

Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Huyu Daudi anastahili apongezwe, maana amekubali kuhatarisha maisha yake kwa mpanda baiskeli!!
ReplyDeleteNashukuru Mungu hakuna aliyekufa, kama kweli Traffic wanfanya kazi hii ajali isngetokea kwani hilo gari ni bovu halifai hata kuwa barbarani. Huu umaskini wetu utatufikisha mbali sana. Sasa Traffic hapo anaandika kitu gani wakati kama hilo gari lingekaguliwa lingekuwa halipo njiani. Nadhani sasa tumefikia mhali pabaya PESA kwanza UHAI baadae.
ReplyDeleteNilishuhudia ajali hii ambayo imesababishwa na ubovu wa lori lililohusika. Gari hilo halikustahili kuwa barabarani na ni matumaini yangu vyombo vya dola vitachukua hatua muafaka. Cha kusikitisha na kuogopesha ni kwamba yapo malori mengi sana ya aina hii Dar es Salaam na sehemu nyingine nchini.
ReplyDeleteKwa kweli hii ndiyo hali halisi ya nchi yetu; ambayo hakuna kujali ubora na viwango vya vyombo vya usafiri wala isiyojali wala kuthamini maisha ya raia wake.
ReplyDeleteMimi binafsi nilishawahi kutahadharishwa mara kadhaa na watu wa karibu kuwa ukiwa Dar unapoendesha ukiona haya malori makubwa ya mizigo yamekaa nyuma yako jaribu kuhamia upande mwingine; maana yanakuwa hayana breki. Hii nilikuwa naona kama ni utani; lakini sasa nimethibitisha kwa hii ajali.
Magari kama haya ukiyaona tu hata kwa nje; hayatakiwi kuwepo barabarani; kwani hayako 'ROAD-WORTHY'.
Hii inasikitisha kwani wadau mnaweza kuwa mashahidi hapa;ukiwa Morogoro Road utaona ndiyo yaliyo mengi yanafia njiani na kusababisha foleni; huku utamwona Traffic anakuja na kupita zake; wakati mwingine baada ya kupoozwa.Sijajua nini maana haswa ya askari wa usalama barabarani; kwani imeshakuwa ni tabia kwamba wao huwa wanasimamisha watu na kuwatafutia vikosa vidogo vidogo na badala ya kuangalia vile vitu vinavyohatarisha usalama wa watumiaji wengine wa barabara.
Askari atakuuliza; tairi zako zinakaribia kwisha; hata kama bado; Huna fire extinguisher nk nk nk.Kero kem kem. Lakini cha ajabu huwa wanapoingia kwenye magari kama haya yanayoonekana kusababisha ajali za namna hii; huwa hawachukui hatua zinazotakiwa ili kuepusha maafa zaidi.
Kwa kweli vyombo vya dola havifanyi lolote kuepusha maafa kwa wanachi; zaidi sana wanatumia mianya iliyopo kutengeneza kula zao.
Utapanda daladala; unasimama mara unashangaa mguu unadidimia chini ya bati; na kiatu kinachanika. Ukiangalia; daladala linatembea; bodi imeoza; ukitazama kwa chini unaona lami.Lakini gari hii hii inachukua abiria.Ukifika kwenye dashboard; hutaamini kama hiyo gari inatembea.Ama kweli; vitu vingine hatuhitaji kuonyeshwa; hata kipofu kwa fimbo yake atatambua;sasa sijui polisi wa traffic wanasubiri nini?
Kwani kusimama barabarani tu na kukusanya za mfukoni ndio wajibu?Hii ni aibu.
Kwa nchi za wenzetu; hilo gari hapo juu hata Scrap Yard haliwezi kuwekwa!!! Ni Hazardous!
WITO KWA DOLA! TUAMKE! KAGUENI MAGARI YOTE YASIYO NA VIWANGO VYA KUWA BARABARANI NA YAFUTIWE LESENI ZA USAFIRISHAJI. NAMNA HII HATUTAFIKA.
Ingekuwa ni gari nyingine ya abiria imegongwa na hilo lori kweli leo hii taifa si lingekuwa linazungumza mengine?
Mungu ibariki nchi yetu; Tuopoe na Wala Rushwa; Tuweze kutimiza wajibu wetu!!
Hili lori tayari lilikuwa mkweche maana badala ya nguzo za umeme kuumia ni lori-mkweche ndilo limepata maumivu. Hii ina nikumbusha gari zilizochoka za kubebea ndizi kule migombani.
ReplyDeleteRejeta ndiyo hilo dumu la njano ndani ya cabin ya lori! si bure likiwa halina breki!
ReplyDeleteHUyo anaonyesha alikua anaspeed tu.. Mbona kama ni residential area hapo? Kukwepa mtu kwenye maeneo hayo isingekua matata katika maeneo hayo kama angekua anaendesha speed limit ya hiyo eneo..
ReplyDeleteHIVI NI KWELI HII GARI INATEMBEA AU NDIO MAMBO YA APRIL FOOLS DAY?
ReplyDeleteKWA KUIANGALIA HATA MARA MIA NITAKANA KUWA HII GARI INAWEZA KUTEMBEA BARABARANI.
YENYEWE TU ILISHAUMIA KABLA YA KUGONGA!
baadhi kubwa wa traffic wa tz wako barabarani sio kwa ajili ya kukagua magari mabovu na kulinda usalama wa raia bali wako kwa ajili ya maisha yao binafsi ya kudairushwa bila ya haya watanzania ni mungu tu ndiye anawalinda sio serikali kabisaaa
ReplyDelete