MWALIKO WA WADAU KUTOA MAONI MBELE YA KAMATI YA BUNGE YA KATIBA SHERIA NA UTAWALA BORA KUHUSU MUSWADA WA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA YA NCHI (THE CONSTITUTIONAL REVIEW BILL, 2011)

Kwa mujibu wa Kanuni ya 114(9) ya kanuni za kudumu za Bunge, kamati ya Bunge ya Katiba, sheria na Utawala Bora inawaalika wananchi na wadau wote kushiriki katika mkutano wa kupokea maoni kuhusu Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya katiba ili kupata maoni na ushauri wao kwa ajili ya kuboresha Muswada huo. Mikutano ya kupokea maoni hayo itafanyika tarehe 7, 8 na ikibidi tarehe 9 April, 2011 Mjini Dar es salaam na Dodoma kama jedwali hapa chini linavyoonyesha:


*7 – 8/April/2011 Itakuwa Dar es salaam

ukumbi wa Karimjee Saa 3 Asubuhi


*7 – 8/April/2011 Itakuwa Dodoma

Ukumbi wa Msekwa.


Kwa taarifa hii, wananchi wote kwa ujumla wanaalikwa kushiriki kwenye mikutano hii kwa ajili ya kutoa maoni yao kama inavyoonekana katika jedwali hapo juu.


Imetolewa na:

Ofisi ya Bunge Idara ya Habari, Elimu kwa

Umma na Uhusiano wa Kimataifa

Dar es Salaam

5 Aprili 2011

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Katiba ya nchi ni suala kubwa sana kwani linatugusa sisi sote. Serikali imekuwa ikipigiwa kelele za katiba mpya tokea 1992, Kinachonishangaza hapa badala ya wao kuandaa mchakato from the drawing board wameng'ang'ania maboresho maboresho, halafu ni nini hasa kinachowafanya watumie zima moto kwenye suala hili?, kwa nini wasitoe muda wa kutosha kwa wadau kutoa mawazo yao kuhusu nini kifanyike, kama ni maboresho au kuandika upya na iandikwe vipi?. Kwa nini wanataka kuburuza wananchi kwa jambo ambalo tukiwa makini linaweza fanyika once and for all? kuliko hizi half cooked measures za kudanganyia watoto peremende.

    Michuzi natumai hutabania hii comment

    ReplyDelete
  2. Kuna namna yo yote inayotuwezesha na sisi wa ughaibuni kushiriki kwa kutoa maoni yetu?

    ReplyDelete
  3. Na siye wa ughaibuni tuwezeshe hii. Na hiyo ya zamani ipo kwenye link gani ili tukiisoma tujue nini ni outdated. Sheria twaziona tu mitaani lakini wapi zimeandikwa hatuzijui....

    Tupeni link

    ReplyDelete
  4. This is a very short notice. Hii ni jambo nyeti sana. Mngetupa taarifa muda mrefu...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...