KUTOKANA NA WINGI WA HABARI NA TASWIRA IMEKUWA KAWAIDA SASA HABARI AMA TASWIRA KWENDA UKURASA WA PILI AMA WA TATU KWA KADRI HABARI NA TASWIRA MPYA ZINAVYOINGIA, AMBAKO HAIMAANISHI ASILANI KWAMBA HABARI AMA TASWIRA IMEONDOLEWA. NI KWAMBA IMESOGEA TU KWENDA KATIKA KURASA ZILIZO NYUMA.

HIVYO BASI, KWA KUPATA HABARI KATIKA UKURASA WA PILI AMA WA TATU NA HATA WA NNE NA KUENDELEA, BOFYA MAANDISHI YASOMEKAYO 'HABARI ZILIZOPITA' CHINI KABISA KULIA ILI KUFUNGUA UKURASA WA UNAOFUATA. BOFYA TENA NA TENA KATIKA MAANDIKO HAYO ILI KUFUNGUA KURASA MMOJA BAADA YA MWINGINE, HATA KWA SIKU MOJA TU.

KWA YULE ANAYETAKA KUTAFUTA HABARI KWA JINA AMA TUKIO, ANDIKA HILO JINA AMA TUKIO NDANI YA NAFASI ILIYO JUU KULIA YENYE MAANDIKO 'TAFUTA CHOCHOTE HAPA' NAWE UTAFANIKIWA. MFANO UKIWA UNATAKA HABARI ZOTE ZA CRDB ANDIKA NENO 'CRDB' KWENYE KINAFASI HICHO NAWE UTAPATA HABARI ZOTE NA TASWIRA ZA CRDB ZILIZOMO HUMU. BOFYA 'HABARI ZILIZOPITA' KUTAFUTA HABARI AMA TASWIRA ZA AWALI ZA CRDB UNAZOZITAKA.

TUMELAZIMIKA KUTOA UFAFANUZI HUU SABABU BAADHI YETU TUNAISHIAGA UKURASA WA KWANZA TU KWA KUDHANI LABDA HABARI AMA TASWIRA ZIMEONDOLEWA. KUMBUKA HABARI HAIONDOLEWI BALI INAHAMIA TU KURASA ZINAZOFUATA AMBAZO ZINAPATIKANA BILA TATIZO KWA KUBOFYA 'HABARI ZILIZOPITA'.

VILE VILE LIBENEKE LA GLOBU YA JAMII LINAPATIKANA PIA KATIKA TWITTER, YOUTUBE NA FACEBOOK. UKIANGALIA JUU KULIA UTAKUTA ALAMA YA HUDUMA HIZO. BOFYA ALAMA YOYOTE UENDELEE KULIBENIKA BILA KELELE WALA MIKWARUZO.

LIBENEKE OYE!
-MICHUZI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 18, 2011

    Ushukuriwe ewe Michuzi kwa kutumuvuzishia ufafanuzi...yaani mimi ndo nlikuwa naishiaga kama ulivyosema, yaani nikiwa na haraka ndo kabisaa!!...long live my Friend!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 18, 2011

    Halafu bwana Michuzi..kuna post unazipost kuhusu haya mambo ya 'Maumbile yetu sisi Binadamu'.Jana ulipost moja kuhusu baba mmoja anayetafuta mtoto + blah blah.Mtoa maoni mmoja alisema kwamba usiwe unazipost zile habari kwenye Blog hii manake glob hii inasomwa na Watu wenye Heshima zao.MIMI NAKUBALIANA NAYE LAKINI NINA NYONGEZA KIDOGO..WATU KWELI WANA MATATIZO SOTE TUNAFAHAMU.INGEKUWA VIZURI UKAFUNGUA KAMA KI-FOLDER CHA KUJITEGEMEA KWENYE BLOG KUHUSU HAYO MASUALA HALAFU ANAYEPENDA KUSOMA HABARI HIZO NA KUSHAURI ABONYEZE MWENYEWE HUKO KULIKO KUZIANIKA HADHARANI(NI MAONI YANGU)>UNAWEZA KUWEKA MDAHALO KUPATA MAWAZO ZAIDI.HATA HIVYO TUNAIPENDA BLOG YETU YA JAMII

    David V

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 21, 2011

    Napendekeza "Habari Zilizopita" isomeke "Ukurasa Unaofuata" maana kwa hakika kwenye huo ukurasa unaosema "Habari Zilizopita" huweza kutokea kukawa na habari mpya ila kwakuwa kwa siku hiyo kulikuwa na habari nyingi, za awali kuingia husogea katika ukusara mwingine wa chini. Hii "Habari Zilizopita" inapotosha kwa maana silazimiki kusoma habari zilizopita kama sina haja ya kurejelea hizo habari. Nadhani wengi tulipitwa na habari kwa sababu tu ya kielekezo hiki "Habari Zilizopita".

    Nawasilisha, bila kujeruhi hisia za wengine!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...