Mwenyekiti wa Kongamano la Pili la Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dr. Kitila Mkumbo (katikati) akiwa kwenye meza kuu wa watoa Mada katika Kongamano hilo ambao ni Jaji Mkuu Mstaafu,Barnabas Samata (kushoto) pamoja na Ndg. F. Kiwinga.Mada kuu ya leo ilikuwa ni Kujadili hukusu Maudhui na Misingi ya Katiba Mpya.Kongamano hili limemalizika mchana huu katika ukumbi wa Nkuruma ndani ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mwasisi wa Mageuzi Nchini na Mwanachama wa CHADEMA,Mabere Marando akizzungumza katika Kongamano hilo.
Mwenyekiti wa Chama cha UDP na mbunge wa Magu Mh. John Cheyo akizungumza katika Kongamano hilo.
Dr. Sengondo Mvungi wa NCCR-Mageuzi nae alizungumza katika Kongamano hilo lililokuwa likijadili mada ya Maudhui na Misingi ya Katiba Mpya katika nchi yetu hii.
Naibu Katibu Mkuu wa CUF-Tanzania Bara,Julius Mtatiro akizungumza katika Kongamano hilo la Katiba Mpya lililomalizika mchana huu katika ukumbi wa Nkuruma,Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA,Freeman Mbowe akizungumza na Mmoja wa wanachama wa Chama hicho,Mabere Marando.
Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake nchini (TAWLA),Bi. Maria Kashonda akichangia mada zilizokuwa zikitolewa katika Kongamano hilo leo.
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA,Freeman Mbowe akichangia mada.
Umati wa watu uliofika katika ukumbi wa Nkuruma ili kufanikisha Kongamano la pili la Katiba Mpya leo.
Kutokana na ukumbi wa Nkrumah kufurika, wadau wengine ilibidi wajikusanye kwenye gari hili ambalo lilikuwa na TV zilizokuwa zikirusha live Kongamano hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. HELLO, I AM SEARCHING FOR THE MONTHLY PRESIDENTIAL SPEECH FROM STATE HOUSE. PLEASE,IF THERE IS ANYONE WITH THE LINK CAN HELP WILL BE APPRECIATED
    Thank you very much
    Mdau USA

    ReplyDelete
  2. nafarijika kumuona kamanda Safari(Prof) akiwa tayari ndani ya gwanda, chadema mwendo huo huo

    ReplyDelete
  3. haya mambo hayawezi kufanyikia sehem nyingine mpaka iwe hapo udsm?mbona tupo nchi za watu na tunasoma vyuo vikuu hatujawahi kuona hayo mambo yana fanyika vyuoni?hakuna sehem nyingine zaidi ya hapo?naweza nikajiuliza mambo mengi hata jibu sijapata viongozi wa siasa hapohapo sasa hata sielewi inamaana hizo siasa ndio sehemu yake ya kupata umaarufu wa mtu hapo?

    ReplyDelete
  4. Anonymous wa 06:16:00pm, Inategemea mkuu wangu, mimi ni USA na chuoni kwangu nimeshuhudia midahalo mingi ya kijamii, Kisiasa, Kiuchumi na Kitaaluma ikifanyika chuoni kwangu na nimeshiriki kuandaa baadhi ya hiyo midahalo. Sasa kama chuoni kwako haifanyiki isiwe kigezo cha kukosoa hayo yanayofanyika Mlimani. Pia nafasi ya wana taaluma na wanazuoni katika masuala ya kikatiba ni muhimu sana.
    Sio kwamba nasifia UDSM ni kitovu cha wanazuoni Tanzania hata kama sifa imeanza kupotea lakini kumbuka kwamba miaka ya sabini, UDSM walikua ni school of thought ndio maana hadi leo unawakuta watu kama kina Issa Shivji wanajulikana kimataifa.
    Au ndugu yangu ulitaka mdahalo ukafanyikie CHUO CHA SANAA BAGAMOYO au Mlimani City KAMA VILE MKUTANO WA WAWEKEZAJI?
    Mdau USA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...