu wa mabweni,kompyuta.maji pamoja na walimu,aidha Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii aliwaahidi kushughulikia matatizo hayo.Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya hiyo,Mh. Nape Nnauye
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda akisikiliza malalamiko ya wagonjwa waliofika kupata matibabu katika hospitali ya Wilaya ya Mkomaindo iliyopo Masasi,nje ya chumba cha x-ray,wagonjwa hao licha ya kutoa kilio chao juu ya matibabu pia walishauri Serikali iongeze idadi ya watumishi katika hospitali hiyo.Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda akiagana na wanachuo hao mara baada ya kutembelea chuo hicho chenye zaidi wa wanafunzi 100 ambapo aliwatoa wasiwasi wa kupata ajira kwani ajira yao inatolewa moja kwa moja kwa wahitimu wa kada za afya nchini.

Wanafunzi wa Chuo hicho wakishangilia baada ya Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii kuingia chuoni hapo kujionea mazingira ya chuo hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hivi ndio visura,sio wale walioshindanishwa juzi...Nape hoyeee!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...