Yaani hii Ankal lazima uiweke kwenye mtandao wetu atiii, yakhe nimejisikia faraja hata sijui kiasi gani, Ankal umenicall live.Nilikuwa kama yule jamaa aliyepigiwa simu na Obama kuulizwa viipi alikuwa benefited na Health Insurence ambayo Wamarekani wameianzisha huko US.

Mzee nakuaminia unatujali wadau, yaani tukikwama kubrowse hata simu unatupigia ili tutatuwe problem inayotupata kuaccess mtandao wa jamii. ahsante sana and keep it up.
Mdau Zenji.
------------------------------------
Mdau wa Zenji,

Timu nzima ya Globu ya Jamii inakushukuru kwa ujumbe wako na pia kuwataka radhi wadau waliopatwa na kwikwi kwa masaa machache kuingia kwenye libeneke. Hii iliyokana na sababu za kiufundi ambazo host wetu huko Marekani amesharekebisha na ameomba radhi kwa hilo.
Ni kwamba wale wanaotumia kiogelea cha microsoft explorer walipata shida kuona ukurasa mzima hasa wakati wa asubuhi. wenye kutumia kiogelea cha mozilla fox waliendelea kupeta sababu kwikwi hiyo haiwahusu. Asanteni wadau wote mliopiga simu ama kutuma email kuelezea kwikwi hio nasi twasema mambo ni mswano kama kawa. Pia nashauri wadau wa-download mozilla firefox kwenye kompyuta zao kwa ufanisi zaidi.
-Michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...