Waziri wa Mambo ya nje na Uhusiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe akiongea leo jijini Dar es salaam juu ya fidia ambayo BAE Systems inatakaiwa kuilipa Tanzania kwa mauzo ya Rada kwa bei ya juu kuliko kawaida
Serikali ya Tanzania imepinga vikali uamuzi wa kampuni ya silaha ya Uingereza – BAE Systems wa kulipa fidia ya Pauni milioni 29.5 za Uingereza kwa Tanzania kupitia asasi isiyo ya kiserikali badala ya kulipa fedha hizo moja kwa moja serikalini kufuatia kukamilika kwa kesi ya rushwa ya ununuzi wa Rada.
Mwanzoni mwa miaka ya 2000, Kampuni ya BAE System iliiuzia Tanzanai Rada kwa gharama ya Paundi milioni 41 za Ungereza wakati gharama halisi ilikuwa Pauni milioni 12.
Akitangaza msimamo wa serikali leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe amesema, uamuzi huu unaenda kinyume na msimamo wa serikali yetu uliotaka fidia hiyo irejeshwe serikalini.
“Fedha hizo ziliibwa kutoka serikalini na hazina budi kurejeshwa serikalini,” amesema.
Tamko la Serikali limekuja miezi sita baada ya uamuzi uliotolewa na Jaji Bean wa mahakama ya Southwark ya Uingereza Disemba 21, 2010 kutoa uamuzi kuwa BAE kulipa Pauni milioni 29.5 kwa wananchi wa Tanzania.
Jaji Bean alitoa uamuzi huo baada ya kutorishika na na maelezo ya makubaliano ya Ofisi ya Makosa makubwa ya jinai ya Uingereza SFO na BAE.
Kwa mujibu wa Waziri Membe, kampuni ya BAE system badala ya kulipa fedha hizo moja kwa moja kwa wananchi wa Tanzania, imeamua kuunda jopo litakalojumuisha watu kutoka ndani mwake kuishauri jinsi itakavyotumia fedha hizo kupitia kwa asasi isiyo ya kiserikali ya uingereza na sio kwa serikali ya Tanzania.
“Msemaji wa BAE amenukuliwa na Ubalozi wa tanzania nchini Uingereza akisema kampuni yake inaongozwa na sera ya kutoa misaada ya kihisani kwa asasi zisizo za kiserikali tu. Kwa msingi wa sera hiyo, kampuni hiyo haitaweza kulipa fidia hiyo moja kwa moja kwa serikali ya Tanzania,” amesema.
Waziri Membe amesema kuwa uamuzi hu wa BAE unalengo la makusudi kuonyesha sura ya kutokuamini mpango wa pamoja wa Serikali za Tanzania na Uingereza ulioelezea jinsi fedha hizo zitakavyotumika.
“Serikali ya Tanzania ilikusudia kutumia fedha hizo kununua jumla ya vitabu milioni 4.4 kwa ajili ya shule za msingi, vitabu vya miongozo ya mitaala 192,000 kwa ajili ya masomo 12 katiak shule 16,000, kununua madawati 200,000 kwenye shule zilizo na upungufu wa madawati na kujenga nyumba 1,196 za walimu katika wilaya zote nchini, kujenga vyoo 2,900’ amesema.
“BAE wanajaribu kujikosha mbele ya asasi mbalimbali zisizo za kiserikali za Uingereza baada ya kukosolewa sana kwa kashfa ya rushwa na kutoka sasa kuonekana kwamba inawajali zaidi Watanzania kukliko serikali yetu,” ameseam.
Waziri Membe ameeleza kuwa kampuni hiyo silaha ikikaidi kutoa fedha hizo moja kwa moja kwa serikali ya Tanzania, hakuna asasi isiyo ya Kiserikali ya Uingereza itakayopewa fedah hizo na kuruhusiwa kuja nchini
Kama ni serikali ndi iliyo over pay kwa makusudi; kwa nini BAE na Waingereza kwa ujumla wawe na Imani kuwarudishia fedha msizo na kazi nazo. Mi naona poa tu ela ziende kwa wananchi direct
ReplyDeletePole sana MH Waziri. Hapa twaweza jifunza mambo mengi:
ReplyDelete1. Serikali ya TZ hamuaminiki
2. BAE wanataka pesa zibaki nchini kwao kwa njia ya ununuzi wa vifaa vya kwao.
3. Mkiendelea kulumbana mnaweza mkazikosa hata hizo ambazo mgezipata
4.Mngemchukulia hatua za kisheria waziri mwenzenu aliyehusika, pengine ingeleta imani kidogo kwa hao jamaa na kupunguza malumbano
Acheni kulalamikia hizo pesa,wenzenu waliwategea kuona mtawafanyia nini waliohusika na mpango mzima wa RUSHWA kama Mh Membe ulivyosema lakini baada ya kuona mnawalea na kuwakumbatia so wameona hata wakizirudisha mtazitumia vibaya1!JARIBUNI KUBADILIKA DUNIA HII SI YA KUKUMBATIA UHARIFU TENA,SHUGHULIKIA AKINA CHENGE TUFUNGE MJADALA MTAPATA HATA MISAADA MINGI TU
ReplyDeleteKwenye kesi hawakwenda wahusika pamoja na wakala wa biashara hii hawajawachukulia hatua uchunguzi hawajafanya leo mnasema mnadai pesa yenu mbona hamkuonyesha juhudi za kuifuatilia ili haki itendeke?
ReplyDeleteWadau mimi naona wanachotaka kukifanya BAE ni poa tu hata kama wanataka kujenga image yao. Najua pesa ikirudi kwa njia ya serikali itafanyiwa matumizi yasiyo lazima. Nadhani kupitia NGO faida ya pesa hizi zitakwenda moja kwa moja kwa wananchi tena vijijini...
ReplyDeleteserikali mli-overpay pesa za watanzania kwa BAE na hamkuzidai kwasababu hamna uchungu nazo, BAE wanajaribu kuwarudishia wenyewe (watanzania) pesa zao (japo kidogo) kwani wamesikia wakilalamikia ingawa serikali hamkujali.
ReplyDeleteThe Brain
Mnapinga nini wakati serikali (katika kuteteana)ilitoa tamko huko nyuma kwamba hatujapata hasara? Waacheni watumie njia wanayotaka wao, kwa kuwa ndio waliogundua rushwa hiyo na kulishikia bango suala hilo. Waliohusika hapa bado hawajafanywa lolote. Nadhani ni fedheha na unafiki kupiga kelele sasa hivi wakati wahusika kwa upande wa TZ bado wana madaraka na heshima kwa jamii.
ReplyDeleteunko michu umebana maoni yangu ya capital letters lakini sawa..ukweli ndio huo we ufiche lakini ujue penye moshi hapakosi moto na siku tukiungua wewe utakuwa mmoja wa wachochea moto kwa kubana ukweli
ReplyDeletePole mh.Membe, mie sikubaliani na kauli ya BAE kusema pesa irudishwe kwa asasi zisizo za kiserikali huo ni ujanja wa kutaka KUWATENGENEZEA AJIRA WATU WAO WA UINGEREZA!!! Watanzania sasa tumeamka sio mbumbumbu kama wanavyodhani.
ReplyDeletemimi naishangaa serikali yetu, kwanza waliitetea sana rushwa hii na kuwalinda wahusika hadi leo.Pili hatukuona juhudi zozote kudai pesa hii hata mahakamani hawakufika. Waziri wa Uk alijiuzulu kwa uchungu wa rushwa hii. hapa kwetu hakuna aliechukuliwa hatua zaidi ya kulindwa.Sasa kwenye chenji mnajifanya mnakumbuka vitabu vya watoto na madawati! huu ni unafiki ina maana wakati tina over pay tulikuwa na madawati na nyumba za walimu za kutosha? mbona mlituambia tule hata majani lakini rada na ndege vinunuliwe. Mi naona hata sisirudi serikalini wataishia kununua mashangingi tu.
ReplyDeleteHivi nikuulize we uncle michuzi, kwa nini unabana mawazo ya mtu ingali hata hajatukana ???? au ndiyo huko kujipendekeza ?? au tabia zenu za kuficha ukweli wa mambo na kunung'unikia pembeni (umbea) ....weka maoni yetu be neutral.
ReplyDeleteMNAJUA UTANI UTANI HUU SIKU MOJA TUTAKUJA KUTOANA ROHO...NYIE LETENI MCHEZO TU...NIKISOMA HABARI HII NASIKIA KITU KIMENIKAA SHINGONI KWA HASIRA TUNAUMIA KWA AJILI YA WAPUMBAVU WACHACHE
ReplyDeleteTanganyika ni ya wadanganyika,pesa hii leo ndio ikanunuliwe madawati,wakati wanaitoa hawakufikiria hata walalahoi wao,leo mlalahoi anakumbukwa ili atetee ubadhilifu uliofanywa kwa manufaa yao,hii pesa wakishapata hapatakuwa tena na madawati wala majiwe, watununulia mashangingi(Magari) na kumalizia majumba yao yalio ktk viwanja walivyopeana huko o'bay na masaki ambavyo pia ni mali ya wadanganyika.
ReplyDeleteMungu yupo na wote waliohusika watahukumiwa hapa duniani
You failed your own people to begin with, so I don't see how you are going to do it RIGHT this time. Let BAE handle the money, may be our students and 'poor' teachers will benefit. Mheshimiwa waziri kuzuia kampuni ya nje kuja kusimamia fedha hiyo hakutawasaidia wananchi kwa njia moja au nyingine sana sana itachelewesha maendeleo. What you need ni kuhamasisha kuwa kuwe na ushirikiano katika ukaguzi wa matumizi ya fedha hiyo na si vinginevyo. Pesa hiyo itatoa ajira kwa watu wengi tu (even if it's for short-term).Sioni ni vipi mtu yeyote mwenye akili timamu alitoa P41 badala ya 12!! Kwani hao viongozi waliohusika kufanya maamuzi hayo wamechukuliwa hatua gani?!
ReplyDeleteukweli inaibisha! Lakufurahisha, ni kuwa Serikali yetu si mtu kusema ataaibika au kuona aibu.. Mheshimiwa waziri pole, lakini unafikiria kwa nini wazirudishe serikalini wakati mgao wa serikali ulishachukuliwa? Kwani wadhani waliolisimamia hilo 'dili' hawakujua bei yake? na BAE wanajuaa hilo. kwa hivyo na wafanye wanavyoona inafaa, hadi pale tutakapokuwa na serikali yenye kufikiria uchumi wa nchi na si vinginevyo.
ReplyDeletebae inajulikana kwenye sekta ya rushwa, imefanya dili nyingi mbovu na saudi, sweden na jmhuri ya czech pia. wanancho fanya ni kuhonga viongozi wa nchi husika kama kina nanihii kipindi kile na kupiga kwa bei juu.jana wamepigwa fine na serikali ya obama ya £49millions kwa sababu ya kucheza rafu. link hii hapa http://www.bbc.co.uk/news/business-13421859 ila katika tuhuma zote neno corruption wameliepuka kwa sababu ikiwa declared kwamba BAE ni corrupted, watapigwa ban na EU kuuza silaha nchi husika na hiyo itakuwa ni ishu ya maana. kuhusu kurudisha hizo fedha, hata wakazilipa kesho kw serikali au kupitia taasisi, still hazitaonekana zimefanyia nini. nafkiri tunatakiwa tuamke sasa kwa sababu hii nchi yetu imezidi ubabaishaji. gold tunazalisha zaidi tani 2000 kwa mwaka, almasi+tanzanite+gesi+coal+chuma+utalii= umaskini kupindukia, yaani ukifikiria sana unaeza umwa na kichwa ankal!!
ReplyDeletemdau