Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mkoa wa Mbeya Sambweli Shtambala na Katibu Muenezi wa Chama Hicho Wilaya ya Ileje Heri Kayuni, wakila kiapo cha Utii na kuwa waaminifu kukilinda na kukitetea Chama cha Mapinduzi CCM baada ya kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM na kukabidhi wa Kadi za Chama Cha Mapinduzi CCM na Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Makao Makuu ya CCM Mjini Dodoma leo. Amour Nassor VPO.
Home
Unlabelled
JK awapokea waliojiunga CCM kutoka Chadema Mbeya na wala viapo leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


Hongereni kwa maamuzi yenu ya busara. Ila tunataka CCM ijivue gamba ili iturejeshee imani tuliyokuwa nayo tangu mwanzo. Japo juhudi tunaziona lakini bado ni kasi ndogo bado. JK kaza buti unaanza kujivua gamba
ReplyDeletehawa viongozi wanaohama kutoka chama kimoja kwenda kingine, sijui watatueleza nn tuwaelewe. Mana kwa macho ya kawaida tunajua ni maslahi tu ndo yanayowafanya wasitulie. They have decided to invest in politics na hiyo ndio njia pekee ya wao kuishi. Hakuna jipya. Watahama sana. Ccm itabaki kuwa ccm na chadema the same way. Wananchi wanaangalia hali yao ya kimaisha na sio kuangalia nani kahama kwenda wapi. Haitusaidii.
ReplyDeleteNjaa tu hizi hakuna lolote la kusema wamependa sera za chama tawala nina uhakika hata ukiwauliza kuwa ilani ya chama tawala inasema nini kuhusu elimu watakuwa hawajui. CCM sasa hivi haina sera ya kuwapa ulaji watu wanaohamia kutoka vyama vingine kwa hiyo kama motive yao ilikuwa something then wajue ni patupu.
ReplyDeleteCHADEMA halitushangazi sana hilo. Sambweli Shitambala siku nyingi alikuwa ameisaliti chadema Ni mtu hakutulia hasa baada ya kukosa ubunge. CCM itawanunua wengi tu maana inakaribia kufa.
ReplyDeleteHata walivyokua chadema walikula kiapo hivi hivi na sasa wanakikana, hili jina la "Kiapo" wangelibadilisha kwa wanasiasa maana wanakufuru, utasikia akisema "Nikiwa na akili zangu timamu, naapa kuilinda na kuitetea sijui nini nini..". Sasa kuna mawili, either wakati wa kuapa alikua hana akili timamu kama alivyosema, au wakati wa kuhama anakua hana akili fresh, au vyote before and after.
ReplyDeleteNa Prof. Safari mnemwonaje. Chadema ni ya kabila na dini fulani, watu wameshangamua. Kalagabaho.
ReplyDelete