TIMU ya mpira wa miguu ya wabunge kutoka nchini Kenya imewasili nchini kwa ajili ya kumenyana na timu ya klabu ya Wazee ya mjini Arusha, mchezo wa kukata na shoka utakaopigwa leo katika uwanja wa mpira wa General Tyre uliopo Njiro nje kidogo ya mji ya Arusha.

Ziara ya wabunge hao iliyoandaliwa na kuratibiwa na klabu ya wazee ya mjini hapa,ni mojawapo ya shughuli za klabu hiyo katika kudumisha ushirikiano na mshikamano baina ya nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki kupitia michezo.

Taarifa hiyo pia ilitaja mojawapo ya shughuli ambazo zitatekelezwa na wabunge hao ni pamoja na kutembelea ujenzi wa jengo la makao makuu ya jumuiya ya Afrika mashariki unaonedelea mkoani hapa.

Baada ya mchezo wa leo wabunge hao watapata fursa ya kupata chakula cha usiku na kubadilishana mawazo na wazee wa Arusha katika viwanja vya General tyre jijini hapa.

Klabu ya wazee ya mkoani Arusha ni mojawapo ya klabu ina jumla ya wanachama 150 kutoka nchi mbalimbali duniani ambao hufanya kazi mkoani hapa katika nyanja za kitaifa na kimataifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. hii imetulia. Hawa wazee wa Arusha naona wako serious. Naona wakati wazee wa miji mingine wakiwa bize na politicos hawa wanadumisha ushirikiano wa Afrika mashariki...safi sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...