ANKAL NAOMBA UPOST HII POST YANGU TAFADHALI.

LEO ASUBUHI YA SAA NNE NA NUSU(TAREHE 5/4/2011) NILIINGIA KWENYE RESTAURANT MMOJA PALE MORROCO, CELAVIE PUB, ALI HASSAN MWINYI ROAD.BAADA YA KULA SUPU NIKAWA NASOMA GAZETI NA MHUDUMU AKAJA NAMI NIKATOA WALLET NA KUMLIPA PESA AMBAPO NILIWEKA WALLET JUU YA MEZA.

DAKIKA KUMI BAADAYE NILIONDOKA PAHALA PALE BILA KUKUMBUKA KWAMBA NILIACHA WALLET JUU YA MEZA,NIKAENDA MMOJA KWA MMOJA OFSINI,NIKAA PALE HADI SAA ZA KULA MCHANA AMBAPO HUDUMA YA CHAKULA IPO PALE PALE,BAADA YA KULA NIKATAKA NILIPE NDIPO NILIPOGUNDUA KWAMBA SINA WALLET MFUKONI.

NIKAENDA MMOJA KWA MMOJA PALE KWENYE PUB MORROCO KUULIZIA LAKINI WAKASEMA HAWAKUONA WALLET KWANI MHUDUMU ALITOA VYOMBA KABLA YA MIMI KUONDOKA NA KUNA WATU WENGINE WALIKETI PALE.

NIMEENDA POLISI KUTOA LOSS REPORT.KWENYE WALLET PALIKUWA NA DEBIT CARD MBILI,MMOJA YA WELLS FARGO BANK NA INGINE CHASE BANK,CREDIT CARD MMOJA YA CHASE BANK,DRIVING LICENCE YA JIMBO LA CALIFORNIA,KITAMBULISHO CHA MKAZI WA CALIFORNIA,BANK CARD YA ACCESS BANK OF TANZANIA,KITAMBULISHO CHA MPIGA KURA CHA TANZANIA,SOCIAL SECURITY CARD YA USA,PESA ALFU 30 NA VITU VINGINE VIDOGO VIDOGO.

TAFADHALI KAMA KUNA MTU KAOKOTA WALLET HII NAOMBA ANIRUDISHIE KWANI HIZO DOCUMENTS ZILIZOMO HUMO NI MUHIMU SANA.

ZAWADI ITATOLEWA KWA ATAKAENIRUDISHIA HII WALLET.MAJINA YOTE KWENYE HIZO DOCUMENTS NI FELIX SONGELAELY MAGANGA,

NA SIMU YANGU NI 0714012536

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Duh pole. Mungu asaidie ipatikane..wangebeba tu hizo pesa wakurudishie other documents.. mi uwa sitembei na such important documents, especially Tanzania..bora huku US unarudishiwa wallet yako hata hawafungui kujua kuna nini ndani au hawachukui chochote. Jaribu kucheck kama hiyo hotel ina camera maybe utamuona aliyechukua au kama uliibeba wakati unaondoka au vipi..

    ReplyDelete
  2. Huyo mbeba box hana visa ya kurudi marekani.. kadi zake tayari zime expire kwahiyo asiwe na hofu.. Kadi ya bank bongo utapata nyingine.. Wewe mbona hatukujui hapa california.. Duh.. Sasa umekimbia kubeba box unabeba zege?? Tangaza kwenye magazeti na kwenye hiyo sehemu uliyopoteza.. WEKA ZAWADI.. SEMA MILIONI NGAPI KWA KURUDISHA HICHO KIWALLET CHAKO..
    GOOD LUCK BRO..

    ReplyDelete
  3. Pole sana be careful na bongo. Si California! By the way, unatembea mitaani bongo na drivers licence ya California ili nini? Uonyeshe watu au? Hizo bank card inaeleweka inawezekana ungehitaji hela lakini driver licence ya nini?

    ReplyDelete
  4. duh pole sana mdau i hope utaipata mbane muhudumu, atatoaje vyombo asiione wallet, ila na we unapenda kula, umeenda asubuhi, ukarudi tena lunch time hahahaha, inaelekea humpatii tip

    ReplyDelete
  5. Pole sana kwa kupotelewa na hizo nyaraka.Lakini kuna kauzembe ulifanya tokea mwanzo. Utatembeaje na Social Security,not only Bongo hata USA? Kama wanatembea na copy za SS card, halafu upo Bongo GREEN CARD unazunguka nayo mitaani(hasa bongo) ya nini? Tukienda Bongo documents za maana unazihifadhi sehemu iliyo salama. Naelewa unaweza tembea na driver licence ambayo ndo kitambulisho chako popote ulipo,lakini hizo documents nyingine zimepotea kwa uzembe wako. Nakuombea urudishiwe japo hiyo Green Card yako. Juu ya hizo credit cards/ATM havijapotea unachotakiwa ni kuwajulisha providers(BANKS) juu ya upotevu

    ReplyDelete
  6. Pole sana ila naamini Mungu atakusaidia utapata docs zako zote.
    Kila la kheri.

    ReplyDelete
  7. Kwani huwezi kupiga simu kwenye hizo bank ulizozitaja na kuwaambia umepoteza kadi ili wazifunge? Na Driving Licence utapata nyingine ukirudi huko California. Wewe kopa hela kwa ndugu jamaa na marafiki hadi hapo utakaporudi Cali uwalipe hela zao. chances za kurudishiwa wallet yako ni ndogo sana unless huijui bongo Darisalam.

    ReplyDelete
  8. pole kaka yangu najua kwa kiasi gani hiyo pochi inakupa stress na haswa ikizingatia kuna document ktk hiyo pochi usikatetamaa mtangulize na mungu akuwezeshe kupata pochi yako achana na watu wengine badala kutoa ushauri mzuri wakuwezakukusaidi wao wanaku-ignore usijali kaka sisi binadamu ndivyo tulivyo kwa baadhi ya watu na wengine ni wivu tu kusikia unatoka marekani roho zinawadunda.Kunamchangiaji mmoja amesema utangaze kiasi cha hela utakayompa mtu atayeokota hiyo pochi hiyo ni wazo zuri kwani mtu akisikia hela nirahisi kurudisha haswa akizingatia hivyo vitu haviwezikumsaidia yeye.nihayo tu nakuombea kwa mungu akuwezeshe upate pochi yako naukipata usiachekuja kutuabarisha hapa kwa michuzi good luck

    ReplyDelete
  9. Kweli box limekua zito...Kama havijaexpire vitu vyako na vilikua vya halali na unacopy zake mambo yote ni mswano utapewa vipya huku USA bila hofu na wala kusumbuliwa mimi nilipoteza wallet huku huku na nilipewa vingine within couple of weeks. Ila unatembea na GC na SS ya nini? Hivyo vya bongo ndio mushiken....Lakini unatembea za documents za USA ukiwa bongo ili iwe nini? Wee mpaka una kadi ya kupiga kura bongo mfukoni you don't need all those other documents ukiwa bongo.

    Hapo juu Califonia wee ni diwani wa kata? Kila mtu umjue wewe ni nani? Acha umbea naona unafurahia kweli mwenzako kupoteza hizo documents kwa vile wewe huna...

    ReplyDelete
  10. utakunywaje chai alafu uache wallet mezani kama kwenu?hilo gazeti ulikuwa unasoma kweli au ulikuwa unasukuma time?
    Bongo mfokoni wanaiba sembuse hiyo ulioweka mezani?Tangaza dau acha mchezo coz ni uzembe wako ili iwe fundisho!!
    Sikulaumu braza ila ndo uweke historia kuwa na wewe yalishakutokea

    ReplyDelete
  11. Pole sana kaka Maganga. Kwa kweli huyo mwenye restaurant anastahili kumhoji huyo mhudumu. Hizo documents ni muhimu si uwongo, bora wachukue pesa. Documents haziwezi kuwasaidia. Ukiwa Bongo lazima uwe mwangalifu sana. Lakini hata hapa USA lazime uwe makini, mimi juzi nilikuwa pickpocketed hapa Boston. Mwizi alikuwa mwanamke mweusi kama miaka 50 hivi. Nilimwambia atakufa papo hapo asiponirudishia wallet yangu. Alirudisha!

    ReplyDelete
  12. OOh jamani hivi kweli tunajua kufariji au tunatania, ni kweli ukitoka kwenye nchi za wenzetu zenye ustaarabu na kamera unajisahau sana ukifika Tz, ukweli Tz asilimia kubwa wanamjua Mungu ila si waaminifu.
    Ila kama imeokotwa na mtu mwema atarudisha i hope utaipata tu usijali. Mungu atakusaidia kumpata msamaria aliyeokota. Wadau kuna tofauti kubwa kuandika Mungu kwa herufi ndogo na kubwa, mungu wa dunia tunatumia kaherufi kadogo, Mungu aliyeumba mbingu na nchi na vyote vilivyopo tunaandika herufi kubwa so iweni makini.

    ReplyDelete
  13. Mangi wa KiboshoApril 06, 2011

    Unaweka wallet mezani? uzembe wa hali ya juu.
    Anyway, vutu hivyo uatapata wenga matangazo tu pale bali fedha huwezi pata kabisa

    ReplyDelete
  14. Wewe kweli wa kuja utatembea na kadi zote hizo za california ukiwa bongo ili iweje.Driver licence ya California,na kadi za benki za california unatembea nazo bongo za nini??? Imekula kwako hiyo

    ReplyDelete
  15. Bro we nenda kwa babu Lolioondo mambo yatakua safi sana watakurudishia. Pole sana

    ReplyDelete
  16. Mimi nafikiri hawa wahudumu wasisumbuliwe. Kuna siku nilienda kula mahali City Centre. Nikakuta wadada wawili wanamalizia kula. Nikaweka Bahasha na Diary mezani walipokuwa nikaenda kunawa. Wale wadada wakaondoka mimi naendelea kusubiri mwenzangu amalize ili nami ninawe, Mara kuangalia mezani sikuamini macho yangu, Jamaa aliyekuwa meza ya pili akachukua fuko la lambo na kuweka bahasha yangu humo pamoja na Diary anaanza kuondoka.

    Nikamuwahi mlangoni akadai eti yeye kaokota baada ya wale wadada kusahau. Ilikuwa kazi kweli kwani watu wengine katka HOTELI walimshangaa na kumzomea ingawa hakupigwa.

    Hivyo yawezekana kabisa kuna mtu aliona umesahau akachukua wala dada wa watu asijue.

    ReplyDelete
  17. Bwana Mkubwa hapo mimi sioni kwa nini uhangaike. hizo nyaraka zote za marekani zinapatikana in 7 days. Kuanzia hizo debit cards za CHase na Wells fargo Bank, Social Security Card. Unajua kabisa taratibu ni kutwanga simu kwa benki zako na wasimamishe hizo kadi.Au ingia kwa Online profile yako kwa hizo bank na uwatumie sms. SMPLE. Na Kwa nini utembee na SOCIOAL SECURITY CARD wakati namba unazijua.Huo ni ushamba.

    Kama unahitaji mshiko from those american Bank Accounts, Ingia kwa online and do TRANSFER ya mshiko wako then unauvuta kwa benki account yako DAR...tumia teknolojia...Thats simple, acha kulalamika

    ReplyDelete
  18. ACHA KUTAUFTA UMAARUFU WEWE MAGANGA, ULISHAONA WAPI MTU ANAWEKA WALLET MEZANI?, HATA CALIFORNIA WATU HAWAFANYI HIVYO. MIMI NINAONA HUYU JAMAA ANATAKA TU WATU WAJUE KUWA AMETOKA MAREKANI NA YUPO BONGO....HAJAIBIWA WALA NINI, KWANZA SIJAWAHI KUONA MTU ANATEMBEA NA SOCIAL SECURITY CARD YAKE MFUKONI. ACHA MAMBO YAKO WEWE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...