Suzan Mashibe akipozi na Bw. Vivek Kundra mtaaamu wa Teknohama ambaye aliwahi kuishi Tanzania miaka ya 80 wakati baba yake akifanya kazi ya ualimu huko Korogwe na Dodoma. Hivi sasa Bw. Kundra anaongoza kitengo cha teknohama Ikulu ya Marekani - White House. Hapa walikuwa sillicon valley kutembelea makao makuu ya Google, Facebook na Linkedln baada ya kushinda tuzo ya viongozi vijana wa dunia ambapo kwa Tanzania Suzan na mshauri wa uchumi wa JK, Bi Elsie Kanza walishinda

Suzan akiwasili Indianapolis alikokwenda katika ziara ya kikazi

Suzan akikagua hoteli ya Mount Meru huko Arusha. Anasema kampuni yake hufanya ukaguzi wa aina hiyo ili kuhakikisha wateja wake wanafikia mahali penye hadhi ya kimataifa

Suzan na wafanyakazi wake wakisherehekea miaka mitatu ya kampuni ya TanJet anayomiliki

Suzan akiwa ndani ya basi la Google alipotembela Sillicon valley Marekani

Suzan akiwa kazini

ULE usemi “usitathmini kitabu kwa kuangalia jalada lake ” una maana kubwa unapomzungumzia Susan Mashibe, mhandisi wa masuala ya ndege na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni mbili zinazoshughulika na masuala ya anga, lakini unapokutana naye kwa mara ya kwanza huwezi kuamini kama mwanadada huyo ana sifa hizo ndio maana nikakumbuka ule usemi, ‘usitathmini kitabu kwa kuangalia jalada lake.’ Kuthibitisha uwezo wake mkubwa katika fani hiyo, hivi karibuni Mashibe alichaguliwa na Taasisi ya World Economic Forum (WEF) kuingia katika kundi dogo la heshima la vijana waliothibitisha vipaji vya uongozi la Viongozi Vijana Duniani (Young Global Leader- YGL)) kwa mwaka huu wa 2011. Sambamba na Susan, Mtanzania mwingine Elsie Kanza, Mshauri wa Uchumi wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete amechaguliwa na taasisi hiyo pia kuingia katika kundi hilo. Mashibe na Kanza walichaguliwa kutoka miongoni mwa viongozi vijana 5,000 waliopendekezwa kutoka duniani pote na hatimaye kupitishwa katika mchujo na kuchaguliwa kwenye mchujo mkali na Kamati Maalumu chini ya uenyekiti wa Malkia Rania Al Abdullah wa Ufalme wa Hashemite wa Jordan. Nenda Habari leo upate stori nzima ya mwanadada Susan Mashibe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...