
Libeneke la NMB FARAJA
Leo Benki ya Jamii ya NMB imezindua rasmi huduma ya bima iitwayo NMB Faraja inayowapatia wateja wa NMB Personal Account Tsh: 600,000 pale mteja atapopoteza mwenza au ikiwa wote wawili watapoteza maisha basi warithi watapata Tsh: 1,200,000/= bure.
Uzinduzi wa NMB Faraja ni muendelezo wa mkakati wa NMB wa kuboresha huduma zake na kuwapa wateja wake manufaa zaidi ya kuwa wateja wa NMB.
Hadi sasa NMB inaongoza kwa kuwa na mtandao mpana zaidi wa matawi zaidi ya 139, Zaidi ya ATM 400 na wateja wanaopata huduma za kibenki kupitia simu maarufu NMB mobile wanaokaribia 500,000.
Afisa Biashara Mkuu wa NMB Kees Verbeek akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa African Life Assurance Julius Magabe na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NMB Imani Kajula wakizindua huduma ya NMB Faraja leo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa NMB Faraja Afisa Biashara mkuu wa NMB Kees Verbeek alisema ‘’NMB inajivunia wateja wake na pia inatoa kipaumbele katika kuwa karibu na wateja wake wakati wa shida hususani wanapopoteza wapendwa wao, NMB ni Benki inayojali wateja hivyo NMB Faraja ni chagizo jingine la lauli mbiu ya NMB ya kuwa benki yako’’
Afisa Mtendaji mkuu wa African Life Assurance Julius Magabe alisema’’African Life inaona fahari kubwa kushirikiana na NMB katika kutoa huduma na hususani huduma ya NMB Faraja’’.
Akizungumza kuhitimisha uzinduzi wa NMB Faraja Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NMB Imani Kajula aliwataka wateja ambao hawajatumia akaunti zao uda mrefu kufufua akaunti zao za Personal Account ili wapate faida za NMB Faraja.
Sasa wateja wa NMB Personal Account sio tu wanaweza kutumia mtandao mpana wa matawi, ATM, NMB mobile na Benki ya Jamii pia wataweza kupata mkono wa pole wakipoteza mwenza’’.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...