Hi Ankal,
Habari za kazi na pole na kazi za kila siku za kutujulisha yanayojiri bongo yetu tukufu!
Naomba unipeperushie kilio changu as follows;
Mimi ni mdau Gianita, mwezi wa kwanza nilituma mzigo (box) hapo Dar kwa express kutoka New York, ukafika baada ya siku 5, kama tracking namba zilivoonyesha, tarehe 26 january . Kaka yangu akaanza kwenda posta lakini hakuti kile kikaratasi cha kuchukulia, akauliza akaambiwa mzigo haujafika, akaendelea kwenda kwa sababu nilikua nimemuhakikishia na kumpa tracking namba kuwa kweli mzigo umefika!
Sasa naomba unisaidie inakuwaje mpaka sasa ni miezi miwili na posta wanasema mzigo wangu haujafika, haujaonyesha kwenye system yao wakati nimewapelekea mpaka print out inayoonyesha maelezo ya mzigo huo kama inavyoonyesha uki track??????
Kitendo hicho kimeniumiza sana sana!!!
Naomba kujua nini nifanye ili nipate mzigo wangu kwani tumekua tunaenda posta kila wiki sasa na hamna kitu!!!
Nitapata wapi contact za wahusika wa Posta ili nipeleke shauri langu??!!! Nimejaribu web site yao lkn sipati jibu email nlizotuma!!!
Very Frustrated
Mdau Gianita Mwakapila.
USA.
Nimekwenda Posta ya New York na kama tracking inavosema mzigo umefika dar jan.26!!!
Kama kuna mwenye jinsi ya kunisaidia naomba awasiliane nami kwa email hii.
Mwakapilag@hotmail.com
Asante.
Habari za kazi na pole na kazi za kila siku za kutujulisha yanayojiri bongo yetu tukufu!
Naomba unipeperushie kilio changu as follows;
Mimi ni mdau Gianita, mwezi wa kwanza nilituma mzigo (box) hapo Dar kwa express kutoka New York, ukafika baada ya siku 5, kama tracking namba zilivoonyesha, tarehe 26 january . Kaka yangu akaanza kwenda posta lakini hakuti kile kikaratasi cha kuchukulia, akauliza akaambiwa mzigo haujafika, akaendelea kwenda kwa sababu nilikua nimemuhakikishia na kumpa tracking namba kuwa kweli mzigo umefika!
Sasa naomba unisaidie inakuwaje mpaka sasa ni miezi miwili na posta wanasema mzigo wangu haujafika, haujaonyesha kwenye system yao wakati nimewapelekea mpaka print out inayoonyesha maelezo ya mzigo huo kama inavyoonyesha uki track??????
Kitendo hicho kimeniumiza sana sana!!!
Naomba kujua nini nifanye ili nipate mzigo wangu kwani tumekua tunaenda posta kila wiki sasa na hamna kitu!!!
Nitapata wapi contact za wahusika wa Posta ili nipeleke shauri langu??!!! Nimejaribu web site yao lkn sipati jibu email nlizotuma!!!
Very Frustrated
Mdau Gianita Mwakapila.
USA.
Nimekwenda Posta ya New York na kama tracking inavosema mzigo umefika dar jan.26!!!
Kama kuna mwenye jinsi ya kunisaidia naomba awasiliane nami kwa email hii.
Mwakapilag@hotmail.com
Asante.
Nyie watanzania mlioko Marekani mbona wagumu kuelewa?
ReplyDeletePosta mnayoiona huko Marekani sio sawa na Posta ya huku Tanzania.
Sisi tulioko Tanzania tukiagiza vitu kutoka Marekani huwa tunatumia couriers - kama vile UPS, FedEx na DHL. Unaletewa mzigo mpaka home, au ukiwa na haraka mzigo ukishafika airport wanakupigia unaufuata ofisini kwao mitaa ya Posta Mpya.
Usiwe kama Mashaka ambaye tiba asili ya Tanzania anaiponda lakini akiuziwa "food supplements" na Wamarekani ananunua!
duh! pole sana , umeliwa m2 wangu.mzigo wako umefika na wajanja wameuchakachua,bongo hii.
ReplyDeleteMDAU POLE KWA MAUMIVU, MIMI YALIPATA HAYO MWAKA JANA, NILITUMA MOBILE PHONE KWA MDINGI, MATUMAINI YANGU KUWA BAADA YA SIKU 14 MZIGO UNGEKUWA UMEFIKA BONGO, NA KWELI ULIKUWA UMEFIKA BONGO, KWANI BAADA YA NENDA RUDI NENDA RUDI POSTA DAR KWA MUDA WA MIEZI MIWILI POSTA BONGO WANASEMA MZIGO HAUJAFIKA, ROYAL MAIL UK, WALINIAKIKISHIA MZIGO UMEFIKA NA TRACKING NUMBER IKAWA INAONYESHA HIVYO. MDINGI AKAWAJIBIKA KUOMBA KUONANA NA MANAGER WA POSTA HAPO BONGO- POSTA MPYA DAR, YULE MANAGER ALISHANGAA KUONA USHAHIDI WA MZIGO KUFIKA NA NDIPO AKAANZA UCHUNGUZI RASMI, HUWEZI KUAMINI BAADA YA SIKU 3,WAKAMWITA MDINGI KUCHUKUA SIMU YAKE, BOXI LIKIWA NIMEFUNGULIWA NA BAADHI YA ACCESSORIES HATUKUWEZA KUZIPATA NA SIMU ILISHAANZA KUTUMIWA, KWANI HAUKUWA NA DALILI ZOZOTE ZA UPYA. POLE SANAAA NA KAZA MSURI, LABDA LABDA UNAWEZA KUUPATA MZIGO WAKO.
ReplyDeleteMwambie huyo ndugu yako akaonane na Meneja wa hiyo branch hapo Posta au huyo meneja wa branch akileta gozi gozi amuone MD kabisa, si unajua watu wote wagonjwa? Pengine mzigo umefika na wafanyakazi bado wako kwenye foleni ya babu au kale kaugonjwa ketu kale kwa kuiba au kudokoa vitu vya watu.
ReplyDeleteMimi nawaatarifu kabisa kuwa karibu nitarudi home, nitaweka vitu vyangu kwenye kontena kisha vyote navipiga picha na video kabisa, halafu mulete hako katabia kenu ka udokozi maana huko kwenye hilo contena nitaweka kasekuriti kamera kaduchu na tunasa sauti!
Kama alivyosema Anonymous wa kwanza hapo juu, Jamaa zetu mlioko Marekani na hata ulaya fanyeni utafiti kidogo, posta za ulaya na marekani sio Tanzania.......mbona kuna huduma nyingine nyingi za kuleta vifurushi na hata mizigo kwa usalama!.........Na kwa anayetuma mobile toka ulaya huyo nadhani amesahau hali halisi ya nyumbani......Kwa ninin utume simu ya mobile toka ulaya? Mbona ziko nyingi sana nyumbani?fanye utafiti jamani......tuma pesa......kama watanunua mobile sawa.....kama watazila si mbaya......wewe umetenda jema.......!
ReplyDeleteNdiyo maana unatakiwa ukatie bima vifurushi unavyotuma bongo.....ungekuwa na bima yako hapo wala usingeangaika, wangekulipa fidia and then wangedili na bongo.....
ReplyDeletePosta Dar wezi. Mi sikujua mwanzoni kama 'wanaiba' mizigo.. nikawa natuma tu(Kutokea Uingereza). Haifiki., na mi nilivyo bwege, natuma tena. Kuja kushtuka nishapoteza pesa kibao. Sasa imebidi kuanza kutumia DHL. Vitabu nilituma mara tatu., vinachukua miezi 3 hadi 4 kufika. Hatari sana, ukiwa na hasira unaweza kutoa mtu utumbo
ReplyDeletePole sana umeshaibiwa tayari. Kama ulivyoshauriwa tumia DHL ni wazuri kabisa. Epuka pia EMS nao hawatabiriki japo zamani walikuwa wazuri.
ReplyDeleteLakini pia ninyi mnaotuma vitu kutoka majuu, fanyeni utafiti kwanza hapa nyumbani siku hizi kila kitu kipo ni pesa yako tu. Mvionavyo huko vingi ni mchina huyu huyu alievileta na bongo pia.
Ni vizuri mkatuma pesa zaidi kuliko vitu. Pesa inakuza uchumi wa nchi zaidi kuliko vitu.
Kweli kabisa posta zetu za kibongo hazifai kabisa. We ukilazimika kutuma kitu bongo bora uingie gharam kidogo lakini utume kwa courier services, achana kabisa na huduma za posta zetu!
ReplyDeleteKweli aisee, mwambie mzee wako amuone manager anaweza akasaidiwa.
Pambaf nyie mtamtoa nani utumbo? tumeni sie tunafungua na tukikuta mzogo 'unajipendekeza' tunaaza nao! kwani nyie wa kwanza? ebo!mshahara wenyewe twapewa kwa AWAMU sie watu wazima bwana na kukaba hatuwezi jamani!
ReplyDeletePOLE SANA MDAU NI VIZURI MKIWA MNATUMA MIZIGO MNATUMA NA RECOMENTATION HAPO KUIBA INAKUWA NGUMU MIMI HUWA NATUMA TU MIZIGO TOKA SWEDEN KWENDA BONGO ILA NAILIPIA INCASE IKIIBIWA POSTA YA SWEDEN INAFATILIA MIZIGO YANGU NA HUWA MZIGO UNAPIGWA MUHURI MWEKUNDU HAO WENYE NJAA BONGO WAKIONA HUO MUHURI WANAJUA HAPO KUIBA HAIWEZEKANI WANAUACHA FANYENI HIVYO GHARAMA ZA RECOMEMTATION SIO GHARI
ReplyDeletekaka pole sana, Posta wezi sana maana hata mimi walinifanyie kitendo hicho miezi saba iliyopita. tumia Fedex na kampuni nyingine lakini sio hao majambazi
ReplyDeleteHi wote, mimi ni dada Gianita nawashukuru kwa maoni na kwa mlioniandikia email mmenipa suluhishi nzuri ambazo nazifuatilia kuanzia dakika hii!! I apreaciate you all. Kweli Watanzania ni watu wazuri nimepata ushauri mzuri sana kwa email. Goad bless you all.
ReplyDeleteMs Mwakapila.
Nyie mnaosema vitu viko bong very contradicting urself. Watu wa bongo ndio wanaagiza hatuamki na kutuma tu ila ukiamka asubuhi kuna messages kibao wanataka hiki na kile? Ukiwaambia nitume hela ununue huko hela wanayotaka huko ni mara tano ya hicho kitu hapa. Ndio vitu viko huko lakini price yake ni ya kuumizana...Ni heri kununua kitu hapa na kutuma DHl unasave mara 5 ya kutuma hela na mtu anunue bongo.
ReplyDeleteNa hakuna kitu kibaya kama kupoteza mzigo ambao ulikua wa kumsaidia mtoto ambaye yuko shule..Kwanza sasa nyingine wanachukua mpaka picha. Hivi picha za mtu humjui unazipeleka wapi? Some people? Na POst Ipo chini ya wizara gani? Hawaoni aibu?
Hiyo ndio BONGO inatisha halafu nakupa ushauri ukienda kuchukua mzigo uwe makini kuna kaujanja mwingine waliotangulia hawajauona watu wa POSTA WAHUSIKA wanachofanya wanafungua mzigo mbele yako na kukadilia kiasi gani unatakiwa kuulipia kamzigo kamoja watakuambia laki nane kiasi ambacho hauna pale kutokana mawazo yako mzigo wako unaweza kukughalimu shs elfu hamsini au elfu sitini sasa utachanganyikiwa watakuambia kaongeze kidogo ukiwapa MGUNGO TUU UMEUMIA watachomoa wanachotaka na kuufunga kama mwanzo, ukija unawapa wanachotaka huna muda tena wakuchungulia ndani, ukifika nyumbani utakuta vitu vingi wamechukua bila huruma ni AIBU. sasa kila anayetumiwa MZIGO aende kwa MENEJA.Itabidi huyo MENEJA afunge ofisi ashughulikie wanaoletewa mizigo.Cha muhimu FUKUZA meneja Mkuu na wote walikuwa zamu siku hiyo,vijana wapo kibao wanatafuta KAZI.
ReplyDeleteMMmmmh huyo manager wa bank kajifugia vijambazi vyake hapo posta Dar. Mie nadhani unaweza kwenda hata polisi ingawa nao lazima wakuchakachue ndo wawe sirious kuwawajibisha hao posta ...........vinginevyo hawatakoma
ReplyDelete