Picha na Habari na Francis Godwin
Wagonjwa Iringa ,Mbeya na Vuruma leo wamiminika nyumbani kwa Dkt Antony Mwandulami (58) mkazi wa kijiji cha Itunduma Wangama wilaya ya Njombe mkoa wa Iringa kupata dozi ya bure ya vikombe vitatu vya dawa kama ya babu wa Loliondo .
Huku wagonjwa waliokunywa na kupona washuhudia kuwa kikombe hicho sio kama cha Mbeya ni kama Loliondo .
Wakitoa ushuhuda wa kikombe hicho akiwemo Nery Kasoli (50) mkazi Mbeya mjini ambaye alikuwa na binti yake Hilda Asenga (30)aliyekuwa asumbuliwa na kichaa na kutoa ongea kwa muda mwingi ambaye sasa amepona .
Alisema kuwa binti yake huyo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa huo kwa muda wa miaka takribani 10 ila baada ya kupata kikombe mtoto wake huyo amepona na anazungumza vizuri kabisa.
Huku Issa Omary (45) yeye alidai kuwa alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na kutibiwa katika hospitali mbali mbali za seikai bila mafanikio ila baada ya kunywa kikombe hicho hali yake ni nzuri na juzi amekwenda kupima Hospitali ya Ikonda ameonekana ni salama.
Wengine waliotoa ushuhuda wao jana ni pamoja na kijana mmoja ambaye alijitambulisha kwa jina moja la Kevin ambaye anadai kuwa alikuwa akisumbuliwa na IHV ila sasa amepima na kuonekana ni salama.
Akizungumza na waandishi wa habari waliofika nyumbani kwake kushuhudia zoezi hilo la utoaji wa dozi ya vikombe vitatu ,Mwandulami alisema kuwa lengo la kuanza kutoa bure dawa hiyo ni kutaka wagonjwa kutoa ushuhuda zaidi wao baada ya kunywa dawa hiyo badala ya vyombo vya habari na watoa huduma hiyo kuendelea kujitangaza zaidi na kujisifia kwa jambo ambalo si geni.
Mwandulami ambaye ni mshauri mkuu wa waganga wa tiba asilia Tanzania ameanza kutoa kikombe hicho ijumaa ya wiki iliyopita na kudai kuwa mti huo hajaotoshwa na Mungu wala mizimu bali alionyesha na marehemu baba yake zaidi ya miaka 18 sasa amekuwa akiutumia miti huo aina ya Makhirikhiri kwa kuchanganya na miti mingine.
Hata hivyo Mwandulami yeye amekuwa akitoa dozi hiyo kwa kutumia kikombe cha udongo huku kikombe cha Plast amekuwa akitumia kugawia dawa hiyo ambayo huiweka katika ndoo kubwa ya lita 60 huku kwa sasa wagonjwa wakipewa dozi hiyo bila malipo yoyote.
Kwani tayari amepata kutumia dawa hiyo kwa muda mrefu sasa kutibu wagonjwa waliokuwa wakisumbuliwa na magonjwa sugu na tayari wengi wao wamerudi kushukuru baada ya kupona na kuwa bado anaendelea na uchunguzi ili kujua kama kweli dawa hiyo inaweza kutibu UKIMWI kabla ya kuutangazia umma.
“Naomba sana wagonjwa wangu wanaofika kupata kikombe ambao wanatumia dozi za UKIMWI kwa sasa kuendelea kutumia dozi hizo ….hadi serikali itakapo tuma timu ya madaktari kuja kuchunguza dawa hii na kujua idadi ya magonjwa inayotibu kama na UKIMWI upo”
Mwandulami alisema kuwa bado anapenda kuikumbusha serikali kuwa makini na utitiri wa vikombe vinavyoendelea kutolewa na kuwa wengi wao ni matapeli ambao wanafanya hivyo kwa ajili ya kujipatia utajiri wa haraka haraka na sio kuhudumia jamii kama ilivyokwake na babu wa Loliondo.
“Mimi huyu babu wa Loliondo ni kama amenifunua kwa kiasi japo mimi na yeye bado mimi ni mkongwe zaidi yake na uhuhuda wa wagonjwa wanaofika kupata tiba hapa na wale waliopatiwa tiba ni ukweli zaidi ya wale wa Loliondo ambao hata miezi mitatu haijamalizika….mimi hapa nimeanza kutoa huduma hii miaka zaidi ya 17 sasa ila ambacho nilikuwa nikikosea mimi ni kuchanganya na miti mingine ndio maana wagonjwa walikuwa wakipona kwa kasi ndogo ila toka ijumaa nilipoanza kuchemsha mtii huu peke yake mafanikio makubwa nimeyaona kwa wagonjwa sugu kupata nafuu”
Hata hivyo alisema kuwa dawa yake hiyo haina masharti yoyote zaidi ya mgonjwa kufika na kunywa japo mambo ya msingi kama ya ulezi wa kupindukia na uzinzi si vizuri kwa mgonjwa kuendelea nayo kwa kipindi cha dozi hiyo.
Pia aliishauri serikali kupitia wizara ya afya kutuma wataalam wake kwake na maeneo mengine ambayo vikombe hivyo vimeibuka ili kuchunguza mti huo na uhaali wa dawa hiyo kama ina sifa kama ile ya Loliondo na kuiruhusu kusindikwa katika chupa ili wagonjwa wengi waweze kuipata pale walipo popote nchini badala ya kutumia gharama kubwa kusafiri hadi Loliondo ama kuja Wilayani Njombe .
“Huu ni wakati wa matapeli kujiinua na kama serikali haitakuwa makini na kubariki haraka haraka kama ilivyo kwa kijana wa Mbeya basi kuna uwezekano wa watanzania kuendelea kupoteza muda wao na kuibiwa na watu hao ambao baadhi yao wameibuka na kudai sasa wanatibu kwa majani ya mahindi jambo ambalo ni utapeli wa wazi “
Pia alisema kuwa dawa hiyo ambayo amekuwa akiitoa inaweza kuhamishika na mgonjwa sehemu yeyopte nchini anaweza kuipata na kuwa mtabibu ambayo anadai kuwa dawa yake haihamishike kama babu wa Loliondo ni wazi kuwa kuna mkono wa ushirikina katika utoaji wa huduma hiyo.
“Hivi Mungu alipomtuma Mwanaye Yesu kristo kuja duniani kuwakomboa wanadamu wote ni sio wa kabila na koo ana mkoa Fulani …..Kwani Mungu alimtuma Yesu kuifanya kazi hiyo sehemu moja peke ….mbona alizunguka mijini na vijijini kuwahubiria injili wanadamu wote bila ubaguzi …sasa huyo babu anataka kusema Mungu wake yeye ni yupi ni Mungu wa wanadamu wote ama ni Mungu wa Loliondo pekee” alihoji Mwandulami
Mwandulami alitaka watanzania kupima na kuchuja mambo kabla ya kuamini na kuwa ni wakati mzuri sasa kujiuliza maswali juu ya vikombe hivyo na kuwapuuza wanaodai kuwa vikombe havihamishiki wakati wao wamehamisha mizizi toka porini hadi katika makazi yao.
Alisema dawa yake imekuwa ikitibu kwa siku tatu baada ya kumaliza dozi ya vikombe vitatu ambapo kila mwezi ni kikombe kimoja na kuwa kwa sasa bado hajapanga ni kiasi gain kwa mgonjwa aweze kulipia ila mbele ya safari kila kikombe kitakuwa shilingi 2000.
Jamani muwaonee huruma wananchi.yaani vikombe viko Tanzania tu.dah .umasikini kitu kibaya sana
ReplyDeleteMganga wa kienyeji huyo na nadhani ni tapeli fulani.
ReplyDeleteAnkal Hadithi za vikombe tumesha zichoka ukizipa zipotezee tu maana sasa inakuwa maudhi na watanzania wanaonekana wamekosa imani. Kama wanaweza kuyumbishwa na vikombe je kwenye siasa si ndio inaonysha jinsi walivyochanganyikiwa hawajui waende wapi?
ReplyDeleteJamani, huu ni utapeli dhahiri. Hivi ni kwanini serikali inafumbia macho mambo haya? Tutafikia mahali ambapo kila nyumba itakuwa na mtu anatoa kikombe. Tupambane na utapeli na ujinga huu.
ReplyDeleteI think something have to be Done...., this is too much jamani. Kitu kikishaingia mwilini mwa binadamu ni vigumu sana kukitoa. Sasa tutanyweshwa sumu.
ReplyDeleteKila dawa kikombe mizizi na zile poda poda ndio basi tena.
ReplyDeleteDuh! sasa hii imezidi sasa watu wanatumia udhaifu wa wananchi kutengeneza pesa, huyu jamaa anaonekana msanii kabisa
ReplyDeleteEti "mbele ya safari kikombe kitakuwa shiling 2000" !!!. Huyu jamaa ameshapanga plani ya biashara. Kwanza anaanza na dozi ya bure kwa ajili ya kuvutia wateja na kuwapa imani... halafu baadae ataanza kutoza shillingi 2000 kwa dozi. Kumbuka dozi zake ni vikombe 3, kwa hiyo ni shill 6000 kwa matibabu. Tofauti na babu wa Loliondo, huyu jamaa ana mpango wa kusambaza dawa zake nchi nzima....sasa sijui atafungua pharmacy kila mkoa.... hio juu yake, lakini inaelekea huyu plani zake ni kali zaidi na zikienda vizuri ataongeza ghorofa hapo nyumbani kwake... wananchi kuweni macho
ReplyDeleteMwandishi wa article hii umetaja mikoa ikiwemo na mkoa wa "Vuruma"je?huu ni mkoa gani??au ni mpya umeanza juzi??naomba kueleweshwa.
ReplyDeletemdau Usa.
Ninachoshukuru ni kwamba kwa mtu yeyote mwenye akili na macho ya rohoni atakuwa anaanza kuona uongo wa mchana kweupe wa ibilisi kwa kuwa yeye ni baba wa uongo, ulio nyuma ya vikombe vyote kuanzia cha babu wa loliondo mpaka hiki.Ndugu zangu ibilisi ana uwezo wa kufanya miujiza ambayo inaweza ikateka maelfu ya watu kama ilivyo kwenye vikombe hivi. kumbuka jinsi wachawi wa farao wa misri walivyofanya miujiza nyakati za musa. Dawa ni moja tu ni toba ya kweli na kuacha dhambi. Dhambi ni ugonjwa ambao hakuna kikombe kinaweza kuutibu na ndio chanzo cha mahangaiko mengi ya wanadamu.
ReplyDeleteHaya suppliers imebaki mitaa ya KIGOMA changamkieni tender, mtu ajioteshe chapchap aanze kukusanya ulaji. BONGO KAZI KWELIKWELI!!!! Daktari naona mshahala wake haulipi ameamua kuanzisha kajibiashara. Demand ipo, why not?? Zikusanye Doc waswahili wanasema " wajinga ndio waliwao"
ReplyDeletei pity our people. this is a phenomenon of the dearth of our health system. pity too that the leadership does not see it as challenge but are also busy stepping over each other to get to the front line for such quack medical service. one day the peiople will awaken; ala Tunisia!!
ReplyDeleteJAMANI JAMANI WATANZANIA TUTUNZE HESHIMA YETU - TUMESHAKUWA GUMZO BAYA KWA WENZETU MAJIRANI, NA HUKO NJE KAMA KUNGEKUWA NA INDEX YA UCHAWI NA UJINGA BASI TANZANIA TUNGERIKUWA NAMBARI WANI 1.
ReplyDeleteSASA HAPA UINGEREZA NA MAREKANI UKISEMA UNATOKA TANZANIA, HAWAKUULIZI IWAPO MT. KILIMANJARO IKO TANZANIA; BALI WANAKUULIZA JE NI KULE KWENYE WACHAWI WENGI WANAOVUNA NGOZI ZA ALBINO NA DAWA ZA KIENYEJI; PIA WANA OFIA SISI HATUNA DINI TUNAAMINI MILIMA NA USHIRIKINA.
UKIENDA KENYA NA UGANDA NDIO HAWANA MBAVU. WATANZANIA WACHAWI WACHA.
ALEX BURA
Watu wanasema kikombe cha babu hakiponyi. Lakini wakianza kutangaza dawa zao wanaasema "ETI NI KAMA YA BABU WA LOLIONDO"
ReplyDeleteWatanzania tuache wivu na roho mbaya. Hata kitu kilicholetwa na Mungu mnakitukana halafu mnadai sisi tuna bahati mbaya.
MTANZANIA ANA SIFIKA KWA ROHO MBAYA!! HATA VIONGOZI WA DINI WANAONGOZA KWA ROHO MBAYA NA WIVU. ETI BABU NI SHETANI.... KUMBE WANAONA WAMEPIGWA BAO....
Tapeli jingine! Wote hawa wanaojifanya wanatibu kama babu ni wasanii tu, sijui WaTZ wanamatatizo gani? Kila anayeibuka wao wamo tu..
ReplyDeleteBaadhi ya wabongo maubongo yao mazito sana au ukosefu wa knowledge. Huyu kaanza kutoa dawa ijumaa iliyopita leo unasema umepona ukwimi. Kama sio ujinga ninini? Hata kama umekwenda kupima that is too soon to prove kuwa umepona. Hivyo virusi saa nyingine vinakua vinajificha kutokanan na dawa. Naio maana wanakwambia kupima ukimwi sio mara mja tu bali ni mara mbili tatu kwa muda fulani ili ujue kweli huna virusi. Na kama ulishakuaa navyo ndugu yangu ukweli unabakia pale pale vinapungua tu mpaka kuna saa havionekani kabisa kutokana na dawa. lakini ukiacha dawa vitarudi tena muulize magic Johnson alikua anahsjiwa siku moja akasema dawa anazotumia ukipima hutaona kabisa kuwa ana ukimwi lakini ni kuwa bado anao akiacha dawa basi vitarudi.
ReplyDeleteElimu muhimu
Nyie ambao mna afya njema Mshukuruni Mungu lakini Msikufuru. Mtu yeyote anaweza kujifanya mjajna akiwa mzima. Msisahau mithali isemayo " Usitukane Wakunga". Mimi namwamini Mchungaji Mwasapile na Nimeona Majirani wasiopungua watatu waliopona Kabisa. Mmoja kisukari, mmoja vidonda vya tumbo na mwingine ukimwi.
ReplyDeleteHawa wengine ni waganga lakini Babu wa Loliondo ni mtumishi wa Mungu. Kuna watu wahubiri na viongozi wa dini wanaompinga Babu na wanasema maombi yao wanatosha. Mimi nimeona wengi wakiombewa hapa Dar Makanisani wenye ukimwi na wengi sana tumewazika. Mbona hatukashifu maombi.
Wahubiri acheni wivu!
Kikombe hapo, kikombe pale, kikombe kila kona. Yaani sasa ni utani. Ngojea kuna siku utasikia watu wamekunywa sumu!
ReplyDeleteEmbu huyo mdau aliyeandika Kenya na Uganda akanushe kauli yake, Kenya na Uganda baadhi ya ndugu, watoto, wazazi wao wameponea kwa babu sasa kama uchawi kwanini wawaachie watu wao na pia babu anachemsha mizizi na maji na kuwapa sijaona indication ya uchawi ila kumbuka imani yako ndiyo inayoponya if you feel like is danger to you it shall be, but mind you there are many Tanzanian here in UK wamebadilisha hata kusema na kujifananisha na Waganda na Wakenya eti wanaogopa kuonekana Wtz wajinga na wachawi but remember wao ni maskini kama sisi na tena serikali yao ina matatizo kuliko yetu so hawana mvuto kwangu. Imani ya Watanzania inayumba sana na hii imenionyesha kuwa ndo maana watu wengi wanahama makanisa kila mara wakidhani kuna kanisa litaenda Mbinguni, Ndugu kanisa halitufikishi mbinguni Imani na matendo. Eti wazungu wa Uk wanatuita wachawi sijaisikia hiyo we mdau ni muongo wape map ya Tz waende kwa babu maana wengi wana Cancer? Miti mingi ndo inatengenezwaga dawa kuna mti unaitwa quinine ile dawa ya malaria. Kama wewe unafuatana na Wakenya na Waganda wakikudanganya kwa wivu wao usiandike tena ishiye kwenye vikao vyenu
ReplyDeletewatanzania fungueni macho, AMKENI NYIYI, acheni kutapeliwa hii tena too much bado tu munangangania vikombe, waekeeeni mikwala hao watawafilisi kila mukijipeleka kwa wingi ndio munawapa nguvu. mutapewa sumu nyinyi AMKENI
ReplyDeleteHII KALI DUH!!!!
ReplyDeleteplausible effect watu wanapona it has been proven watu wakiamini dawa kutoka hospitalini hata kama sio za kutibu ugonjwa fulani kuna baadhi ya watu wengi wanaweza kupona wakipewa dawa ambayo ina maji tu ili wapone labda kisukari. Lakini hii siyo kwa kila mtu ndo maana baazi ya watu wanapona na mtindo wavikombe na wengine hata wazunguke kwa vikombe vyote hawata pona unless dawa iwe ni tiba sahihi.
ReplyDeleteWABONGO KWA KUCOPY VYA WENZAO ... KA WACHINA BANAA! .... BUNINI VYA KWENU, NDIO MAANA HATUENDELEI! ... MTU AKIFUNGUA DUKA MTAANI, ANAPATA NA WEWE UNATAKA UKAFUNGUE DUKA HAPO HAPO! (SAMAHANI KAMA HIVI VIKOMBE VINATIBU KWELI ILA MI NAONA NI UTAPELI TU BAADA YA KUONA WATU WANAENDA KWA BABU)
ReplyDeleteWIZI MTUPU
ReplyDeleteNinyi mnaosema vikombe vinahamishika mna matatizo. Maelekezo anatoa Mungu siyo nyinyi. Mungu alimwagiza Naamani akajichovye mara saba kwenye Mto Yordani. Yule Naamani akaanza kudai kuna mito mizuri zaidi huko kwao Ashuru. Nabii akamwambia Mto ni Yordani. Watu Bwana kama Mungu anawajua ninyi mbona hakuwaletea hiyo dawa ninyi.
ReplyDeleteDawa hii itazidi kufanya kazi na wazungu sasa hivi wanakuja kibao. Nimesikia viongozi wakuu kutoka nchi za nje wameomba kuja Loliondo.
Ndiyo hapo mtakapoumbuka
This is too much now! AFu inaonesha wazi jinsi gani wabongo tusivyo wabunifu yaani kuigana tu.
ReplyDeleteHivi hawa waganga walikuwa wapi mpaka Babu akaanza kugawa dawa nao ndo wanafwata? wameona babu anafaidi sana eee! Hebu muone huyo kwanza ni mganga wa kienyeji..... alafu ni lazima watumie format ya mtumishi Mwasapile ya kikombe?
ReplyDeleteNa wananchi nao wakisikia kitu wanaenda sijui wanaona ni sifa
Sipendiiiiiiiiii
Mdau Usa river
Huyu ni mganga wa kienyeji na anafahamika ukanda mzima wa Nyanda za juu kusini. Ni mchawi pia na anao vijana wake kadhaa. Kwenda kwa huyu ni sawa tu na kwenda kwa babu wa Bagamoyo.
ReplyDeleteNadhani Dr. yuko sahihi niliwahi soma makala fulani hapa au pahala pengine akidai kuwa kuwa ile dawa ni ya kawaida inajulikana na waganga wengi tu akiwemo yeye. Na hawakuweza kuitangaza kwa sababu ya kizuizi cha kisheria. Na alidai mti ule ni dawa inayoweza kutolewa na mtu yeyote yule bila yale masharti ya ziada yaliyoongezwa na babu Ambilikile.
ReplyDeleteNadhani Dr ameamua kufanya advocacy kwa vitendo ili serikali ijuwe kuwa inachofanya kwa Ambilikile inapaswa kufanya na kwa waganga wengine pia. Go ahead Dr tena kwa vile napendelea dawa za mitishamba nikiumwa nitakunywa yako na si ile ya ambilikile iliyoongezewa masharti eti ndoto ya MUNGU.
Mdau Belgium
Kigoma ,Kasulu eneo linaloitwa folkland kuna jamaa mmoja kama sikosei ni mtu wa kagera naye kaja na kikombe kwa mia tano tu,si haba angalau anapata watu saba ama nane kwa siku,wakifika waandishi na kumtangaza najua biashara yake itachangamka.
ReplyDeleteHeti dawa inaitwa MAKHIRIKIRI,huu ni U TP,ili jina la Makhirikiri si ni wale WATSAWANA waliokuja na bendi yao juzoi juzi,sasa ilo jina alibatiza kabla ya bendi kuja au baada ya bendi kuja,au labda hiyo dawa inatoka Botswana?
ReplyDelete