Balozi Peter Kallaghe

JUMUIYA YA WATANZANIA-TANZ-UK ikishirikiana na TA Reading Inapenda kuwakumbushia tena watanzania wote waishio Reading, Slough, Oxford na vitongoji vingine, Kuwa Ziara ya Balozi wetu MH Peter Kallaghe akiambata na Mama Kallaghe Itaanza rasmi siku ya Ijumaa jioni tarehe 8/4/11 na kuendelea Tarehe 9/4/11 Jumamosi ambapo Mh. Balozi Kallaghe atakutana na Jumuiya mbali mbali za Ki-Tanzania, pamoja na kutembelea miradi na Taasisi mbali mbali za KiTanzania.

Wakati Huo huo Mama Kallaghe atajumuika na na akina mama wote Jumamosi kuanzia saa nane Mchana. Kisha Mh Balozi na Mama watahudhuria hafla kubwa iliyoandaliwa na Wanajumuiya kwa ajili ya kuwakaribisha kuanzia saa 16.00 jioni. Bongo DJs watakuwepo wakifanya makamuzi mpaka usiku wa manane. Jumapili 10/4/11 kutakuwa na ibada ya Kiswahili itakayohitimisha Ziara hii ya kipekee.

Kutokana na muitiko mkubwa pamoja na ushirikiano wa hali ya juu kutoka kwa wanajumuia imelazimu kubadilisha ukumbi ili kufanikisha zaidi ziara hii. Anuani ya Ukumbi itakuwa WYCLIFFE 233 KINGS ROAD, READING RG1 4LS. Tunawaomba Radhi wote kwa usumbufu uliotokana na mabadiliko hayo muhimu. Tafadhali mjulishe mwenzako na tuzingatie mda.

Kwa mawasiliano zaidi kuhusu ziara hii tafadhali wasiliana na wafuatao: Ndg. Hussein 07865673756, Ngd. Upete 07796122127, Mama Maria 07919874182.

Asanteni sana kwa ushirikiano wenu.

TANZ- UK / TA READING




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...