Ankal haya ni mambo ya mwanza jana jioni..
bonge la tangazo kwa wale wa kwa Babuuuu..

Ila kuna taarifa za uhakika kutoka huko zinasema fisi anayesadikika kuwa na kichaa amemvamia mwananchi mmoja na kumng'ata vibaya sana sehemu ya mkono. Majeruhi amekimbizwa hospitali ya Monduli ila kuna dalili atahamishiwa Arusha kwa matibabu zaidi kwani hali yake ni mbaya.

Hivi sasa msako wa huyo fisi umeanza ili auwawe na kudhuru watu zaidi. Habari zaidi zitaletwa kadri tutavyoendelea kuzipata

Sent from my BlackBerry® smartphone.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Huyo aliyeng'atwa itakuwa alimfanyia madhambi babu!! Unafanya mchezo na babu!! Babu haibiwi wala hadhulumiwi..

    ReplyDelete
  2. kingangitiApril 08, 2011

    Oh! pole sana lakini si lazima wamuue huyu ni kumtegea mtego akamatwe apigwe kikombe cha babu hafu akawekwe zuu basi.hafu Ankal cheki hiyo sentensi yako "Hivi sasa.....auawe na kudhuru watu zaidi." imekaaje hapo.Mungu bariki wasitokee wanyama wengine wakali.Kikombe hoyee!..

    ReplyDelete
  3. Kwan babu anafanya biashara!? @ hapo juu

    ReplyDelete
  4. Nimekutana na kituko cha mwaka wiki huu. Rafiki yangu fulani anayesali kwenye kanisa fulani hapa mwenge mjini amekuta wakifanya maombi maalumu kumlaana yule mchungaji wa Liliondo afe. Na wakaomba kwamba viongozi nao waliokunywa dawa hiyo wapatikane na magonjwa mabaya.

    Nimesikitishwa sana sasa hata kama kweli babu ni mganga nani ni mbaya zaidi yule anayesaidia watu wapone au yule anayeombea waliopona wafe. Nimestushwa sana na nasikia wakati maombi haya yanafanyika Tv ya kanisa hilo ilikuwa iko hewani. Sijui yupo mwingine aliyesikia?

    Ndiyo maana tulisema wivu ndiyo sababu ya wengi kumpinga babu.

    ReplyDelete
  5. Anoy Fri-08,07:51:00

    Kweli kumuombea mtu afe sio kitu kizuri.Lakini babu anachofanya ni ushirikina kwa sababu kama mitishamba inatumika miaka mingi kwa kuponya magonjwa tofauti.Na hata hao wanasayansi hutumia baadhi ya miti kwa kutengeneza dawa za magonjwa tofauti.Lakini BABU anatumia nguvu za imani ambayo moja kwa moja ni ushirikina.Haiwezekani kwamba dawa hio isitoke nje au haiwezi kupimwa na wanasayansi kuangalia tiba zake.Na sasa inadhihirisha ya kuwa wananchi wanaamini sana ushirikina kuliko kitu chochote kile na yote yanasababishwa na kutokuwa na elimu hasa ya dini.Kwani kama ndoto wengi tunaota matukio tofauti ambazo ndoto nyingine huwezi hata kuzitafsiri unapoamka.Huyu babu hana tofauti na sheikh Yahya maana yeye hupiga ramli na anaijua dini vizuri kama inakataza kumshirikisha mungu lakini kwa tamaa ya pesa anajisahau.Kwayo hapo huwezi ukasema ni wivu isipokuwa kuna watu ambao hawana imani na dawa hiyo.Mimi namjua binamu yangu kasumbuliwa na sukari tokea akiwa na umri wa miaka 18 na sasa hivi umri wake ni 43 na amekwenda kujaribu kabla ya watu kuwa wengi lakini amejuta kwa sababu hakuna tofauti yeyote na pamoja na wote alioenda nao walikuwa watu 5 na mmoja imebidi aende hospitali baada ya wiki mbili maana ilipanda sukari kupita kiasi.Yaani haya mambo ni ya kuangalia tu kwasababu huwezi kumueleza mtu kitu juu ya hili suala inabidi uwache watu wakajionee wenyewe.

    ReplyDelete
  6. KUMWOMBEA MTU AFE NI SAWA SAWA NI WACHAWI WANAOURUKA NA UNGO NA KUROGA WATU NA KUUWA.

    KANISA NI MAHALI PA WATU KUPONEA SIYO KUUAWA. SASA MAKANISA MENGI YANAYOJIITA YA "KIROHO" YAMEPOKEA MAFUNDISHO KUTOKA NIGERIA YA KUUWA WATU WASIOKUBALIANA NAO.

    ANAYEUA NI WA SHETANI NA ANAYEPONYA NI WA MUNGU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...